Matukio makubwa ya uhalifu yaliyowahi kutokea na kusisimua Nchini Tanzania

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
76,019
159,773
Huu ni uzi maalum wa kukushana uhalifu mbalimbali uliotokea Tanzania 🇹🇿 kwa nyakati mbalimbali.

Matukio haya hayako kwenye mtiririko maalum wa kikalenda.

1. Matukio ya uchunaji ngozi watu mkoani Mbeya wilayani Mbozi.
Matukio haya ya aina yake yalitokea mkoani Mbeya ambako ngozi za watu zilikuwa zikichunwa na kuuzwa kwa Bei ya shilingi milioni ishirini.

Ilikuwa inatakiwa ngozi ya mtu mzima, mwanaume au mwanamke, isiwe na kovu Kubwa au jeraha Kubwa. Wanunuzi wa ngozi hizo walikuwa Ni raia wa Malawi, Zambia na Zaire kabla haijajtwa Congo DR.

2. Wizi wa Justine Kasusura
Justine alikuwa ni mfanyakazi wa kampuni ya ulinzi na aliajiriwa Kama dereva. Alitumwa aende airport akachukue mzigo na kuupeleka Stanbic Bank.

Jamaa akashtukia kuwa ule mzigo Ni pesa ndefu 2 million dollars. Jamaa akatoroka nao. Baada ya miaka miwili akakamatwa na akahukumiwa kifungo Cha miaka 30 jela, alikata rufaa na kushinda kesi.

3. Mauaji ya Dr. Kleruu Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Dr. Kleruu alipigwa risasi siku ya Krismas alipoenda kukagua mashamba ya ujamaa. Akamkuta mkulima Mwamwindi Yuko shambani kwake akifanya kazi, akamuuliza kwànini hauko kwenye shamba la Kijiji?

Mwamwindi akajibu kwenye shamba la Kijiji hamna mtu wote wameenda kula sikukuu. Kukatokea majibishano. Mwamwindi akakasirika, akaingia ndani, ukatoka na bunduki, akampiga risasi Mkuu wa Mkoa, Kisha akaipaandisha maiti kwenye trekta na kwenda kuibwaga polisi.

Mwamwindi alihukumiwa kunyongwa Hadi kufa na Mwalimu Nyerere. Ndiye mtu pekee aliyenyongwa enzi za utawala wa Mwalimu.

4. Salim Njwete a.k.a Scorpion kutoboa mtu macho
Tukio hili la kusisimua lilimhusisha mtaalam wa karate SALIM NJWETE SCORPION na kinyozi. Scorpion alikuwa amekodiwa na watu waliokuwa wakimtumu kinyozi kuchukua mwanamke wao.

Scorpion alihukumiwa kifongo Cha miaka saba jela na kulipa milion 30
Scorpion ni mhalifu hatari ambaye amekuwa akifanya mambo mengi ya kinyama kwa watu na mali zao eneo la Buguruni na maeneo mengi ya jijini Dar na Tanzania kwa ujumla.

Wiki iliyopita alifanya tukio la kinyama la kumtoa macho mpita njia maeneo ya Buguruni na wananchi wakawa wanaogopa hata kusaidia, ila inaonesha ana genge kubwa analoshirikiana kufanya huu unyama na ndio mana anapata jeuri ya kufanya unyama wa kutisha mbele za watu bila kuogopa.

Hivyo tunamuomba Waziri wa mambo ya Ndani Mh Mwigulu Lameck Nchemba, IGP Ernest Mangu na Idara yote ya usalama wa taifa wafuatilie vizuri mizizi ya huyu mtu na kuing'oa hiyo mizizi, ili kuweza kuwalinda watanzania na watu hatari kama hawa.

Kingine ni kuiomba serikali itoe adhabu kali kwa huyu muuaji scorpion ili pia iwe fundisho kwa wenzake waliopo mtaani.

Hizi ni baadhi za picha za muuaji scorpion na aina ya maisha yake


View attachment 413366

Mshindi wa shindano laDUME Challenge 2012, Salum Njwete "Samjet" (kushoto) akipokea hundi ya shilingi milioni 20 na cheti cha ushindi toka Meneja uhusiano na mawasiliano wa T-MARC Tanzania, Maurice Chirimi (kulia) katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za T-MARC jijini Dar es Salaam Jumatatu. Hongera Samjet.

