Mbowe: Madaktari msiende Kenya, Rais anacheza na maisha yenu, Kenya sio salama kwa sasa

Kama sera yetu ni kuwatafutia ajira nadkatari baada ya kuwa hatuwezi kuwaajiri ni bora tuwatafutie nafasi nchi nyinginezo zenye utuvu kama botswana nk.
 
Ninamuheshimu na kumkubali sana Mheshimiwa Freeman Alkaeli Mbowe japo Mimi ni Mwana CCM niliyetukuka ila nadhani kuna mahala katika maelezo yake kidogo ametokota na inaonyesha pia hakumsikiliza vizuri Mheshimiwa Rais JPM na hata Waziri husika juu ya hao Madaktari 500 wanaokwenda nchini Kenya.

Ni kwamba Madaktari ambao watapewa Vipaumbele kwenda nchini Kenya ni wale wa Sekta binafsi ambapo ndipo naamini kuna Kundi kubwa la Madaktari ambao bado hawajapata Ajira ila Tangazo hili au Fursa hii haiwahusu Madaktari wote wa Serikalini na walio katika Mikataba maalum.

Ni vizuri siku nyingine Mheshimiwa Mbowe akatuliza kwanza Kichwa chake pale anapotaka kutolea ufafanuzi jambo fulani ambalo kimsingi linahitaji utulivu na uchambuzi wa kutukuka kabisa katika kulikabili.
MBONA UNAONGEA UTUMBO,KWANI HAO WA SEKTA BINAFSI WANATIBU WANYARWANDA HAPA NCHINI AU WATANZANIA?.
Unafikiria kwa kutumia mas..... nini?
 
Rais angekataa ungesikia ohoo Rais ana Roho mbaya anawabania madaktari Rais afanye nini ili mridhike nyie msio na chemvbe ya huruma kwa wa Tz kujifanya mnajua kila kitu
Hoja hujibiwa kwa hoja we nyumbu.

Hivi akili zenu zilisha paralize?
 
Rais Mkapa alikataa kupeleka wanajeshi qetu kule Congo na kauli yake naikumbuka: sitaki kupokea majeneza. Haya ya Rais wetu 'kuwpeleka' madaktari amabao hawana ajira wala mkataba wowote na serikali ni kiini macho cha kuwapeleeka katika matatizo na kisha wakipata shida wanabaki wakiwa. Sijui hata kwa nini tunatumia kauli ya kuwa Tanzania inapeleka madaktari?

Mwambie ndugu yako asiende sisi mbele kwa mbele. Pia hakuna anayelazimishwa ukitaka uende au usiende tena kwa kupeleka maombi. Hatuna wapinzani hapa tz
 
Wananchi au madaktari wamuamini Mbowe ambaye hana Balozi nchini Kenya wakumpa taarifa....wasimuamini Rais JPM

Wapinzani kama ni hawa tulionao ni sheeedah
 
Ninamuheshimu na kumkubali sana Mheshimiwa Freeman Alkaeli Mbowe japo Mimi ni Mwana CCM niliyetukuka ila nadhani kuna mahala katika maelezo yake kidogo ametokota na inaonyesha pia hakumsikiliza vizuri Mheshimiwa Rais JPM na hata Waziri husika juu ya hao Madaktari 500 wanaokwenda nchini Kenya.

Ni kwamba Madaktari ambao watapewa Vipaumbele kwenda nchini Kenya ni wale wa Sekta binafsi ambapo ndipo naamini kuna Kundi kubwa la Madaktari ambao bado hawajapata Ajira ila Tangazo hili au Fursa hii haiwahusu Madaktari wote wa Serikalini na walio katika Mikataba maalum.

Ni vizuri siku nyingine Mheshimiwa Mbowe akatuliza kwanza Kichwa chake pale anapotaka kutolea ufafanuzi jambo fulani ambalo kimsingi linahitaji utulivu na uchambuzi wa kutukuka kabisa katika kulikabili.
Hali ya usalama sio uko Kenya sio nzuri kwa vyovyote vile hawapaswi kwenda coz nchi pia INA ukosefu mkubwa madaktari,waajiriwe serikalini
 
Mdogo wangu ninayeishi naye hapa Dar nmeishamwambia atume maombi ya kwenda Kenya na kama hayuko tayari eti sijui usalama basi aende akaishi kwa Mbowe....
 
SEHEMU YA II - CHADEMA tunasema hivi, Rais Magufuli acha mchezo wa kucheza na maisha ya madaktari wetu, katika mazingira ya kawaida, ingekuwa wanakwenda Kenya wakati kuna hali ya utulivu, kuna hali ya uhakika wa Usalama Kenya tungeruhusu vijana wetu wakafanye kazi kwa sababu hata Wakenya ni ndugu zetu, lakini katika mazingira ambayo kuna mgomo Kenya, kuna kutoelewana kati ya Serikali ya Kenya na madaktari wao, sisi ndio tuwe kimbelembele cha kuwatoa watoto wetu kwenda kutibu Kenya wakati Wakenya wenyewe hawawataki ni kuweka maisha ya Watanzania wenzetu , wataalam wetu katika risk, sisi Kama Chama Kikuu cha Upinzani tunapinga, na naomba Mkutano huu Mkuu wa Kanda ya Pwani utoe tamko la kupinga madaktari wetu kwenda nchini Kenya.

Magufuli na Serikali yake wawape ajira vijana wetu vituo vya afya havina madaktari, Sera yetu ya Taifa inasema vituo vyetu vya afya lazima vihudumiwe na madaktari lakini mpaka leo hakuna madaktari kwenye vituo vya afya kwa sababu Serikali imeshindwa kuajiri.

Kwa hiyo wapo vijana wengi kwa muda wa miaka miwili hawajaajiriwa lakini suluhu sio kuwakimbizia nchi za jirani ambazo zina migogoro na wataalam wao, suluhu ni Serikali yetu itafute fedha iwaajiri vijana hawa, mama zetu, wazee wetu, vijana wetu wanawahaitaji madaktari hawa wawatibu katika vituo vyetu vya afya katika zahanati zetu katika hospitali zetu, Kwa hiyo naomba Mkutano Mkuu Maalum wa Kanda Pwani, naomba mnikubalie Kama Mwenyekiti wa Chama kupitia Mkutano huu tutoe tamko hili rasmi la kupinga madaktari wetu kwenda nchini Kenya.

Nimecopy kwa @FreemanMboweTz
Mbowe chizi, mbona yeye hajawaajiri kwenye SACCOSS yake ya Chagadema?
 
Back
Top Bottom