Matumizi ya Kiswahili: EAC igeni mfano wa AU, Magufuli kaonesha Njia

We chakaza mbn unatumia muda mwingi kuponda tu matumizi ya kiswahili
Tuwe wakweli tuu na kuacha propaganda, hivi style ile ya mkulu kusoma hotuba ndiyo inayotakiwa kweli kwa kiongozi wa nchi? Hotuba haina mvuto wa kusikiliza hata kwa wanaojua kiswahili sembuse wasiojua? Kiswahili kitamu bwana, lakini sio vile unasoma kama unakimbizwa na mbwa wa polisi!
Lakini ukweli ni kuwa msomaji wa hutuba ile hakuisoma kwa kiswahili kwa nia ya kupromote bali hakuwa na mbadala. Kama kupromote kwenyewe ndio kule hakika hata watu hawataitaka hiyo lugha kwani haina mvuto kama walivyoisikia kutoka kwa msomaji.
 
Inabidi kwanza tukubaliane ni kiswahili cha aina gani tunachoweza kuiga. Tuwe wakweli kile sio kiswahili tunachoweza kujivunia nacho. Labda tuongeze juhudi ya kujifunza kwanza kiswahili.
 
Wanajitahidi, lakini sio lugha yao ya kwanza. Dunia hii ni kiingereza/kifaransa/kijerumani/Spanish kama lugha za kwanza. Hizi nyingine zinafuata baadae. Ni utani usiomithilika viongozi wote kupeleka watoto wao shule zinazofundisha kwa kiingereza kisha kujifanya wanakienzi kiswahili. Ukienda maofisini ili uweze kupata kazi nzuri ama inayohitaji ujuzi barua na cv yako unapeleka kwa kiingereza, halafu leo mtu anatuletea maigizo ya kiswahili. Huu udhaifu uko wazi na wala hauna mahusiano yoyote na uzalendo.

Umemaliza kila kitu mkuu
 
Mkuu kupongezwa mtu hakuji kwa kulazimisha Bali ni matokeo ya kile ulichofanya. Ile hotuba haikuwa ya kutoa maagizo bali kujaribu kuweka sawa historia ya Mwl na mchango wake. Ni hotuba iliyo paswa kuwa na Rambo za mvuto uliojaa bashasha hasa ukizingatia wapo wengi mle wamenufaika na juhudi za Mwl.
Kuisoma kama Fundi cherehani ashonavyo Nguo siku mbili kabla ya Iddi au Christmas huku ukiruka nukta na koma ni kunvunjia hadhi babavwa taifa na sisi wote tunao muheshimu.
Ile hotuba angeisoma Kagame au Museveni na katika kiswahili hichohicho Dunia nzima ingezizima kwa kilicho semwa. Sisi pamoja na kuwa ni wa nyumbani tumepoteza hata nini kasema
 
Nampongeza Rais Magufuli kwa kuongea kiswahili katika mkutano wa umoja wa mataifa huru ya Africa, AU.
Kutokujua vema lugha ya kiingereza kumempatia vema Mh. Rais fursa ya kutangaza lugha yetu zaidi. Au pengine hata angali akijua kiingereza angaliweza pia kuamua kutumia kiswahili kwa sababu ya uzalendo wake. Ikumbukwe pia kuwa Kiswahili ni lugha rasmi ya mawasiliano katika shughuri za umoja huo, pamoja na Kifaransa, Kiarabu na Kiingereza. Lugha zote hizo zinapozungumzwa lazima kuwapo na mtafasiri, isipokuwa kiingereza, ambacho hutumika zaidi kwa kutunzia nyaraka za umoja huo. Kiswahili hakitumiki kutunzia nyaraka/kumbukumbu katika AU.
Lakini ni vema pia kukumbushana mapema kuwa katika mikutano ya umoja wa mataifa ya dunia (UN), kiswahili hakitambuliki. Kwa hiyo, Mh. Rais atalazimika kujiendeleza zaidi katika kiingereza ili aweze kumudu mawasiliano ndani ya UN, endapo atalaziika. Au anaweza kujifunza Kiarabu, Kifaransa au Kichina ambazo hutumika huko UN.
Namaliza kwa kumshukuru zaidi Mzalendo Mh. Rais kwa kutangaza lugha yetu adhimu ya kiswahili.
Nawasilisha.
 
Hapo sawa, pia kumyima Mkalimani asiongee.
Picha inaonyesha watumiaji wote wa lugha za kiingereza na kiswahili huko AU wakiwa wamevaa vitafsiria wakiwapo kina Museveni na hata balozi Mahiga lakini yeye akiwa hajavaa sawa na waarabu wa Tunisia jambo linaloashiria kuwa anajua kiarabu ama hakujua kinachoendelea humo ndani ya ukumbi
 
Picha inaonyesha watumiaji wote wa lugha za kiingereza na kiswahili huko AU wakiwa wamevaa vitafsiria wakiwapo kina Museveni na hata balozi Mahiga lakini yeye akiwa hajavaa sawa na waarabu wa Tunisia jambo linaloashiria kuwa anajua kiarabu ama hakujua kinachoendelea humo ndani ya ukumbi
Kagame alikuwa anacheka sijaelewa kwa sababu gani
 
Back
Top Bottom