View attachment 413152View attachment 413153View attachment 413154View attachment 413155View attachment 413156View attachment 413157View attachment 413158View attachment 413159

Habari zaidi soma=> Mahakama ya Ilala imemhukumu Salum Njwete 'Scorpion' Kifungo cha miaka saba na faini ya sh milioni 30


5. Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na Watu wasiojulikana.
Tukio hili la kipekee lilitokea mchana kweupeeee jijini Dodoma kwenye makazi ya viongozi ambapo Tundu Lissu akiwa kwenye lunch break alishambuliwa. Hadi leo hamna aliyekamatwa Wala kuhojiwa kwa tukio Hilo.
Breaking News: TUNDU LISSU APIGWA RISASI DODOMA....ANGALIA PICHA HAPA
by Malunde TV 6 months ago

WhatsApp%2BImage%2B2017-09-07%2Bat%2B16.09.47.jpeg


Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kupigwa Risasi hii leo mkoani Dodoma (Picha na Mwananchi Digital)


Mbowe akiwa na Dereva wa Tundu Lissu aliyeshika nguo zenye damu
 
Tukio la Mauaji ya Mwandishi wa habari wa channel Ten, ndg: Mwangosi.

Hili Tukio lilitokea Mkoani Iringa Ambapo Ndugu Mwangosi aliuawa kwa Bomu na Askari police wa Tz akiwa anatimiza majukumu yake katika mkutano wa chadema.

Askari police alihukumiwa miaka 15 jela .
 
Mauaji ya wafanyabiashara wa madini wasio na Hatia

Wana JF, kesi hii ni ya kipee sana, inatuonesha namna ufisadi ulivyokuwa unaendelea kulivamia Taifa kila kona yaani BOT, TANESCO, ATCL, hadi POLISI nk. Kesi hii imeanza tena baada ya kuahirishwa kwa muda wa miezi kadhaa. Haya ndo yaliyoendelea jana.


Katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, mahakama hiyo ilielezwa na upande wa mashtaka kuwa mshitakiwa wa 11 Koplo Rashidi alishinikizwa na wakuu wake wa kazi, Zombe na Bageni, kutoa maelezo ya uongo kwenye tume ya Polisi na ya Jaji Kipenka.

Shahidi huyo, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Edson Mmari (55) kwa sasa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora na wakati wa tukio hilo alikuwa Mpelelezi wa Makosa ya Kuwania mali, Makao Makuu ya Upelelezi.

ACP Mmari aliieleza mahakama kuwa alikuwa ni mmoja wa maofisa walioteuliwa kuchunguza kesi ya mauaji inayomkabili Zombe na polisi wenzake.

"Baada ya kuteuliwa tuliambiwa washitakiwa wamekamatwa na wako Kituo cha Polisi Kati (Central) hivyo tuliwahoji,"alisema ACP Mmari.

Mmary alikuwa akihojiwa na wakili wa Serikali Alexander Mzikila na shahidi huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa Machi 6, mwaka 2006 majira ya asubuhi aliitwa makao makuu ya upelelezi.

Alidai baada ya kufika ofisini na mshitakiwa wa 11 Koplo Rashidi kutoka kituo cha Polisi cha Kati (Central) alifikishwa ofisi hiyo ya upelelezi. Baada ya maelezo hayo majadiliano yalikuwa kama ifuatavyo:-

Wakili Mzikila: Baada ya mshitakiwa huyo kuletwa makao makuu ya upelelezi mlifanya nini?

Shahidi: SSP Mkumbi alimuuliza jinsi anavyofahamu tukio hilo na mshitakiwa alisema maelezo yote aliyoeleza tume ya polisi na ile ya Jaji Kipenka yalikuwa ni ya uongo na kwamba angetueleza ukweli wa tukio lilivyotokea.

Wakili: Alieleza ni sababu zipi zilizomfanya atoe maelezo ya uongo?

Shahidi: Alidai maelezo ya uongo aliyoyatoa, alishinikizwa na viongozi wake wa kazi yaani Zombe na Christopher Bageni (mshitakiwa namba mbili) na alionyesha kikaratasi kilichoandikwa maelezo aliyotakiwa kujibu kwenye tume hizo.

Wakili: Baada ya hapo mlifanya nini?

Shahidi: Mimi na afisa mwingine wa polisi Inspekta Omar tulimpeleka mshitakiwa katika mahakama ya Mwanzo Kinondoni kwa ajili ya kutoa maelezo ya ungamo.

Wakili: Wakati anatoa maelezo ya ungamo kwa mlinzi wa amani wewe na afisa mwenzako mlikuwa wapi?

