Matukio makubwa ya uhalifu yaliyowahi kutokea na kusisimua Nchini Tanzania

TUKIO LA UVAMIZI NA MAUAJI KITUO CHA POLISI UKONGA STAKISHARI
MAJIRA YA SAA NNE NA DK 20

Majambazi yalifika eneo la tukio wakiwa na gari bodaboda mbili boxer na fekon

NDANI YA KITUO
Mama mmoja na mume wake walimleta mhalifu wa tukio la wizi kabla hawajamaliza ngazi majambazi yakawafyatulia risasi na kufa hapo hapo.

Polisi walitaharuki kwa kuwa hawakutegemea yakaanza mapambano ya risasi yakaua polisi hao na kwenda store

Walipofika store sasa hapa ndio kuna maswali mazito funguo waliipata wapi. Walikua na viroba wakaaza kupakia silaha hizo

Kuna kitu cha kujifunza hapa kama wana gari kwa nini waweke kwenye viroba jibu ni kuwa kuna safari mbili mbele ya safari gari litawaacha na wao watapata usafiri mwingine.

WAKATI WA KUONDOKA
Kuna askari aliejeruhiwa alijificha chini ya gari alimpiga risasi ya mguu dereva mmoja wa pikipiki ikabidi washuke na kuanza kuchechemea dereva huyu alikodiwa majambazi wakampiga risasi inaonekana alitakiwa kuwabeba na mwisho auwawe.


Majambazi yakakimbilia Kitunda na gari lao
 
Umesahau matukio ya wabunge waongeaji sana kufa kwa ajari ili hali dreva anatoka mzima kabsaaa.

Umesahau tukio la kutekwa kwa doctor (nimemsahau jina naisi ndio alikuwa mwenye kiti wa umoja wa madaktari) wakati wa mgomo wa madaktari
Dk. Ulimboka
 
Hiyo namba 1 Nakumbuka utotoni nlikuwa mtundu sana, Maisha yangu nlikuwa Naishi kwa kupigwa patration tu nkatupwagwa chimala, huko walikuwepo
Wachuna ngozi walikuwa maarufu kama nyambuda
Walitisha sana huko maana kila kukicha kesi zao tu

Ova
 
1.Upotevu wa 1.5trilion
2.Upotevu wa 1.5 trilion
3.Upotevu wa 1.5 trilion
4.Kutumbuliwa kwa CAG
5.Ujenzi wa Uwanja wa Chato.

Halafu ndo yanafuata haya

Popo Bawa
Tukio la Ditopile kumpiga Risasi dereva wa daladala
Polisi walipompiga risasi Akwelina
Mkurugenzi aliyemliga risasi raia kanisani
Kupigwa risasi kwa Mh Rais mtarajiwa Tundu Lissu
Kuvuliwa ubunge Lissu
Wabunge wa upinzani kuunga juhudi.
Spika kumtambua Mwambe kama mbunge japo alijiuzuru
Udukuzi wa sauti za akina membe,nape na kinana
Babu wa Loliondo
Kifo cha Ruge
Kifo Cha Nyerere
Kifo Cha Kanumba
Ajali ya treni ya Dodoma
Ajali basi la Airmsae
Ajali basi la shabibi lilioua watu wote kule Songea
Ajali Mv Bukoba
Ajali Mv Spice islander
Lowassa kwenda Chadema
Lissu kupigwa Risasi


Ongezea na hii
Mapokezi ya ndege kuanzia Jiwe,naibu Rais,mawaziri,wakuu wa mikoa na wilaya,makatibu wakuu,wananchi wanyonge nk walijazana pale Airport kuipokea Ndege hivyo walisimamisha nchi
 
Back
Top Bottom