Matumizi ya Serikali Kwenye Magari ya Taasisi za Umma ni ufujaji, Wafanye Hivi

Makamura

JF-Expert Member
May 19, 2022
358
551
Bajeti ya magari ya serikali kila mwaka Bilioni 600, Hii pesa haimaanishi kuwa inanunua magari pekee na pesa ikaisha.

Hivyo kwanini Serikali iwe na utaratibu mzuri Kila Taasisi Ijinunulie Magari yake kutoka kwenye Mishahara Ya wafanya Kazi, tuone kama watanunua V8 na VX kama wanavyofanya sasa. Yani mfano TRA magari si wanatumia wafanyakazi basi Asilimia kadhaa kutoka kwenye Mishahara yao inunue hayo makari kama mkopo, Hii italeta Heshima katika utunzaji na Ununuzi wa magari kiholela. Unakuta Mkurugenzi anatumia PRADO V8 ya mwaka 2023, ila akipewa nafasi ya kununua gari kwa mshahara wake hawezi nunu hili atanunua Vits au Passo ili kubana matumizi.

Hii itasaidia Hizi taasisi kuwa na Nidhamu katika matumizi ya pesa za serikali
 
Back
Top Bottom