Mbegu bora ya samaki ni ipi na je inapatikana wapi?

Amaniwood

Member
Mar 23, 2022
27
56
Habari wadau wa ufugaji. Kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa mbegu bora ya samaki. Zilizopo nizile ambazo hazikui sana kufikia kiasi cha Sato mkubwa, asilimia kubwa zinakuwa kama perege. Je ni wapi au ni namna gani mfugaji anaweza akawa au akapata mbegu bora ya samaki aina ya Sato inayokuwa kwa muda mfupi na ukubwa wakuridhisha?
 
Mbegu bora ya samaki ni ile inayozalishwa na wataalamu wa ufugaji samaki zipo taasisi zilizojikita kuzalisha mbegu ya samaki wa kufugwa kama vile Big fish, Eden agri-aqua, SUA n.k

Kwa uzoefu wangu mbegu nzuri kwa samaki aina ya sato ni Nile Tilapia (Oreochromis niloticus) hii ni specie nzuri samaki anaweza kufika hadi uzito wa 1kg - 2kg kama utamfuga na kumlisha vizuri

Pia kama unataka matokeo mazuri nunua vifaranga ambavyo ni madume pekee (mono-sex) samaki madume wanakuwa haraka kuliko majike, ukifuga madume pekee utazuia population na kutengeneza mazingira mazuri kwa samaki wako kukuwa kwa haraka

Karibu kwa ushauli na msaada zaidi kuhusu chochote kuhusiana na ufugaji samaki
 
Interesting!!
Wanawatenganishaje vifaranga wadogo namna ile kama sisimizi
 
Kimsingi vifaranga uzalishwa hatchery, tunakusanya vifaranga toka midomoni mwa majike tunapeleka hatchery kwenye incubator jar hapo mayai yanakaa kwa siku 1 - 3 vifaranga vinatotolewa,

Hatua inayofata inakuwa ni kuwapa dose ya kufanya wawe madume kwa siku 21 tunawapa hormone kwa ajili ya sex reversal

Baada ya hapo mbegu/vifaranga vinakuwa tayari kwa kupandikizwa bwawani

Kuhusu kuwatenganisha na kuwa hesabu tunafanya manual, mfano unahesabu vifaranga 50 - 100 mara 3 hadi tano unapima uzito wao kujua vifaranga 50 ni sawa na gram ngapi, unapima makundi 3 - 5 tofauti tofauti unapata wastani ukipata wastani inakuwa rahisi kufanya makadilio ya kujua idadi ya vifaranga
 
Njia nyingine ya kuzalisha samaki madume inajulikana kama YY, njia hii wanatumia samaki ambao ni Super male aina hii ya samaki waki mate namajike samaki watakao zaliwa hapa watakuwa madume wote

Nyingine ni kutumia species mbili tofauti ambazo zikikutana razima vifaranga watakaopatikana wawe madume mfano Tilapia nilotica × T. aurea
 
Mbegu bora ya samaki ni ile inayozalishwa na wataalamu wa ufugaji samaki zipo taasisi zilizojikita kuzalisha mbegu ya samaki wa kufugwa kama vile Big fish, Eden agri-aqua, SUA n.k

Kwa uzoefu wangu mbegu nzuri kwa samaki aina ya sato ni Nile Tilapia (Oreochromis niloticus) hii ni specie nzuri samaki anaweza kufika hadi uzito wa 1kg - 2kg kama utamfuga na kumlisha vizuri

Pia kama unataka matokeo mazuri nunua vifaranga ambavyo ni madume pekee (mono-sex) samaki madume wanakuwa haraka kuliko majike, ukifuga madume pekee utazuia population na kutengeneza mazingira mazuri kwa samaki wako kukuwa kwa haraka

Karibu kwa ushauli na msaada zaidi kuhusu chochote kuhusiana na ufugaji samaki
acha fiksi wewe hakuna sato mwenye kilo moja duniani
 
Kimsingi vifaranga uzalishwa hatchery, tunakusanya vifaranga toka midomoni mwa majike tunapeleka hatchery kwenye incubator jar hapo mayai yanakaa kwa siku 1 - 3 vifaranga vinatotolewa,

Hatua inayofata inakuwa ni kuwapa dose ya kufanya wawe madume kwa siku 21 tunawapa hormone kwa ajili ya sex reversal

Amazing!!
 
