Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Kwa jinsi wanavyoelezewa hao usalama wa taifa huku mitaani najiuliza kua labda uwezo wao umepungua kiutendaji ama wafanya kusudi pengine rushwa au wamebadilishiwa majukumu
 
Ndugu zangu. Ninaomba tufumbue macho yetu sote tuone, tutumie akili zetu kutafakari na mioyo yetu iwe na amani kwa maamuzi tunayofikia.

1. Ni idara gani ya serikali iko kwa ajili ya wananchi kwa sasa? Mwenye jibu aseme.

2. Ni idara gani inayoongozwa kwa kutumia wasomi waadilifu na wazalendo waliojaa nchi nzima zaidi ya wateuliwa kwa misingi isiyo na maslahi ya taifa?

3. Si kweli kwamba, ikiwa kuna wasomi walioko kwenye system, hawakuteuliwa kwa ajili ya usomi wao ili wautumie kwa maslahi ya taifa zaidi ya mahusiano ya kibinafsi na watawala?

4.Ni lini kwa mara ya mwisho serikali ya ccm imechukua hatua zinazoonyesha kwamba iko na inajali maisha ya Watanzania katika idara zake zote, kama si pale tu kwa namna moja palihusisha uhai wa ccm na usalama wa familia tawala?

5. Hii inatofauti gani na tawala za Saddam Hussein aliyekuwa akiishi maisha ya juu sana na familia yake, pamoja na jamaa alikouwa karibu naye hapo baghdadi wakati raia wengine wakitembea, wanawaza mauti zao zitakuwa za namna gani. Angalieni walivyokuwa wakiishi kama ngedere, wakizikwa wanaume na vijana wa kiume kwenye makaburi ya pamoja, wengine wakitwangwa kwenye motor za kokoto wakiwa hai katika nchi ya maziwa na asali. Iraq ya Saddam.

6. Ni dhahiri kwamba ccm na serikali yake haipo kwa ajli ya watanzania wa kwenye peripherals. Hii tusahau ndugu zanguni.. Serikali iko kwa ajili ya kulilnda maslahi ya viongozi wa ccm na watawala tu!. Hamjifunzi kwa katiba pendekezwa?

Hamwoni huduma zote za Afya? Miundo Mbinu? Polisi? TISS hao? Elimu? Kilimo? Tamisemi? Katiba? n.k, ni kwa kiasi gani vinafanywa kuwa mbali na maslahi ya wananchi wa kawaida huku vikitoa mwanya kwa watawala kujiimarisha na kujijengea maisha safi wao na vizazi vyao?

Tufungukeni macho. Tutakwisha. Kwa suala la Albino, ni sawa na suala lingine lolote linalohusu usalama wa sisi watanzani wa kawaida. Tusitegemee serikali ya ccm. Hiyo haipo kwa ajili yetu ndugu zangu. Tuliunda majesi ya sungusungu ili kujilinda na ndiyo yamekuwa msaada mkubwa kwa usalama wetu kuliko hao polisi warugaruga wa ccm.

Ninashauri, bila kuchelewa, tuunde kitengo katika Sungusungu zetu. Kitengo cha inteligensia ambacho kitajumuisha kila sungusungu, maalumu kuangalia na kusimia suala la ukataji viungo vya binadamu kwa ushirikina ikiwemo albino.

Tutawadhibiti tu, badala ya serikali. Serikali si ya kwetu. ni ya viongozi wa ccm na watawala.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Binafsi siamini kama usalama wa Taifa wameshindwa, Nahisi kuna namna wanasiasa wanahusika kwa namna moja ama nyingine.

Na mtandao wao ni mkubwa na haigusiki kama wa madawa ya kulevya.
 
Naamini hakuna usalama wa Taifa bali kuna genge la watesaji wapinzani, nilikua nasikililiza kipindi cha Madawa ya Kulevya Radio ya Upendo ni aibu kubwa sana BAK
 
Last edited by a moderator:
Naamini hakuna usalama wa Taifa bali kuna genge la watesaji wapinzani, nilikua nasikililiza kipindi cha Madawa ya Kulevya Radio ya Upendo ni aibu kubwa sana BAK

Mkuu Elli , zamani ilikuwa mtu akisemwa kuwa huyu ni Usalama wa taifa kila mtu anataka ampe favor yeyote ili hata kama ni kumnunulia soda au kumpa lift. Sasa hivi ukijitaja kuwa wewe Usalama wa taifa ujue umetangaza uadui na wanaokuzunguka.
Na kwa ukweli kabisa, hii Taasisi imeharibika sana hii awamu ya nne ya uongozi.
 
