hivi wanaotakiwa kujifunza ni wanasiasa au wataalamu ni aibu kwa waziri kusema anakwenda kujifunza ndio maana tunaona maneno mengi kuliko vitendo.Kama wanataka kujifunza wangesoma azimio la arusha na kulielewa kwani hivyo viwanda wanavyozungumzia tulianza kuwa navyo kabla ya vietnam watafute sababu kwanini viwanda vyetu vilizorota na vietnam imepata mafanikio , data zote wanaweza kuzipata BOT badala ya kupoteza kodi za wananchi
Uliwaza kama mimi, bila kuheshimu division of labour tutaingia kwenye confusion nyingine tena.
Hichokinachoenda kijifunza usikite kipo kwenye majarida na kabrasha za wanataaluma zimejaa vumbi kwakuwa tu hakuna communication wala coordination.
Mfano aquaculture wavietnum wanasoma na watanzania kwenye vyuo mbambali duniani, tofauti na sisi wao wanataaluma wao wakirudi wanawatumia kuwatengenezea alternative policies ambazo zinakuwa legitimized na policy makers bungeni.
Sasa waziri aende kujifunza kesho anatolewa wizara hii anaenda nyingine huo utaalamu wenyewe pengine hata muda wakuu extend kwa wengine hana....kweli?
Tujifunze kufanya kazi kila mtu sehemu yake ila tuwe coordinated vinginevyo tutakuwa tunazunguka duara tikajikuta tuna rudi kule kule.