Mbona Tunapiga Sana Kelele Kuhusu Sukari?!.Hii ni Bidhaa Muhimu au ni Starehe Tuu!.

ndivyo tulivyo wabongo,watu wanalalamika bei ya sukari wamesahau ya kwamba elimu ni bure sukari ndo na hela hii inamaanisha ya kwamba sukari ni tamu kuliko elimu..
Acha upotoshaji. Rais anafanya kile anachokijua. Kumbuka, kati ya wanaomhujumu waliwai kumtukana mbwa mwenye mbwa! Halafu mbwa amekuwa mwenye mbwa wanataka kumhujumu ili aendelee kuwa mbwa! Kisa hafungamani nao. Hata mtangulizi wake yuko nyuma ya hujuma na Magu analijua hilo. Tumpe mda, iko siku nchi itawaka moto. Magu anavizia tu, usishangae siku moja Riz kuwa mbele ya pilato na hakuna dhamana! Wanaamini ktk miungu, na tunaamini ktkk Mungu. Haturudi nyuma, Mungu saidia Tz.
 
mkuu upotoshaji hapo uko wapi sasa,ina maana kwani elimu sio bure nchini mwetu? mbona unakulupuka na kutoa povu kwa vitu ambavyo viko wazi ila tu wewe unaviita upotoshaji? au una undugu na Tundu lissu mkuu
 
Kukusaidia kidogo wewe na mwandishi, naomba ujue kwamba sukari na chumvi ni bidhaa muhimu sana katika uchumi wa nchi.

Hizo zinaitwa necessities maana yake ni bidhaa muhimu kwa binadamu.
Yes kiuchumi, mainly viwandani & Pasco kasemea hilo. Doubt yake ni umuhimu wake katika kunywea chai ...

Nikukumbushe pia, madhara ya table sugar/salt kwa mwili.
 
Je, Pasco, kabla ya kuleta mada hii umetumia kinywaji kilichotiwa sukari na ingridents zingine mbili tatu kisha mchanganyiko huko ukaachwa uchache?
 
Wanabodi,

Hili ni swali, Mbona Tunapiga Sana Kelele Kuhusu Sukari?!. Hii ni Bidhaa Muhimu kihivi au ni bidhaa ya starehe Tuu?!. Inawezekana hizi kelele zote ni kujiendekeza tuu?!.

Ninafuatilia jinsi nchi inahaha kuhusu hii bidhaa inayoitwa sukari!, watu wanahaha kuanzia rais wa nchi amekuwa mkali hadi kutishia watu maisha, kisa sukari!, TRA sasa ni kusaka tuu sukari!, Jeshi la Polisi sasa ni sukari tuu!, Takukuru nao sasa ni sukari!, vijana wa Rashid Othman ndio usiseme!, hatuchelewi kusikia hadi vijana wa Mwamunyange nao watajitosa katika hii maana sasa naona imegeuka vita! vita ya sukari, maana inatishia amani, utulivu, usalama wa nchi hadi kuhatarisha ulinzi wa taifa hivyo tutumie jeshi letu na silaha kali kabisa tumwangamize adui huyu!, hivi hii sukari ni nini haswa na ina umuhimu gani kustahilimili hizi kelele zote?!

Swali ni kuwa kwani sukari ndio nini?!, ukiondoa sukari inayotumika kuzalishia bidhaa viwandani, yaani sukari ya viwandani, hii sukari ya majumbani, tunaoitumia kuiweka kwenye chai, sio bidhaa adimu lolote, sio bidhaa adimu chochote, kwa sababu sukari sio bidhaa muhimu kivile, hivyo hizi kelele zote za kila kona sukari, sukari, Watanzani huku ni kujiendekeza tuu!.

Mimi nilikuwa Primari kipindi kile cha "miezi 18 ya kukaza mikanda baada ya vita ya Kagera" bidhaa muhimu ziliuzwa kwa ration ikiwemo sukari, tulipanga foleni hadi kupanga mawe kutushikia nafasi kwenye maduka ya kaya ili tuu kuuziwa kilo mbilimbili mbili kwa wiki kwa kila familia!.

Labda hii kelele yote ni kufuatia tuu utamu wa sukari, lakini sio umuhimu wa sukari kwa sababu kwenye miili yetu, sukari sio muhimu kivile!, virutubisho vilivyo kwenye matunda, yaani sucrose, ni lishe bora mara mia kuliko sukari!. Asali ina virutubisho mara elfu kuliko sukari!, sasa hizi kelele zote za sukari za nini?!. Na kwa msio jua, vyakula vyote vyenye wanga, vikimengevywa na vimengenyo vya pelipeptaid, peptaid na pepton, vinazalisha nguvu mara 100 ya inayozalishwa na sukari!. Ukinywa maziwa fresh ya ngombe, vimengenyo vya renin na pepsin vinazalisha lishe bora mara 100 kuliko hiyo sukari!, why kelele zote hizi za sukari?!.

Baada ya ile miezi 18 ya shida, nilijiunga sekondari ya Tambaza nikila sukari, baada ya hapo nikajiunga Ilboru kule Arusha, huko ndiko nilikojifunza kuwa sukari japo ni bidhaa adimu, lakini sio bidhaa muhimi kivile zaidi ya kujiendekeza tuu!. Shule ya Ilboru chini Mwalimu Mkuu aliyeitwa Bino, aliamua shule hainunui sukari na Ilboru ikawa haitumii sukari!. Kule sukari iliitwa "dawa ya sumu" hivyo ile tuu kujulikana umepangwa Ilboru ili ukasome kwa raha, miongoni mwa bidhaa muhimu za kufungashiwa, ilikuwa ni sukari!, kwa vile mimi nilitokea shule za Dar, wengi niliotoka nao Dar kujiunga Ilboru, walikuwa ni watoto mujini, baadhi yao laini laini na kweli walifungashiwa sukari!, mimi ni miongoni mwa wale wagumu ambao tulitinga Ilboru bila kufungashiwa sukari, ila nilikuwa na fungu, ukitokea umuhimu nitanunua!. Na hapo Ilboru nilipangwa bweni la Oldonyo, wale wa Dar wote niliopangwa nao, walihama kuhamia mabweni mengine yenye heri!, mimi nilikomaa na Oldonyo!.

Asubuhi ilikuwa ni uji wa chumvi!, ulioitwa "sumu" na sukari ndio "dawa ya sumu" saa 4 ni chai ya rangi ya majani ya chai tuu kila mtu anaweka sukari kivyake!, mwanzo nilipoanza kunywa uji wa chumvi nilishindwa, nikajilazimisha, kisha nikazoea!, baada tuu ya kuzoea, ndipo nikatambua kumbe kupenda sukari ni kujiendekeza tuu kupenda utamu!, sukari sii lolote sii chochote!, uji wa chumvi ukawa ni mtamu kuliko uji wa sukari!, nikavikia kiwango hata sukari ikiwepo, sihitaji tena hiyo sukari!.

Baada ya kufaulu zoezi la uji wa chumvi likafuatia zoezi la chai ya rangi bila sukari, hapo napo ilikuwa kazi lakini niliweza, na tena ukiweza kunywa chai ya rangi bila sukari, ndio unapata ladha halisi ya chai au kahawa, ile aroma original yenyewe, na ukiishawezakupata aroma ya chai au kahawa, hutakaa unywe tena chai ya sukari!. Hivyo matumizi ya sukari ni kijuendekeza tuu!, wenzetu Wachina, sukari hawali, chumvi hawali na chinese food hawatumii mafuta!.

Lengo la hawa waficha sukari ni kucreate demand ila wapandishe bei na kutulangua kutokana na uhaba wa sukari. Natoa wito kwa Watanzania wenzangu katika umoja wetu!, tuache kujiendekeza kwa utamu wa sukari!. Tuishii kama maisha ya Ilboru ile, maisha ya bila sukari!, tuisusie hiyo sukari ili hao walioificha iwadodee kwa sababu sukari sio bidhaa muhimu kivile!.

Namalizia na hili swali,
Hili ni swali, Mbona Tunapiga Sana Kelele Kuhusu Sukari?!. Hii ni Bidhaa Muhimu kihivi au ni bidhaa ya starehe Tuu!. Inawezekana hizi kelele zote ni kujiendekeza tuu?!.

Tuache kujiendekeza kwa maisha laini laini, tuishi kiugumu ugumu bila bidhaa ya sukari, na akiwezekana hata tumshauri Magufuli apige marufuku matumizi ya sukari ya majumbani!, au unaonaje?!.

Mgumu Pasco.
Pasco nakuunga mkono kabisa. Badala ya watu kulalamika saana na serikali kuacha kufanya vitu vingine kila uchao ni sukari sukari tu. Sukari kwanza ina madhara mengi tu miilini mwetu kubwa ikiwa kusababisha maradhi ya moyo na pressure na ugonjwa wa kisukari. Kuadimika kwa sukari nafikiri ingekuwa ndio fursa ya wakulima wetu wa asali kunyanyuka. Serikali ingewekeza sasa ktk asali na elimu kwa watumiaji ili asali ishike hatamu. Tuache kabisa kupiga kelele ya sukari as if ndio bidhaa muhimu kivile
 
Wanabodi,

Hili ni swali, Mbona Tunapiga Sana Kelele Kuhusu Sukari?!. Hii ni Bidhaa Muhimu kihivi au ni bidhaa ya starehe Tuu?!. Inawezekana hizi kelele zote ni kujiendekeza tuu?!.

Ninafuatilia jinsi nchi inahaha kuhusu hii bidhaa inayoitwa sukari!, watu wanahaha kuanzia rais wa nchi amekuwa mkali hadi kutishia watu maisha, kisa sukari!, TRA sasa ni kusaka tuu sukari!, Jeshi la Polisi sasa ni sukari tuu!, Takukuru nao sasa ni sukari!, vijana wa Rashid Othman ndio usiseme!, hatuchelewi kusikia hadi vijana wa Mwamunyange nao watajitosa katika hii maana sasa naona imegeuka vita! vita ya sukari, maana inatishia amani, utulivu, usalama wa nchi hadi kuhatarisha ulinzi wa taifa hivyo tutumie jeshi letu na silaha kali kabisa tumwangamize adui huyu!, hivi hii sukari ni nini haswa na ina umuhimu gani kustahilimili hizi kelele zote?!

Swali ni kuwa kwani sukari ndio nini?!, ukiondoa sukari inayotumika kuzalishia bidhaa viwandani, yaani sukari ya viwandani, hii sukari ya majumbani, tunaoitumia kuiweka kwenye chai, sio bidhaa adimu lolote, sio bidhaa adimu chochote, kwa sababu sukari sio bidhaa muhimu kivile, hivyo hizi kelele zote za kila kona sukari, sukari, Watanzani huku ni kujiendekeza tuu!.

Mimi nilikuwa Primari kipindi kile cha "miezi 18 ya kukaza mikanda baada ya vita ya Kagera" bidhaa muhimu ziliuzwa kwa ration ikiwemo sukari, tulipanga foleni hadi kupanga mawe kutushikia nafasi kwenye maduka ya kaya ili tuu kuuziwa kilo mbilimbili mbili kwa wiki kwa kila familia!.

Labda hii kelele yote ni kufuatia tuu utamu wa sukari, lakini sio umuhimu wa sukari kwa sababu kwenye miili yetu, sukari sio muhimu kivile!, virutubisho vilivyo kwenye matunda, yaani sucrose, ni lishe bora mara mia kuliko sukari!. Asali ina virutubisho mara elfu kuliko sukari!, sasa hizi kelele zote za sukari za nini?!. Na kwa msio jua, vyakula vyote vyenye wanga, vikimengevywa na vimengenyo vya pelipeptaid, peptaid na pepton, vinazalisha nguvu mara 100 ya inayozalishwa na sukari!. Ukinywa maziwa fresh ya ngombe, vimengenyo vya renin na pepsin vinazalisha lishe bora mara 100 kuliko hiyo sukari!, why kelele zote hizi za sukari?!.

Baada ya ile miezi 18 ya shida, nilijiunga sekondari ya Tambaza nikila sukari, baada ya hapo nikajiunga Ilboru kule Arusha, huko ndiko nilikojifunza kuwa sukari japo ni bidhaa adimu, lakini sio bidhaa muhimi kivile zaidi ya kujiendekeza tuu!. Shule ya Ilboru chini Mwalimu Mkuu aliyeitwa Bino, aliamua shule hainunui sukari na Ilboru ikawa haitumii sukari!. Kule sukari iliitwa "dawa ya sumu" hivyo ile tuu kujulikana umepangwa Ilboru ili ukasome kwa raha, miongoni mwa bidhaa muhimu za kufungashiwa, ilikuwa ni sukari!, kwa vile mimi nilitokea shule za Dar, wengi niliotoka nao Dar kujiunga Ilboru, walikuwa ni watoto mujini, baadhi yao laini laini na kweli walifungashiwa sukari!, mimi ni miongoni mwa wale wagumu ambao tulitinga Ilboru bila kufungashiwa sukari, ila nilikuwa na fungu, ukitokea umuhimu nitanunua!. Na hapo Ilboru nilipangwa bweni la Oldonyo, wale wa Dar wote niliopangwa nao, walihama kuhamia mabweni mengine yenye heri!, mimi nilikomaa na Oldonyo!.

Asubuhi ilikuwa ni uji wa chumvi!, ulioitwa "sumu" na sukari ndio "dawa ya sumu" saa 4 ni chai ya rangi ya majani ya chai tuu kila mtu anaweka sukari kivyake!, mwanzo nilipoanza kunywa uji wa chumvi nilishindwa, nikajilazimisha, kisha nikazoea!, baada tuu ya kuzoea, ndipo nikatambua kumbe kupenda sukari ni kujiendekeza tuu kupenda utamu!, sukari sii lolote sii chochote!, uji wa chumvi ukawa ni mtamu kuliko uji wa sukari!, nikavikia kiwango hata sukari ikiwepo, sihitaji tena hiyo sukari!.

Baada ya kufaulu zoezi la uji wa chumvi likafuatia zoezi la chai ya rangi bila sukari, hapo napo ilikuwa kazi lakini niliweza, na tena ukiweza kunywa chai ya rangi bila sukari, ndio unapata ladha halisi ya chai au kahawa, ile aroma original yenyewe, na ukiishawezakupata aroma ya chai au kahawa, hutakaa unywe tena chai ya sukari!. Hivyo matumizi ya sukari ni kijuendekeza tuu!, wenzetu Wachina, sukari hawali, chumvi hawali na chinese food hawatumii mafuta!.

Lengo la hawa waficha sukari ni kucreate demand ila wapandishe bei na kutulangua kutokana na uhaba wa sukari. Natoa wito kwa Watanzania wenzangu katika umoja wetu!, tuache kujiendekeza kwa utamu wa sukari!. Tuishii kama maisha ya Ilboru ile, maisha ya bila sukari!, tuisusie hiyo sukari ili hao walioificha iwadodee kwa sababu sukari sio bidhaa muhimu kivile!.

Namalizia na hili swali,
Hili ni swali, Mbona Tunapiga Sana Kelele Kuhusu Sukari?!. Hii ni Bidhaa Muhimu kihivi au ni bidhaa ya starehe Tuu!. Inawezekana hizi kelele zote ni kujiendekeza tuu?!.

Tuache kujiendekeza kwa maisha laini laini, tuishi kiugumu ugumu bila bidhaa ya sukari, na akiwezekana hata tumshauri Magufuli apige marufuku matumizi ya sukari ya majumbani!, au unaonaje?!.

Mgumu Pasco.

Pasco sukari sio bidhaa ya starehe Kama ulivyo pamba kwenye Uzi wako.
MATUMIZI YA SUKARI
1) kutengeneza mikate,mandazi,vitumbua,keki Na vyakula vingi ili kuviwezesha kustahamili uharibikaji.
2) soda,jams pombe za aina zote.
3) madawa ya kuondoa maumivu
Ziko bidhaa nyingi hutumia sukari.
Sasa Kwa nini Ni kilio Kwa WaTanzania?
Mahoteli,MamaLisha Na kina mama wengi wanatumia sukari kwenye biashara zao ambazo ndio zimetusomesha mamilioni ya WaTanzania.
Kwa hiyo sukari sio kiungo cha chai tu.
 
Hatuna haja ya kujua stori yako bana. Watu tunataka sukari. Sukari haitumiki kwenye chai tu, au maziwa -- sukari ina matumizi mengi mfano hata kwenye maharage inatumika. Sukari kwenye pilau inatumika. Sukari inasaidia kuupa mwili nguvu ili
uweze kujiendesha. Tuseme tu, sukari
ikitumiwa kwa wingi ina madhara
makubwa sana kwa afya ya binadamu. Lakini hii siyo hoja watu tunataka sukari hasa ndugu zetu waliopo vijijini wanahitaji sana sukari.
 
Kelele na vurugu zinazotoka upande wa serikali ni jitihada za pande hiyo kujaribu kulinda hadhi ya kiongozi ili kushawishi umma kwamba hakukosea kutoa amri ya kuzuia uingizaji wa sukari. Huko wapo wafuasi wakereketwa wa mkulu au chama, vyombo vya dola, mamlaka za mapato na udhibiti wa bidhaa nk. Upande wa pili ni wakosoaji wa hatua ile. Huko wamo washauri wa uchumi, wanaharakati wa mambo ya kijamii, wapinzani wa kisiasa, wenye maslahi ya biashara na wananchi wasiojifunga na siasa za upande mmoja, ili mradi kila mmoja anakosoa kwa misingi ya shughuli au maisha yake.
 
Back
Top Bottom