Mauaji yanayoendelea Kibiti, Pwani: Maoni, Ushauri na Mapendekezo ya nini kifanyike ili kuyatokomeza

Ushauri wangu kwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas
Njia sahihi ya kukomesha mauaji ambayo yametokea Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji, mkoani Pwani Kibiti ni kuwakamata wauwaji wote na kuwapeleka kwenye Vyombo vya sheria na si kuwaua kwa kudhani!.

You nailed the point. Ukishamuua mtuhumiwa ndo umefikia wapelelezi wa nchi za wenzetu wanaita "dead end". Inatakiwa ujitahidi abaki mzima hata kama ni kwa kumpeleka "first class" kwenye hospitali zetu ila anapopona akupe inteligensia "intel" ya kusaidia kupata "root" na mwisho mtandao mzima wa uhalifu. Hapa kwetu inashangaza sana. Naamini hii haihitaji "rocket science".
 
Acheni watu wafanye kazi,
walipouawa maaskari nane hamkutoa mawazo yenu.
eti Magaidi wakamateni Askari msiwauwe na kuchoma magari yao na Askari wa kike msiwauwe
leo sijui mmetokea wapi kuwa washauri
 
Bado kuna ukakasi mwingi kwenye matukio yanayoendelea kule Kibiti!

% kadhaa naamini kwamba jeshi letu pendwa linatengeneza mauaji ili kutuaminisha kuwa ni kweli wale ndio wahusika...

Haiwezekani unamkamata mtuhumiwa wa mauaji makubwa vile halafu una mkokota eti akupeleke walipo wenzake, walishindwa nini kwenda naye kituoni na wamuhoji ili kuchukua taarifa muhimu?

Haya ni yale yale ya mapango ya Amboni na ugaidi..
 
Ushauri wangu kwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas
Njia sahihi ya kukomesha mauaji ambayo yametokea Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji, mkoani Pwani Kibiti ni kuwakamata wauwaji wote na kuwapeleka kwenye Vyombo vya sheria na si kuwaua kwa kudhani!.
Waambie wajitokeze basi ili wakamatwe...
 
Mm nasubiri kauli ya siro tu kama hao wanao wauwa ndio wahusika wa mauaji kibiti?hatutaki usanii
 
Acheni watu wafanye kazi,
walipouawa maaskari nane hamkutoa mawazo yenu.
eti Magaidi wakamateni Askari msiwauwe na kuchoma magari yao na Askari wa kike msiwauwe
leo sijui mmetokea wapi kuwa washauri
Acheni usanii wa kijinga mtuhumiwa anaweza kutoroka vipi Jeshi la Polisi akiwa chini ya Ulinzi? ??
Baada ya kufika eneo la msitu wa Ngomboroni kikundi cha watu wanaokadiriwa kufikia watano walikurupuka kutoka kwenye kichaka na kuanza kukimbia ndipo polisi kwa tahadhari kubwa walianzisha mashambulizi na kufanikiwa kumjeruhi mhalifu mmoja kwa risasi, katika mashambulizi hayo mtuhumiwa aliyekuwa mkononi mwa polisi naye alijaribu kutoroka na hivyo kupelekea kumjeruhi kwa risasi hivyo idadi yao kufikia wawili,”
 
Umeandika point nakuunga mkono.
Haiwezekani unamkamata mtuhumiwa wa mauaji makubwa vile halafu una mkokota eti akupeleke walipo wenzake, walishindwa nini kwenda naye kituoni na wamuhoji ili kuchukua taarifa muhimu?

Bado kuna ukakasi mwingi kwenye matukio yanayoendelea kule Kibiti!

% kadhaa naamini kwamba jeshi letu pendwa linatengeneza mauaji ili kutuaminisha kuwa ni kweli wale ndio wahusika...

Haiwezekani unamkamata mtuhumiwa wa mauaji makubwa vile halafu una mkokota eti akupeleke walipo wenzake, walishindwa nini kwenda naye kituoni na wamuhoji ili kuchukua taarifa muhimu?

Haya ni yale yale ya mapango ya Amboni na ugaidi..
 
data=238efJooqRaH9sbPvlQlDCVu-egKyviv-DtcsM_6xzKn6eFuy35HOddOB-XUVAP1xxIiKKAWiIV2ADwau59Fl8mjJBc4-03ozheQpZ4J-zYcWWpcbq335gsuBPYHruyhSbTJNDELzpvZ5ByAHWXqknX1bRmD2qtXx7v-ZcSrZk2RTmR9WpVdA4hB56p1icx7KJbZq0f1u2GCKTo7NjdURg

Habari kutokana na matukio ya kuuawa mara kwa mara kwa wananchi wasio na hatia katika Wilaya ya Kibiti, mkoani Pwani, unaushauri gani kwa Serikali/Jeshi la polisi?
 
Mi nikajua unatoa ushauri... kumbe unauliza tena...

Ila Hongera, Post yako ya kwanza JF umeanza na Kibiti...

We inabidi tukutafute uisaidie polisi maana si kwa kasi hii...
 
Washauriwe nini wakati operations zao zimeanza kufanikiwa kwa wauaji kuuawa
 
data=238efJooqRaH9sbPvlQlDCVu-egKyviv-DtcsM_6xzKn6eFuy35HOddOB-XUVAP1xxIiKKAWiIV2ADwau59Fl8mjJBc4-03ozheQpZ4J-zYcWWpcbq335gsuBPYHruyhSbTJNDELzpvZ5ByAHWXqknX1bRmD2qtXx7v-ZcSrZk2RTmR9WpVdA4hB56p1icx7KJbZq0f1u2GCKTo7NjdURg

Habari kutokana na matukio ya kuuawa mara kwa mara kwa wananchi wasio na hatia katika Wilaya ya Kibiti, mkoani Pwani, unaushauri gani kwa Serikali/Jeshi la polisi?
ushauri ulishatolewa na mnyika na lema bungeni nadhani wao wana taarifa nzuri ya kuisaidia polisi.
 
Kutokana na hali inavyoenda huko kibiti, mkuranga na ikwiriri ,nimeona ni vyema ukaanzishwa uzi uwe Sticky kutokana na umuhimu wake. Wahenga walisema dalili ya mvua ni mawingu.. Na tusipoziba ufa tutajenga UKUTA. Suala la kibiti limekuwa geni kwa watanzania kutokana na historia ya kuwa na amani tangu uhuru.. Tuanzishe jukwaa hili ili kwa uhuru kila mtu atoe maoni yake, ushauri kwa serikali, kuwataja watuhumiwa hata wahusika Kama wanafahamika. Nina wasiwasi tusipochukua hatua mapema huenda siku zijazo tukajikuta tunakabiliana na mambo kama haya sehemu kubwa ya nchi tukashindwa kuyadhibiti. Mungu epusha haya ndani ya nchi yetu. Jumapili njema wana jf
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom