Mimi nawaza kunyume kabisa na nyinyi.Soma historia vizuri juu nguvu ya "bidhaa sukari" katika kuamua hatma za nchi na watawala. Kimsingi sukari ni siasa ktk nchi maskini ,kama zilivyo bidhaa/huduma nyingine kama chunvi, mafuta ya taa,petroli,unga, maharage,nauli n.k. Kwa nchi zilizoendelea "bidhaa siasa" ni kama mkate, gesi za majumbani,petrol,nishati/umeme,nauli, gharama/bima za matibabu n.k. Zaidi ya hapo tukumbuke kuwa kiwango cha utumiaji wa sukari ktk ngazi zote kuanzia mtu mmoja mmoja(consumption per capita), kaya hadi taifa ni kigezo/kielelezo muhimu cha level ya maendeleo ya kaya, mtu au jamii husika.Kwa mfano, linganisha matumizi ya sukari kwenye kaya maskini na tajiri zilizoko kijiji au mtaa mmoja zenye idadi ya watu sawa.Hivyo hivyo linganisha kwa nchi maskini na tajiri.We unawaza kama mimi