Last edited by a moderator:
Mashambulizi dhidi ya albino: Usalama wa Taifa wako wapi?
Lula wa Ndali Mwananzela
Toleo la 396
11 Mar 2015

KAMA vile walikuwa wameenda likizo watu wenye kuhusika katika utekaji na ukataji viungo ndugu zetu albino wameibuka tena; na wameibuka kama wana kisasi. Hadi hivi sasa watoto kadhaa tayari wamekutana na jinamizi hili ambalo ni binadamu wenzetu, na cha kutisha zaidi ni kuwa dalili za watu hawa kutokomea kimoja hazipo. Wapo na wamerudi tena. Hili linahitaji tafakari ya aina yake. Nasema jambo hili linahitaji tafakari ya aina yake kwa sababu hadi sasa mwitikio wetu na hasa wa vyombo vya usalama na viongozi wa kisiasa unasikitisha na kwa kweli unapaswa kubezwa na kila mtu mwenye kutaka kukomesha vitendo hivi.

Mwitikio wa wana usalama wetu ni wa kushtuka na kufuata matukio; si mwitikio ambao unaweza kusifiwa kuwa unaonyesha weledi, mikakati, mbinu au teknolojia. Wameshindwa Jambo la kwanza ambalo ni lazima tuliweke wazi na sidhani kama linahitaji mjadala zaidi ni kuwa vyombo vyetu vya usalama vimeshindwa kukomesha matukio haya na kushindwa huko inawezakana kuna sababu zake nyingi. Inawezekana wameshindwa kwa sababu ya kukosa vitendea kazi, mbinu hafifu, utaalamu au hata weledi wa kuweza kufuatilia mambo haya.

Hili ni muhimu kufikiriwa kwa sababu kila vitendo hivi vinapotokea tumesikia kuwa ni zaidi ya mtu mmoja anahusika na watu wanaofanya vitendo hivi wamekuwa kama mizuka ya aina fulani; wanaingia na kufanya unyama na kutoweka. Kushindwa huku kunatisha. Na naomba kupendekeza kuwa kushindwa huku kunatokana pia na kutokuwa na uongozi wenye weledi na wenye maono ya kuweza kupambana na uhalifu ambao hauko katika vitabu. Ni rahisi kuwafuatilia watu wenye kufanya uhalifu wa ujambazi, wizi, au ubakaji, lakini unaweza vipi kufuatilia watu ambao wanafanya mauaji au kukata viungo katika mazingira ambayo ni vigumu kufuatilia? Lakini kushindwa huku kunafunua jambo ambalo nimekuwa nikiliandika mara nyingi – kulegalega kwa usalama.

Hakuna jambo la hatari kwa taifa lolote lile kama kuwa na vyombo ambavyo ama vimelegalega au havina uwezo wa kukabiliana na changamoto za usalama za zama hizi. Na binafsi naamini kuwa hakuna chombo ambacho kimeshindwa kazi hii, kama Idara ya Usalama wa Taifa.

Usalama umetengenezwa kushindwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa ni Rashid Othman, maarufu kwa baadhi yetu kama R.O. Rashid Othman amekuwa katika kiti cha enzi cha Idara hiyo muda mfupi tu tangu Rais Kikwete aingie madarakani na pamoja wamekaa muda wote huu na kuna uwezekano hatoondoka sasa hadi ngwe hii ya pili ya Rais Kikwete itakapoisha, baadaye mwaka huu. Hata hivyo kama kuna jambo tunaweza kulisema kwa uhakika mkubwa – hasa tukiangalia matukio mbalimbali – ni kuwa hakuna chombo ambacho ni sehemu ya matatizo yetu sana kiusalama kama Idara ya Usalama wa Taifa. Na hapa sizungumzii kirahisi rahisi.