Sijakuelewa hapa mkuu
Nimejaribu kuelezea kwa ufupi zoezi la utotoleshaji wa vifaranga vya samaki

Samaki sato ni aina ya samaki wanaotunza, kutolesha na kutunza vifanya wao mdomoni (mouth brooders)

Ili kuzalisha vifaranga ambao watakuwa na uniform size inakulazimu kukusanya mayai toka kwenye vinywa vya Samaki wazazi (egg robbery) na kupeleka kwenye incubator kwa ajili ya kuyatotolesha

Mayai yatakaa kwenye incubator jar kwa muda wa siku 1 - 3 hadi pale vifaranga wote watakapo totolewa kabla ya procedures zingine kuendelea
 
acha fiksi wewe hakuna sato mwenye kilo moja duniani

Kaongeza chumvi kidogo.

Ila kwa ufugaji wa samaki, haishauriwi ufuge samaki mpaka afike kilo 1 kwa sababu ya muda, soko, na gharama ya chakula.

Wafugaji wengi wa kisasa wanatoa samaki kwa miezi 6/7 akiwa na gramu 300-500 kilo moja unapata samaki 3-4. Kwa uzito huu ni rahisi hata kuwauzia watanzania wa kawaida wanao taka samaki wa 2000/3000/1500.
 
Namashaka na uelewa wako kuhusu samaki, nimekuwa kwenye industry kwa zaidi ya miaka mitatu nimeshuhudia samaki wengi tu ambao wanazaidi ya kilo 1

Fatilia utaona, tembelea sehemu zenye vizimba (cage culture) au miradi mikubwa ya ufugaji samaki au landing site zilizo around Ziwa Victoria utaona samaki wenye hadi 2kg
 
Kaongeza chumvi kidogo.

Ila kwa ufugaji wa samaki, haishauriwi ufuge samaki mpaka afike kilo 1 kwa sababu ya muda, soko, na gharama ya chakula.

Wafugaji wengi wa kisasa wanatoa samaki kwa miezi 6/7 akiwa na gramu 300-500 kilo moja unapata samaki 3-4. Kwa uzito huu ni rahisi hata kuwauzia watanzania wa kawaida wanao taka samaki wa 2000/3000/1500.
Nilichoandika na ushahidi nacho

Huyu samaki anazaidi ya kilo moja, picha niliipiga mimi mwenyewe
 
Attachments

  • 584995.png
    584995.png
    308.2 KB · Views: 40
Samaki sato ni aina ya samaki wanaotunza, kutolesha na kutunza vifanya wao mdomoni (mouth brooders)

Ili kuzalisha vifaranga ambao watakuwa na uniform size inakulazimu kukusanya mayai toka kwenye vinywa vya Samaki wazazi (egg robbery) na kupeleka kwenye incubator kwa ajili ya kuyatotolesha
Oh thanks sikujua hili, kujifunza hakuna kikomo mkuu
  1. Kwa utaratibu huo samaki mwenyewe anakulaje
  2. Nawe mtaalamu unatumia mbinu gani kuyapata hayo mayai kinywani mwa samaki wakati yuko majini
  3. Unamtambuaje kuwa yupo katika stage hizo
 
na useme ana miaka mingapi sio kusema kilo moja tu, sema ana miezi sita tukucheke
Niweke sahihi, hoja ilikuwa hakuna sato mwenye kilo moja

Twende kwenye hoja ya pili muda ambao samaki anachukua hadi kufikisha kilo 1 au zaidi

Naomba nijikite kwenye samaki wa kufugwa, muda unategemea na factors kama vile chakula, ubora wa maji na management kwa ujumla

Binafs nimeshuhudia samaki akifikisha 1kg kwenye cage culture
 
Oh thanks sikujua hili, kujifunza hakuna kikomo mkuu
  1. Kwa utaratibu huo samaki mwenyewe anakulaje
  2. Nawe mtaalamu unatumia mbinu gani kuyapata hayo mayai kinywani mwa samaki wakati yuko majini
  3. Unamtambuaje kuwa yupo katika stage hizo
1. Sato ni samaki anaekula vyakula aina ya mimea na wanyama/wadudu (phytoplankton and zooplankton) ila kwenye ufugaji tunawalisha chakula chenye mchanganyiko wa virutubisho muhimu (pumba za mahindi, mpunga, mabaki ya dagaa, soya, mashudu ya alizeti n.k) usagwa, uchanganywa na kisha utengenezwa na mwisho samaki wanapewa kikiwa in pellet form ili kiweze kuelea juu ya maji wakati wa kulisha

2 & 3. Samaki wazazi (brooders) uwa wanatengwa nakuwekwa kwenye Happa net kwa ratio ya majike wa 3 kwa dume mmoja na mayai yanakusanywa toka kwenye vinywa vya majike kila baada ya wiki mbili. Majike wenye mayai wanajulikana kwa tabia yao ya kupana midomo pindi unapomshika na taya zao zinakuwa zimejaa na pia wanakuwa very aggressive unapowatoa kwenye maji
 
Barikiwa mtumishi, nimejifunza makubwa toka kwako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom