Mbunge Susan Lyimo: Kama kweli hostel za UDSM zimejengwa kwa Mil 500, nitatoa hela zijengwe zingine

Yakitokea hayo basi utakuwa ni uzembe wa UDSM wenyewe, kwani si kuna wataalaamm pale. Wameshindwa kukagua nyummba zao wenyewe?
Yakitokea hayo basi utakuwa ni uzembe wa UDSM wenyewe, kwani si kuna wataalaamm pale. Wameshindwa kukagua nyummba zao wenyewe?
Huyo mtaalam wa UDSM asiyependa kibarua chake au uhuru wake hadi kujaribu kupekenyua "siri" za mkuu wa nchi sijamwona bado.
 
Kwa kweli sisi watanzania tuna matatizo na ni vigumu sana kupata maendeleo. Hapa watu wengi watakua na majibu ya ushabiki tu na malimbano yasiokua na maana.
Ilitakiwa kwanza watuwekee uchambuzi wa haya majengo. Watuambie hayo majengo yana ukubwa kiasi gani kwa idadi ya hao wanafunzi. Je ni mawe kiasi au tani ngapi yanatakiwa, kokoto, mchana, cement, nondo, kila kitu na bei. Hapo ndipo tutakapo weza kutoka hoja zenye maana kama kuna iwezekanavyo au hakuna kwa hiyo bei.
Wengi tuliokua humu ndani hatujui ujenzi, na tukijenga hua mtu anajenga taratibu kwa miaka tena hadi mtu u apoteza mahesabu. Na huyu mbunge alitakiwa kwanza aje na mahesabu yake kwanza sio aropoke tu hapo, utadhani alikosa hoja kuchangia.
Mbunge hana shida. Huenda yeye ameshafanya hesabu zake.
Kinachotakiwa, waliotupiwa mpira waucheze ili UDSM wajipatie ghorofa jingine.
 
Mimi nafikiri inawezekana, kuna mada hapa ilishawahi kujadiliwa kuna chuo cha umma kimoja kilijenga jengo lake moja kwa gharama fulani na chuo kingine cha dini kikajenga majengo mawili kwa gharama ile ya jengo moja la chuo cha umma (sijataja majina ya chuo mana huo uzi sijauona).

Ili watu muamini kuwa hili linawezekana subirini majengo ya ukonga magereza, hapa suala ni ujamaa kutumia akili ya ziada, uzalendo na kubana matumizi, tuna wataalamu wengi tunawalipa kwa mwezi, tuna vijana wa jkt na bado tuna wafungwa inaweza kutungwa sheria ndogo ya kuweza kuwatumia hawa wafungwa katika kazi za kijamii.

Arthi ni mali ya serikali kwa hiyo mchanga na kokoto hawanunui ni kuweka mafuta na kubeba, sementi tunanunua kwa wingi ni suala la kuleta mtambo mdogo wa kutengenezea sementi hapo site.
 
Hili jambo nilimuambia rafiki yangu siku mbili tu baada ya mheshimiwa Rais kuzindua Yale majengo.......tulipita pale tukayatazama tukaona yalivyopendeza, nikamuambia jirani yangu.....kwa mil 500 kwanini tusijenge ya vyuo vyote vya serikali?
 
Milion 500 unajenga nyumba ya room kumi hela inaishia kwenye lenta..... Hiyo hela bado ndogo sana
Inawezekana: Kiwanja cha bure kilichopimwa, Nondo kodi free, Saruji kodi free, Mabati kodi free, Wajenzi ni waajiriwa wa Serikali wanalipwa mshahara. Mimi naona iilitosha. Huyu Suzana apewe Kiwanja fasta akajenge hiyo pesa yake serikali isiilazie damu.
 
90% ya wataalam wa UDSM ni zero.

Ni Zero kwa maana gani labda.?
Kipi kimekufanya uwaone ni Zero. Moja kati ya taasisi bora Tanzania ni UDSM. Ukatae au ukubali ukweli ndo huo. Watu wake wakitoka kuja kujichanganya kwenye siasa ndo huwa wanapotea, ila wale ambao wanabakia kwenye taaluma zao bila kujihusisha na siasa huwa bora zaidi. Ila usiseme eti 90% ya wataalamu wa UDSM ni Zero. SIO KWELI
 
Inawezekana: Kiwanja cha bure kilichopimwa, Nondo kodi free, Saruji kodi free, Mabati kodi free, Wajenzi ni waajiriwa wa Serikali wanalipwa mshahara. Mimi naona iilitosha. Huyu Suzana apewe Kiwanja fasta akajenge hiyo pesa yake serikali isiilazie damu.
Kama ni free kwanini hawakusema?Wanatafuta sifa?
 
Simu yako labda ndio ina tatizo.


Simu yako labda ndio ina tatizo.
3b503c646467c732a3190b7d96eb3518.jpg
 
Wadau hata mimi nakubaliana na mheshimiwa mmbuge,kwa ile standard ya yale majengo ya mabibo hostel ni zaidi ya hiyo 500milion,Kwanza tu yale madirisha ya aluminium yaliyowekwa mule ni yakiwango cha juu sana!, sio ya kuchakachua ni mfano tosha.Tusipende kudanganyana jamani!.
 
“Naomba CAG afanye ukaguzi maalum katika hostel mpya UDSM na kama kweli jengo moja linalochukua wanafunzi takribani 390 linagharimu Milioni 500 basi mimi nitatoa Milioni 500 serikali ijenge jengo lingine la ghorofa tatu ili tuweke vijana wengine”. - Susan Lyimo (Mbunge-Chadema)

Toa maoni yako
Unajua kwenye ujenzi kuna gharama za aina mbili: Direct costs + Indirect costs
Direct costs ndio hizo wamenunua mchanga, cement, nondo nk. Ambazo more or less zinafika kwenye hiyo M500.
Ila indirect costs, ukiangalia wale wengi ni wafanyakazi wa TBA na JKT, ambao mishahara yao iko nje ya hizo milioni mia tano.
Vifaa vya ujenzi ni mali ya TBA ambapo gharama zake haziko ndani ya hiyo milioni mia tano.
So ingekuwa ni kampuni binafsi, gharama zingekuwa kubwa kwa kuwa lazima na wakurugenzi na wafanyakazi walipwe mishahara kutokana na contract prices.
 
Back
Top Bottom