Matatizo haya ya msingi ya Idara hii yanatokana zaidi na kisheria na kimfumo kwani kati ya sheria mbovu zilizowahi kutungwa na Bunge letu ni ile iliyounda Idara hii. Wakati mwingine tunaweza kusema kuwa ilikuwa ni vizuri wakati Idara inaongozwa kutokana na sheria mbalimbali za Usalama wa Taifa kuliko ilipoundwa sheria kuifanya idara hii rasmi mwaka 1996. Sheria ile imetengeneza chombo ambacho kwa jina kinatisha lakini kivitendo kinaonekana kuwa legelege. Ni kama sanamu ya simba iliyowekwa kwenye nyasi na kutishia kila anayepita karibu; hadi pale wanapogundua kuwa si simba wanaweza kufanya lolote.

Matukio haya ya mauaji na ukataji viungo albino ni ishara kuwa kuna watu wanaamini kabisa kuwa vyombo vya usalama havina uwezo wa kuwafuatilia. Na hili ni kweli hasa unaposikia kuwa watu wanaolipwa na Watanzania wanakuja na masuluhisho ambayo ni ya kihisia kuliko kihalisia. Kwa mfano, mwitikio wa serikali yetu ni kuwalaumu waganga wa kienyeji. Wanataka watu waamini kuwa vitendo hivi dhidi ya albino vinasababishwa na waganga wa kienyeji; wanashindwa kujiuliza maswali mawili rahisi tu: Mbona waganga wa kienyeji wamekuwapo tangu enzi na enzi na havikuwapo vitendo kama hivi? Kweli wanaamini kabisa kuwa waganga wa kienyeji wakifutiwa usajili Tanzania ndio utakuwa mwisho?

Kwani nchi nyingine jirani na Watanzania wengi wanaenda kwa shughuli mbalimbali hakuna waganga wa kienyeji? Lakini hata kama tukikubaliana kuwa wapo waganga wa kienyeji wenye kufanya biashara hii tunajiuliza hivi kweli kabisa Polisi na Usalama wa Taifa miaka yote hii wameshindwa kabisa kwenda kwa kujificha (under cover) kuweza kuzama kwenye mtandao huu? Miaka yote hii kweli kabisa tumeshindwa kupeleka watu wakaweza kuufuatilia mtandao huu na kuukata kuanzia kwenye mzizi badala ya kuhangaika na majani yake? Hatari ya kushindwa ni kubwa zaidi Kinachonitisha mimi na kwa namna fulani kimshtue kila Mtanzania ni hatari ya kushindwa huku.

Ukiondoa ukweli kuwa kushindwa huku kumesababisha kuibuka tena kwa vitendo hivi naamini kunaweza kuwa na matokeo mengine yasiyotarajiwa; tunaweza kujikuta tunanyonga watu wasiohusika. Mojawapo ya mambo ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara vinapotokea vitendo hivi ni mara moja kuwashuku baba wa watoto hao; na kama baba hajui kujieleza vizuri au anababaika basi mara moja ni rahisi kuonekana kuwa na hatia. Matokeo yake vyombo vya usalama vinaweza kujikuta ili kutuliza hasira za wananchi vinawashikilia wazazi (hasa baba) kwa kuwahisi kuhusika na vitendo hivi.

Kama ikatokea kweli baba hakuhusika lakini ameshindwa kujieleza vizuri au kupata utetezi mzuri wa kisheria basi tunaweza kujikuta tunawapeleka watu kunyongwa wasiohusika na hivyo kufanya janga hili kupiga mara mbili! Ni kwa sababu hiyo naamini suala hili linahitaji kukabiliwa kisayansi na kwa mbinu za kisayansi zaidi. Lakini pia linahitaji kuangaliwa kwa kuhakikisha kuwa badala ya kuwa tunaitikia matukio ni muhimu tuangalie nje ya kawaida tuliyozoea.

Je, hakuna njia bora zaidi ya kuhakikisha tunajua watoto albino katika mazingira yenye matukio haya walipo; je, hatuwezi, kwa mfano, kuhakikisha kuwa kila familia yenye albino hasa kwenye maeneo yenye matukio haya inapatiwa simu maalumu ambayo wanaweza kupiga namba sekunde moja tu (speed dial) pale watu wasiofahamika wanapobisha hodi majumbani mwao? Je, inawezekana kuhakikisha kuwa Helikopta ya Polisi au za jeshi zinakuwa tayari kuruka sehemu yoyote kwenye mikoa ya Geita, Shinyanga, Rukwa na Mwanza endapo simu inapigwa kuwa kuna mtoto kashambuliwa? Je, maofisa wa Usalama wanaweza vipi kujipanga kwenye hili?

Ni wazi kuwa hadi hivi sasa chini ya R.O wameshindwa na inaonekana Rais Kikwete bado – kama ilivyo kwenye Jeshi la Polisi – haamini kuwa kuna tatizo katika uongozi wa idara hizi. Labda mpaka tutakaposikia watoto wa vigogo wanaanza kukatwa viungo kwa imani za kishirikina; nina uhakika sidhani kama watafikia watoto hata kumi kabla dunia nzima ya Watanzania haijapinduliwa. - See more at: Raia Mwema - Mashambulizi dhidi ya albino: Usalama wa Taifa wako wapi?

CC: Tized, Mr Rocky, Fixed Point, lyinga, NATA, Chakaza, Elly B, Ablessed, Michelle, KikulachoChako, kill 3, Daudi Mchambuzi, everlenk, MziziMkavu, Ablessed, afrodenzi, Heaven on Earth, Power to the People, Jasusi, Eiyer, idawa, nguruvi, Mentor, Sikonge, Dingswayo, MANI, tpaul, Bramo, Bulesi Bulldog, Sangarara, MTAZAMO, Erythrocyte, Mag3, Mimibaba, zumbemkuu, Crashwise, amkawewe, Idimi, Ogah, Chakaza, mshana jr, JokaKuu, MWALLA, genekai, PRINCE CROWN, Tuko, Shark, lynxeffect22, samaki2011, MoudyBoka, adolay, Elli, nyabhingi, Janjaweed, S.N.Jilala, MEANDU, Tabby, Candid Scope, Honolulu, August, dyuteromaikota, BONGOLALA, Gefu, Bigirita, Kozo Okamoto, Shark, mirisho pm, Camp 05, Ngoami, Kamakabuzi, jerrytz

Ukitaka kuwajua usalama wa taifa we anzisha mgomo au andamana. Huna hata nusu saa utajikuta unateswa
 
Waswahili wanasema mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe, hili jambo sababu hakuna ndugu zao na watoto wao ndo maana haliwagusi, iliyobaki wananchi tuungane tuingie mzigoni wenyewe hakika kwa pamoja tunaweza, ingelikuwa kuna watoto wao hadi FBI wangeletwa kusaidia hilo jambo.
BAK kwanini mambo haya in kipindi cha uchaguzi tu? Kuna nini hapa?????
 
Last edited by a moderator:
Kila kiongozi anakemea , wananchi tunasikitika, wanaotakiwa kutulinda nao wanakemea, wateja wa hivyo viungo ukute nao wanakemea tena kwa nguvu na wakati huo huo mauaji yanaendelea bila kukoma. Sasa tujiulize ni nani mwenye jukumu la kulinda wananchiiii
 
Wewe ndio uachane na uvivu wa kufikiri, kazi ya vyombo vya dola ikiwemo huo usalama wa Taifa, unadhani hawa wanauawa ama kunyofolewa viungo vya mbali mbali wangekuwa watoto wa viongozi unadhani hili tatizo lingedumu muda mrefu kiasi hiki!? Uwe una tafakari kwa kina badala ya kukurupuka na kuandika pumba.

Tatizo ni la jamii nzima na kuna vyombo husika ambavyo vinatakiwa kusimamia hili tatizo kuhakikisha linatokomezwa kabisa, kuendelea kuwepo kwa tatizo hili ni ushahidi tosha kwamba vyombo hivyo vimeshindwa kwenye utendaji wake wa kupambana na tatizo hili.


Hili tatizo ni la jamii nzima sio mtu mmoja au taasisi moja.acheni uvivu wa kufikiri
 
Back
Top Bottom