Mbunge Susan Lyimo: Kama kweli hostel za UDSM zimejengwa kwa Mil 500, nitatoa hela zijengwe zingine

Mbunge mbululu huyuu, hizo mil 500 tazitoa tu labda haijui serikali vizuri!

ha ha ha ha na jengo lingine tutahenga atashangaa na roho yake!
 
View attachment 510866

“Naomba CAG afanye ukaguzi maalum katika hostel mpya UDSM na kama kweli jengo moja linalochukua wanafunzi takribani 390 linagharimu Milioni 500 basi mimi nitatoa Milioni 500 serikali ijenge jengo lingine la ghorofa tatu ili tuweke vijana wengine”. - Susan Lyimo (Mbunge-Chadema)

Toa maoni yako

Atoe hizo fedha aone kama ghorofa haijengwi.
 
Atoe kuonyesha mfano kwanza na aanzishe yeye kulijenga, bila kusahau kutumia watu walio ktk payroll pia na etc

Naona anachemka tu.

Tatizo liko wapi? Yeye ameomba athibitishiwe kama sh. 500,000,000 ndiyo gharama halisi atoe za kuongezea jengo moja.

Si mtoe huo uthibitisho muone Kama atashindwa?!
 
Hakuna kinachoshindikana.

Kujenga kwa billion kumi ni kitu kinachowezekana kabisa na chenji inaeza kubaki. Ni sawa na kumshangaa mtu anae-survive kwa mshahara wa laki tatu kwa mwezi na ana familia. Wakati wewe una mshahara wa milioni tatu uko bachelor na haukutoshi.

Kama TBA wana ma-engineer wao permanent kabla hata ya mradi, au labda tuseme waongeze wachache kukidhi mahitaji. Posho za vibarua wa Tanzania kila mtu anajua ilivokua aibu hata kuzitaja, japo ndo wanalipwa hivo. Design kuanzia architectural mpaka structural pamoja na usimamizi BICO ya CoET ipo (wasioijua BICO, ni engineering Consulting firm ya UDSM), wana wafanyakazi wanalipwa always wawe wamefanya kazi au lah, na kazi ni ya chuo chao wenyewe ni suala la kutoa maagizo tu hiyo kazi inafanyika.

Ukija kwenye material, Serikali ina share 30% twiga cement, possibility ya kupata Cement kwa bei chee upo. Kokoto na nondo ndio pekee wanaweza kununua kwa bei ya soko. Furniture zote, kuanzia vitanda, makabati yote yametoka workshop za CoET. Kwanini pesa hiyo isitoshe.

Katika mfumo wa kawaida architect atatafutwa atafanya kazi na bado atasimamia. Structural engineer atafutwa na atasimamia kazi, Contractors watatafutwa kuanzia structure yenyewe mpaka services zote (maji, umeme n.k) hapo wote inapaswa wafanye kazi kwa faida na wahakikishe pia wanakuepo site muda wote wanaohitajika. Hapo bado misunderstanding kibao zinazosababisha mradi uchelewe.

Tatizo la nchi hii ni moja tu, haijulikani imeegemea mfumo gani kama ni ubepari au ujamaa. Na kamani vuguvugu basi ijulikane, ili kila mtu kuanzia raisi mpaka housegirl ajue hilo na wote tuishi na kuzoea aina hiyo ya maisha. Ili kusudi kiongozi akija kivingine tumshangae wote kwa Pamoja. Lakini saiv hatujui tuko upande gani, makampuni mengine yanafunga biashara kwasababu wakati wanakuja waliamini sisi tunaelekea kwenye ubepari, sasa raisi Mjamaa kaja hawana chao tena, sharti wafunge virago.

JK aliendesha nchi kipebari na yale yote yaliyotokea katika utawala wake yalitokana na mfumo huo. Kaja JPM nchi inaenda kijamaa na matokeo yake ndo haya mambo yanafanyika kijamaa ile pesa iliyokua inatakiwa iingie kwenye mifuko ya watu inaenda kwenye real things. Hapo lazima watu walie tu.
Analysis nzuri na kwa vigezo hivyo inawezekana ila sasa hapo kuweka record sawa ni vyema kutambua nguvu kazi iliyotumika kwa kuithaminisha hata kama haijalipwa ili kupata thamani halisi ya jengo kwa hali ya kawaida (kuna madhara yanaweza yakatokea mfano matetemeko au vimbunga alafu majengo yamekatiwa bima ya thamani hiyo si itakuwa majanga kwenye kulipa)
 
Susan ana bahati anatoka upinzani, angekuwa anatoka tawala angeitwa msaliti na kutumwa India kwenye matibabu! Kweli hosteli zile ni abracadabra!

Katika chama chetu huu ni uchochezi unastahili kujiuzulu mara moja kuna kila dalili umeshindwa kwenda na kasisi ya mtakatifu yuleee.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Mkuu wanaweza wakajenga hizo ghorofa kwa hiyo hela lakini zikawa substandard. Nasikia wachina walikataa kujenga kwa hiyo hela. Kuna rumours kuwa zimeshaanza kuharibika. Wasiwasi wangu ni zisije zikaanguka wakati vijana wetu wameanza kukaa ndani. Zingechekiwa ubora kabla ili kuepusha madhara ya baadae ya "loss of human lives".
HIZO TAARIFA UMEZITOA WAPI NDUGU , HATA UDSM PENYEWE SZANI KAMA UNAPAJUA AU ULISHAAHI SOMA HAPA. MBONA ZIKO KATIKA HALI NZURI TU
 
unataka kulinganisha ujenzi binafsi na ujenzi wa serikali?
vifaa vya ujenzi mnanunua bei moja?
michoro na kazi nyingine za ki injinia wao wamelipa kama wewe?
ardhi wao wamenunua kama wewe?
vibali vya ujenzi wao wamevilipia kama wewe?

hayo machache tu ya kutofautisha gharama.
mbona mnakuwa na vichwa vigumu hivo?
Kwanini hamkufafanua kama sio wanafiki nyie ili muonekane eti mnabana matumizi?
.
 
Hakuna mbunge wa chadema mwenye hoja ya msingi sasa hivi wote ni kuropoka tu wake kwa waume. Sijui wamekumbwa na zimu gani, hadi wamemuambukiza na Zito Kabwe na mropokaji siku hizi badala ya kujenga hoja
Wewe ni nani mpaka uwe kipimo cha hoja za msingi. Sema wana hoja usizopenda kuzisikia.
 
Nakumbuka nyumba ya Gavana wa BOT ilijengwa Masaki kwa 1 billions na ushee. Ilikuwa talk of the day kipindi hicho. Mwisho wa siku Kamati ya Bunge chini Zitto akasema wamechunguza na kuona gharama ni sawa. Je itakuwa hiyo mighorofa kwa bei ndogo hivyo. Labda tuambiwe nyumba ya Gavana hela zilipigwa sana
 
CAG Hana muda wa kuchezea .... watu wanataka maendeleo ... !!
 
500 million imetosha, endapo tu haya yafuatayo ndio yaliyofanyika..

1. Ardhi ilikuwa bure, kupima na kibali cha ujenzi kilikuwa bure...

2. Ramani na Michoro ilikuwa bure. Naongelea gharama za kutengeneza michoro architectural and structural drawings...

3. Hakukuwa na kodi kwenye Gharama za vifaa na material ya ujenzi...

4. Vibarua walikuwa wachache, na shughuli nyingi zilifanywa na mashine.... Na pia gharama za usimamizi zilikuwa chini...

5. Endapo TBA walifanya ujenzi huu pasipo kuleta faida...

Kama hayo ndio yaliyofanyika basi bilioni 10 imetosha kabisa, vinginevyo ni uongo mkubwa kusema pesa hiyo inaweza kujenga ghorofa kama zile....
 
K
Hakuna kinachoshindikana.

Kujenga kwa billion kumi ni kitu kinachowezekana kabisa na chenji inaeza kubaki. Ni sawa na kumshangaa mtu anae-survive kwa mshahara wa laki tatu kwa mwezi na ana familia. Wakati wewe una mshahara wa milioni tatu uko bachelor na haukutoshi.

Kama TBA wana ma-engineer wao permanent kabla hata ya mradi, au labda tuseme waongeze wachache kukidhi mahitaji. Posho za vibarua wa Tanzania kila mtu anajua ilivokua aibu hata kuzitaja, japo ndo wanalipwa hivo. Design kuanzia architectural mpaka structural pamoja na usimamizi BICO ya CoET ipo (wasioijua BICO, ni engineering Consulting firm ya UDSM), wana wafanyakazi wanalipwa always wawe wamefanya kazi au lah, na kazi ni ya chuo chao wenyewe ni suala la kutoa maagizo tu hiyo kazi inafanyika.

Ukija kwenye material, Serikali ina share 30% twiga cement, possibility ya kupata Cement kwa bei chee upo. Kokoto na nondo ndio pekee wanaweza kununua kwa bei ya soko. Furniture zote, kuanzia vitanda, makabati yote yametoka workshop za CoET. Kwanini pesa hiyo isitoshe.

Katika mfumo wa kawaida architect atatafutwa atafanya kazi na bado atasimamia. Structural engineer atafutwa na atasimamia kazi, Contractors watatafutwa kuanzia structure yenyewe mpaka services zote (maji, umeme n.k) hapo wote inapaswa wafanye kazi kwa faida na wahakikishe pia wanakuepo site muda wote wanaohitajika. Hapo bado misunderstanding kibao zinazosababisha mradi uchelewe.

Tatizo la nchi hii ni moja tu, haijulikani imeegemea mfumo gani kama ni ubepari au ujamaa. Na kamani vuguvugu basi ijulikane, ili kila mtu kuanzia raisi mpaka housegirl ajue hilo na wote tuishi na kuzoea aina hiyo ya maisha. Ili kusudi kiongozi akija kivingine tumshangae wote kwa Pamoja. Lakini saiv hatujui tuko upande gani, makampuni mengine yanafunga biashara kwasababu wakati wanakuja waliamini sisi tunaelekea kwenye ubepari, sasa raisi Mjamaa kaja hawana chao tena, sharti wafunge virago.

JK aliendesha nchi kipebari na yale yote yaliyotokea katika utawala wake yalitokana na mfumo huo. Kaja JPM nchi inaenda kijamaa na matokeo yake ndo haya mambo yanafanyika kijamaa ile pesa iliyokua inatakiwa iingie kwenye mifuko ya watu inaenda kwenye real things. Hapo lazima watu walie tu.

Katiba yetu inasemaje kuhusu siasa ya nchi yetu? Kuhusu gharama za ujenzi na ubora tungependa ziwe Billioni 500 ili tujue ni majengo yenye ubora na kandarasi wapewe wa Meku?

Kwa wazee wenzangu waambieni vijana gharama za ujenzi wa TAZARA nchi za magharibi zilidai gharama halisi ni Sh. ngapi na muda wa ujenzi walikadiria miaka mingap? Hali halisi baada ya kupewa mchina ikawa Sh.ngapi?

Poleni najua inauma njia zote zinazidi kuzibwa.Naukumbuka msemo wa CUF ya kale,haki sawa ,haki kwa wote.Shikamoo JPM.
 
Back
Top Bottom