Mbunge Sugu achague kuongea kiswahili au kiingereza bungeni anatuchanganya

Mkuu YEHODAYA kama hujui uliza. Hakuna kitu kiitwacho Kiswanglish. Kwa tuliosomea lugha sekondari hiyo yaitwa Code switching na Code mixing. Inaruhusiwa. Shughulisha akili yako mkuu

Kakingereza kalugha ka mkoloni na wewe naona kamekukolea.Mkoloni mwingereza kaondoka lakini ukoloni bado uko kichwani kwako haujakutoka.Unaendelea kukutawala kupitia lugha ya kiingereza.Malkia akisikia mnavyoshobokea hiyo lugha atashangaa na kujiuliza hivi hawa walitaka uhuru wa nini.
 
Huyu mbunge Sugu akichangia hoja huwa anachanganya kiswahili na kiingereza ili aonekane msomi.Wakati hamna kitu.Ukimsikiliza tu anavyoongea unajua ana elimu ya kuunga unga akitafuta aonekane naye yumo yumo.
This is what we call fanatics hivi unapinga kwa kuwa ameongea Kiingereza au kwakua yeye ni mbuge wa CHADEMA?
Ushauri wangu achague ama aongee kiswahili au kiingereza.Lakini hicho cha kuunga unga na kuokoteza okoteza maneno ya kiingereza anatuchanganya na kutukera.
 
Kakingereza kalugha ka mkoloni na wewe naona kamekukolea.Mkoloni mwingereza kaondoka lakini ukoloni bado uko kichwani kwako haujakutoka.Unaendelea kukutawala kupitia lugha ya kiingereza.Malkia akisikia mnavyoshobokea hiyo lugha atashangaa na kujiuliza hivi hawa walitaka uhuru wa nini.
Mimi sijui kiingereza mkuu. Nilikuwa nakupa darasa tu juu ya hoja yako.
 
Hoja yake ni nzito na ya msingi mno kuizingatia kuliko code mixing na code switching language aliyotumia. Think like an educated man with enough exposure just for once and you will do your country a lot of favor.
 
Samahani Mkuu hiki Kiingereza ndiyo chako au cha SUGU?
 
Unasema kuwa SUGU hajui Kiingereza na anababia babia naomba uniambie ni nani labda unadhani anajua Kiingereza kuliko mwenzie hapa Tanzania? Kwa taarifa yako tu kuwa Graduates wengi hawajui Kiingereza kuliko hata huyo SUGU unayemdhihaki na sisi tunaokuwa katika Interviews Panels mbalimbali tunajua hili tatizo. Kwa level ya Elimu ya SUGU hicho Kiingereza chake hakina tatizo na ninachompendea hana AIBU katika kukizungumza ilhali Misomi mingi ikialikwa katika Warsha mbalimbali zinazoendeshwa kwa Kiingereza inasepa au kuomba udhuru. Halafu kibaya sasa huyo unayemsema humu ana Pesa yake ya kutumia kutokana na Hadhi yake ya Ubunge ambayo pengine inataanza kupungua ( siyo kuisha kabisa ) mwaka 3010 huku Wewe sasa katika Akaunti yako Benki umebakiza Tsh 3,200/ tu huku ukisikilizia ni wapi Sukari ya bure itagawiwa Kesho uwahi kupanga foleni.
hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaa yaani umenichekesha sana mkuu na umetoa point kwelikweli mtu anamkalia mtu hajui huyo mtu ana kiasi gani anachoingiza hata akiwa na lughanglish
 
Hii ni pekee Tanzania mtu akiongea ki english anajulikana kama msomi hii kali sana sasa nenda nchi nyingine ambazo ziko chini ya common wealth mfano namibia zambia nigeria south africa botswana au malawi ukiongea kingereza wanakuona kama fala flan af wanaona kama wakuja vile sasa hapa mtu akitia ngeli ishaonekana kesi oooh anajifanya mtu flan mtoa mada una lack exposure kichizi au nenda rwanda burundi ongea kifaransa wanakuchukulia Poa kichizi... Hyo mifano kidogo
 
hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaa yaani umenichekesha sana mkuu na umetoa point kwelikweli mtu anamkalia mtu hajui huyo mtu ana kiasi gani anachoingiza hata akiwa na lughanglish

Usijali Mkuu kuna Watu wengine huwa Wanaboa mno kwa HOJA zao. Hivi Mtanzania kutokujua Kiingereza ni DHAMBI KUU hadi Watu tuanze kupoteza muda humu KUJADILI? Kwanza yeye mwenyewe anakijua hicho Kiingereza? Kama anakijua angeandika kwa Kiswahili chake hicho cha Kindengereko?
 
mbona sie wahaya tunachanganya kiswahili na hiyo English hautushangai??? iweje Sugu Mkuu?? Sugu moto chini.......
 
Mtoto wa Mjini anawakilisha Mbeya Mjini tatizo liko wapi! Pale fasi ya Mwanjelwa MaNiggar wana mfeel kinyama! Keep on Mkubwa wa kazi Sugu Baba Rai,the Don himself! Watchoooo we run da Globalll
 
Huyu mbunge Sugu akichangia hoja huwa anachanganya kiswahili na kiingereza ili aonekane msomi.Wakati hamna kitu.Ukimsikiliza tu anavyoongea unajua ana elimu ya kuunga unga akitafuta aonekane naye yumo yumo.

Ushauri wangu achague ama aongee kiswahili au kiingereza.Lakini hicho cha kuunga unga na kuokoteza okoteza maneno ya kiingereza anatuchanganya na kutukera.

Kwani lazima umsimkilize? Wakuunga unga wenzie tunamuelewa.
 
Kwa kuchanganya lugha ya kiingereza na Kiswahili ungetusaidia kujua ni kanuni ipi ya ya bunge anayovunja ili tuwe na sababu ya msingi kumlaumu.
Kimsingi hajavunja kanuni yoyote ila alitakiwa aanzie kwa Rasi Simba kwanza ili apunguze ugoko
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom