Pascal Ndege
JF-Expert Member
- Nov 24, 2012
- 2,977
- 1,897
Nadhani wataambatana na ujumbe wa wataalam wa wizara husika.
kwanini wasipeleke wataalam tu
Nadhani wataambatana na ujumbe wa wataalam wa wizara husika.
Ni kweli kabisa kuna sarakasi nyingi kwenye hiliNadhani ni utashi wa kisiasa tu. Magufuri Haitaji kujifunza kitu hukoVEVE. Viatel (Hallotel) walivunja mkataba so Magu akataka kuitimua Jamaa ndio amekuja kupooza soo.
Kwani wamekwambia wanaenda kujifunza UTAALAMU WA KILIMO.Nyumbu mna akili ngumu.Wanaenda kujifunza mikakati ya kisera na jinsi ilivyofanikiwa kutekelezwa ndani ya muda mfupi na kuleta TIJA Vietnum.Kama ni wataalamu tunao.Nafikiri tungemwomba Rais wa Vietnam atuletee exparts na consultants waje watushauri tufanye nini ili tupige hatua kama wao, kwenda huko sidhani kama kuna tija, kwanza jiografia ya vietnam na tabia za watu wao ni tofauti na za kwetu, pili huwezi enda wiki moja au mbili vietnam ukaja na weledi labda tupeleke maprofesa wa SUA.
Mkapa alipotaka kuanzisha mradi wa mabasi ya mwendo kasi alimleta mtaalamu mshauri prof mmoja kutoka Brazil laiti tungefuata ushauri wa Mkapa sasa hivi usafiri dar usingekuwa tatizo. Tuwale wa Vietnam watufundishie hapahapa.
nitake radhi mie sio nyumbu, hoja yangu kwanini tusilete mtaalamu mwelekezi ili atizame mazingira yetu alinganishe na ya Vietnam halafu atushauri nini cha kufanya.Kwani wamekwambia wanaenda kujifunza UTAALAMU WA KILIMO.Nyumbu mna akili ngumu.Wanaenda kujifunza mikakati ya kisera na jinsi ilivyofanikiwa kutekelezwa ndani ya muda mfupi na kuleta TIJA Vietnum.Kama ni wataalamu tunao.
Bila shaka kila Waziri husika atachagua timu ndogo ya wataalamu atakaofuatana nao watakaomsaidia kujifunza, kuchambua na hatimaye kuandaa ripoti na mkakati wa utekelezaji hapa nyumbani.hivi wanaotakiwa kujifunza ni wanasiasa au wataalamu ni aibu kwa waziri kusema anakwenda kujifunza ndio maana tunaona maneno mengi kuliko vitendo.Kama wanataka kujifunza wangesoma azimio la arusha na kulielewa kwani hivyo viwanda wanavyozungumzia tulianza kuwa navyo kabla ya vietnam watafute sababu kwanini viwanda vyetu vilizorota na vietnam imepata mafanikio , data zote wanaweza kuzipata BOT badala ya kupoteza kodi za wananchi
Mkuu si ushukuru kwa kuwa hivi sasa unaweza hata kuwahesabu na kuwasubiri wengine kwa hamu na si kama ilivyokuwa mwanzo? Yaani nikiona nafsi yako nadhani unatamani waruhusiwe wengine upate cha kuandika. Duh,kweli Magufuli kawaweza. Hongera Rais wetu.Safari moja huanzisha ingine....1)Majaliwa na Mahiga..2)Mwijage na Mwingulu...3) tusubiri watakuja
huyu muhaya MWIJAGE ni wa ajabu kweli naona hajaacha sifa zake, Huyu bwana tangu tukiwa naye Manchester ni majisifu na majigambo tupu ila uwezo wa kutekeleza ni mdogohivi wanaotakiwa kujifunza ni wanasiasa au wataalamu ni aibu kwa waziri kusema anakwenda kujifunza ndio maana tunaona maneno mengi kuliko vitendo.Kama wanataka kujifunza wangesoma azimio la arusha na kulielewa kwani hivyo viwanda wanavyozungumzia tulianza kuwa navyo kabla ya vietnam watafute sababu kwanini viwanda vyetu vilizorota na vietnam imepata mafanikio , data zote wanaweza kuzipata BOT badala ya kupoteza kodi za wananchi
mkuu umeongea ukweli,hivi wanaotakiwa kujifunza ni wanasiasa au wataalamu ni aibu kwa waziri kusema anakwenda kujifunza ndio maana tunaona maneno mengi kuliko vitendo.Kama wanataka kujifunza wangesoma azimio la arusha na kulielewa kwani hivyo viwanda wanavyozungumzia tulianza kuwa navyo kabla ya vietnam watafute sababu kwanini viwanda vyetu vilizorota na vietnam imepata mafanikio , data zote wanaweza kuzipata BOT badala ya kupoteza kodi za wananchi
tupeleke vijana wakasome masters vietnam, kupeleka nchemba na mwijage kupoteza muda tu, kwani hao wavietnam walijifunza wapi si nasisi tukajifunze hukohuko.Wanaotaka waende wataalam wa Kilimo wanashangaza, mtu tayari keshakuwa mtaalamu halafu aende akafanye nini?, inabidi waende wasiojua
maajabu yanaanza badala ya kuwapeleka wakulima kujifunza wanawapeleka mawaziri, hivi kwa nini wasipelekwe mabwana shamba na mameneja wa viwanda? hivi na hapo inaitaji kuwa na Phd kuwapata wanaotakiwa kwenda kujifunza? ila kwa kuwa utawala huu hautaki kushauriwa au kukosolewa wapo watakaonipinga tena watakuwa wapenzi wa ccmTangu Novemba 5 wakati Dk John Magufuli alipoapishwa, ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Augustine Mahiga pekee waliotoka nje ya nchi, lakini jana Rais aliwaruhusu mawaziri wengine wawili kusafiri nje.
Rais Magufuli alizuia safari za nje siku chache baada ya kuapishwa akisema watumishi wa umma watakaokuwa wakitaka kwenda nje watalazimika kuomba kibali kutoka Ikulu, ikiwa ni mkakati wake wa kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali.
Tangu wakati huo, safari za nje kwa watumishi wa umma zimekuwa za nadra na mawaziri wamekuwa wakifanya ziara za kwenda mikoani kufuatilia utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Jana, Rais Magufuli aliwaruhusu mawaziri wawili kwenda Vietnam kujifunza mbinu za kuinua kilimo na kujenga viwanda ili kuwaondoa Watanzania kwenye lindi la umaskini.
Mawaziri wawili waliopata kibali hicho ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba.
Rais Magufuli alitoa uamuzi huo jana baada ya kufanya mazungumzo na Rais Truong Tang Sang wa Vietnam juzi na kukubaliana kuweka sawa mazingira ya biashara na uwekezaji baina ya nchi zao.
Akizungumza jana baada ya kumtembeza Rais huyo kwenye Eneo Maalumu la Uwekezaji la Benjamini Mkapa (EPZ) lililopo Ubungo jijini hapa, Waziri Mwijage alisema Dk Magufuli ametoa kibali hicho baada ya kuridhishwa na mabadiliko ya muda mfupi ya Vietnam.
“Kutokana na hatua waliyopiga, Rais ameniruhusu mimi na Waziri wa Kilimo, Mwigulu Nchemba kwenda nchini humo muda mfupi baada ya Rais Truong kuondoka.
"Nitakwenda kujifunza mbinu zao ili sekta ya viwanda iajiri zaidi ya asilimia 46 ya vijana wa Kitanzania,” alisema Mwijage.
Baada ya kuondolewa vikwazo na Marekani, Vietnam ilichagua kuendeleza maeneo maalumu ya biashara na kufanikiwa kujijenga kiuchumi na kufikia uchumi wa kati katika kipindi cha miaka 23.
Rais Truong alieleza kuwa waliwekeza Sh10 bilioni katika miradi na asilimia 80 ya fedha hizo ilielekezwa katika mauzo ya nje.
“EPZ zina mchango mkubwa kwenye uchumi wetu. Ninaamini, Tanzania inaweza kupata zaidi ya Dola 20 bilioni kwa mwaka itazipata kutoka katika maeneo haya.
"Hata sisi wakati tunaanza tulikuwa na EPZ chache lakini sasa tunazo nyingi na zinatuingizia dola 20 bilioni (za Marekani) kwa mwaka,”alisema.
Pamoja na eneo hilo, Mwijage alisema Serikali ina mpango wa kuijenga Bagamoyo na kuifanya kuwa mji wa uwekezaji.
“Taratibu za kuwalipa wananchi ili kupisha eneo la kilomita 100 za mraba zimekamilika na ndani ya mwaka huu mchakato huo utahitimishwa kabla wawekezaji hawajaanza kukaribishwa,” alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa EPZ, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia alisema Serikali imeuagiza kila mkoa kutenga eneo la uwekezaji ili kuongeza idadi ya viwanda vilivyopo nchini.
“Kwa sasa EPZ zinaingiza kiasi cha dola bilioni moja za Marekani (zaidi ya Sh2 trilioni) kwa mwaka.Serikali kwa kushirikiana na Singapore imetenga dola 10 bilioni (zaidi ya Sh20 trilioni) ambazo zitatumika kujenga mji wa Bagamoyo,” alisema Kanali Simbakalia.
Mikoa mingine iliyotengwa kwa ajili ya kujenga EPZ ni Kigoma, Morogoro na Mtwara.
![]()
tija tuliyoipata Singapo ndio hiyo ya bomoa bomoa dartupeleke vijana wakasome masters vietnam, kupeleka nchemba na mwijage kupoteza muda tu, kwani hao wavietnam walijifunza wapi si nasisi tukajifunze hukohuko.
prof tiba alipeleka akina mnyika mchechu lembeli kule singapole hongkong Ethipia tumepata tija gani? bado hatujifunzi tu.