Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Ninamuonya Mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe kuwa ni lazima ajue kuwa CHADEMA,Familia na Biashara ni vitu tofauti. Kwa siku za hivi karibuni umewatumia vibaya vijana wa BAVICHA kuja mitandaoni kukanusha ''kasha''na matendo yako binafsi nakuonya si sawa.
Miaka michache iliyopita ulikitumia chama kukulinda na kashfa ya kuzaa na mbunge wa viti maalum ambayo mwenyewe hukuwahi kukanusha zaidi ya kutuma watu mitandaoni wakilialia.Tulimuonya Makene alipokuja na propaganda za kutetea uhamishwaji wa fedha nyingi nje ya nchi uliohusishwa na utakatishwaji (money laundering), hukujibu badala yake BAVICHA wametumika kulia lia mitandaoni kukutetea.
Unatumia chama vibaya kujibu mambo ya familia na biashara binafsi hata kama muasisi wa chama ni Baba mkwe wako sio sawa. Taarifa kutoka NHC zinaonyesha wewe ni mdaiwa sugu (defaulter) wa zaidi ya bilioni moja, kwa mujibu wa Mkurugenzi mkuu wa NHC Bwana Mchechu badala ya kujibu kiueledi unakimbilia kwenye mitandao unaandika maelezo yasiyo na sahihi yako nani ataamini?...dawa ya deni ni kulipa na sio kutumia vibaya BAVICHA kuja mitandaoni na kukanusha, kama unadhalilishwa au unaonewa kwanini usiitishe vyombo vya habari na ukanushe?
unatakiwa kuyasemea mambo ya familia na biashara kupitia wasemaji tofauti na chama la sivyo unazidi kuthibisha kuwa CHADEMA ni kampuni binafsi na sio chama cha siasa/taasisi ya umma.Yawezekana BAVICHA na vijana uliowatuma kuleta ''porojo'' za utetezi kwenye mitandao wanatumika sababu ya umasikini au kutokujua....imefika mwisho ukome kuwatumia vibaya nao wanahitaji heshima na utu kwani huenda kesho watahitaji kuwa viongozi kumbukumbu ya 'kutukika vibaya' itawapa shida kujiuza.
Wito kwa vijana mliotumika kuleta utetezi wa Mbowe kwa masuala binafsi mkiyahusisha na siasa mmedhalilishwa vya kutosha...jitahidini mtafute ajira nyingine ili angalau kuhifadhi utu wenu.
Nawasilisha