je parle
JF-Expert Member
- Nov 28, 2018
- 2,022
- 3,908
Hapa Mbagala msikitini kituo cha pili kutoka Mtongani, ni hatari sana kwa maisha ya wananchi wanaoishi maeneo haya. Hiko kituo gari zikitoka Mbagala mission zinakuja speed sana na ukizingatia hapa kuna mporomoko na hakuna matuta.
Wakazi wa hapa kifo sio stories tena kwao, mana kila siku watu wanagongwa wanakufa na hizi gari za Dangote ndio balaa, zinapiga honi moja tu, usiposikia zinakuvaa na kutembea.
Boda boda ndio usisema wao wanagonga na kupita mbio.
Hapa palivyo ni kama hakuna serikali, maana hakuna hatua yoyote inayochukuliwa sababu kulikuwa na matuta yalijengwa baada ya kugongwa mwanafunzi, lakini hii kampuni inayojenga mwendokasi imeyaondoa kwa ajili ya kusawazisha na hawajarudisha tena.
Hapa ni haipiti siku kadhaa bila mtu kufa au kuvunjika miguu.
Serikali tunaomba mtusaidie hapa Mbagala kituo cha Msikitini, wananchi wanaangamia mno. Cha kushangaza hapa gari au pikipiki ikishagonga haisimami na hakuna wa kuipata
Basi hata muweka camera na kibao cha kuamuru madereva kutembea speed fulani ndogo.