Shahidi: Tulikuwa nje.

Wakili: Katika upelelezi wenu mlifanya nini tena?

Shahidi: Machi 6, mwaka 2006 mshitakiwa PC Rashidi alitueleza kuwa yuko tayari kutuonyesha eneo halisi la tukio.

Wakili: Tukio lipi hilo?

Shahidi: Tukio la majambazi ambao walidaiwa kuuawa katika msitu wa Pande huko Mbezi Luis.

Wakili: Je mlikwenda huko?

Shahidi: Machi 7, mwaka 2006, saa 4 asubuhi tuliondoka mimi na maafisa wengine tuliokuwa tukifanya upelelezi na kwenda huko katika msitu wa Pande.

Wakili: Je ni nani alikuwa akiwaonyesha njia?

Shahidi: Mshitakiwa ndiye alikuwa akituonyesha njia.

Wakili: Eneo hilo likoje?

Shahidi: Ndani ya msitu wa Pande hakuna makazi ya watu lakini kuna barabara inayofika eneo hilo.

Wakili: Nyie kama timu ya upelelezi mlifanya nini?

Shahidi: Katika msitu ule yalipatikana maganda mawili ya risasi yanayoweza kutumika kwenye bunduki aina ya SMG na SAR na pia tuliona damu iliyokuwa imeganda na kuchanganyika na udongo.

Wakili: Baada ya hapo mlifanya nini?

Shahidi: Tulichukua sampuli ambayo ilipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa ajili ya kubaini kama damu ile ni ya binadamu au ya mnyama.

Wakili: Nini matokeo ya uchunguzi huo wa Mkemia Mkuu?

Shahidi: Matokeo yalionyesha kuwa ile ilikuwa ni damu ya binadamu.

Wakili: Katika upelelezi wenu mlifanya kitu gani tena?

Shahidi: Tulipiga picha za video na za kawaida na pia tulichora ramani ya eneo lile.

Wakili: Mshitakiwa alieleza nini zaidi ya hayo?

Shahidi: Alieleza kuwa yeye binafsi hakuhusika kuwapiga marehemu risasi bali Koplo Saad ambaye bado hajakamatwa ndiye aliyehusika.

Pia alidai marehemu hao walikuwa wakitolewa mmoja mmoja kutoka kwenye gari na kulazwa kifudifudi na kupigwa risasi.

Wakili: Baada ya kumaliza mlielekea wapi?

Shahidi: Mshitakiwa alidai kwamba katika ya Januari 17 na 18 mwaka 2006 waliagizwa na Bageni (Mshitakiwa wa pili) waende Bunju wakafyatue risasi na kumletea maganda ya risasi na alienda huko akiwa na Koplo Saad.

Wakili: Je mlienda huko?

Shahidi: Tulienda na mshitakiwa alituonyesha walikofyatulia risasi.

Wakili: Je walifyatua risasi ngapi?

Shahidi: Rashidi alidai walifyatua risasi 3 na mwezake Koplo Saad alifyatua risasi 6.

Wakili: Nyie kama timu mlifanya nini zaidi ya hayo?

Shahidi: Pia tulipiga picha za video na za kawaida.

Wakili: Baada ya shughuli hiyo mlifanya nini tena?

Shahidi: Tulienda Makao Makuu ya Upelelezi na kuandika tena maelezo ya Rashidi ili kueleza aliyokwenda kutuonyesha.

Wakili: Nyie kama wapelelezi mlifanya nini tena?

Shahidi: Tulienda kuangalia kitabu cha kumbukumbu za silaha kuona kama bunduki hizo zilichukuliwa kihalali na kwamba risasi ngapi zilitumika.

Wakili: Kitabu hicho ni cha kituo kipi?

Shahidi: Ni cha kituo cha polisi cha Oysterbay.

Wakili: Katika kitabu hicho mliona nini?

Shahidi: Tuliona kuwa Januari 14, mwaka 2006 Rashidi alipewa silaha na risasi 30 na alirejesha Januari 15 mwaka 2006 na alirudisha risasi zote lakini kulionekana kumefutwafutwa na kuandikwa risasi 27. Kwa Coplo Saad ilionyesha zilipungua risasi 9.

Wakili: Rajabu alikamatwa lini na alipelekwa lini mahakamani?

Shahidi: Alipelekwa Machi 8, mwaka 2006.

Wakili: Shahidi ulisema mliandika maelezo ya mshitakiwa wa pili SSP Bageni, je alisema nini kuhusu shitaka linalomkabili?

Shahidi: Bageni hakukiri kosa moja kwa moja bali alidai kulikuwa na mapambano kati ya polisi na majambazi na yeye alitoa maelekezo majambazi hao wauwawe.

Wakili: Bageni alikueleza matokeo yoyote ya mapambano hayo na majambazi?

Shahidi: Alidai mapambano hayo, yalitokea katika ukuta wa posta Sinza na baada ya mapambano hayo waliokuwa wakidaiwa ni majambazi walijeruhiwa.

Wakili: Kilifuata nini baada ya maelezo hayo?

Shahidi: Februari 20, mwaka 2006 tuliwafikisha washitakiwa mahakamani.

Wakili: Siku hiyo washitakiwa walikuwa wangapi?

Shahidi: walikuwa washitakiwa 8.

Wakili: Februari 22 ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa ofisini na tuliondoka na maafisa wengine kwenda eneo la tukio Sinza block C Palestina karibu na maduka.

Wakili: Kwanini ulienda Sinza Block C badala ya kule alikosema Bageni?

Shahidi: Tulienda huko baada ya kupata maelezo ya mashahidi kwamba wanaodaiwa kuwa ni majambazi walikamatwa eneo la Sinza C.

Wakili: Madhumuni ya kwenda huko yalikuwa nini?

Shahidi: Tulienda huko kwasababu hao marehemu walidaiwa kuwa walifika kwa mama Bernadetha Lyimo (shahidi wa 2) kumpelekea fedha na huko tulimkuta pia Majatta Kayamba (shahidi wa 6).

Wakili: Baada ya hapo kilifuata nini?

Shahidi: Mjatta alituonyesha mahali ambapo marehemu walikuwa wamepaki gari lao na nyumba ambayo marehemu Sabinus alikwenda kukabidhi fedha kwa mama Bernadetha.

Wakili: Nyie kama wapelelezi mlifanya nini?

Shahidi: Tulipiga picha za video na za kawaida pamoja na kuchora ramani ya eneo lile.

Wakili: Baada ya hapo kilifuata nini?

Shahidi: Tulienda eneo la Sam Nujoma mahali ambako kunadaiwa gari la kampuni ya Bidco liliporwa fedha.

Wakili: Katika upelelezi wenu mlifanya nini hapo?

Shahidi: Tulichora ramani na baada ya hapo tuliondoka kwenda posta kulikodaiwa kuwa kulitokea tukio la mapambano kati ya majambazi na polisi.

Wakili: Eneo hilo likoje?

Shahidi: Pembeni yake kuna nyumba na gereji.

Wakili: Kutoka ukuta wa posta hadi gereji kuna umbali gani?

Shahidi: Kwa kukisia ni kati ya hatua 10 hadi 15?

Wakili: Je urefu wa ukuta wa posta ukoje?

Shahidi: Ukuta ni mrefu kiasi kwamba huwezi kuchungulia upande wa pili.

Wakili: Katika ukuta huo, mliona nini?

Shahidi: Tuliona matundu manne yanayodaiwa kuwa yalipigwa na bunduki aina ya SMG.

Wakili: Matundu hayo yalikuwa na umbali gani?

Shahidi: Hayakupishana sana.

Wakili; Ulivyoyaona yalipigwaje?

Shahidi: Yalipigwa kwa usawa.

Wakili: Kitu gani kingine uliona.

Shahidi: hakukuwa na kitu kingine.

Wakili: Je mlihoji majirani?

Shahidi: Tulihoji na walisema hawakuwahi kusikia milio ya risasi siku ya Januari 14, mwaka 2006.

Wakili: Je mlifanya uchunguzi kujua silaha zilizotumika?

Shahidi: Zilitumika SMG.

Wakili: Mlijua zilitoka kituo kipi na zilitumika ngapi?

Shahidi: Zilitoka kituo cha polisi cha Oysterbay Dar es Salaam na zilitumika SMG mbili.

Wakili: Mlipeleleza kujua walikabidhiwa askari gani?

Shahidi: Moja alipewa Coplo Saad na nyingine alipewa Constebo Rashidi (mshitakiwa wa 11).

Baada ya mahojiano hayo wakili Mzikila aliiomba mahakama iende maeneo mbalimbali ya tukio ambayo shahidi huyo, ameyazungumzia katika ushahidi wake yakiwemo msitu wa Pande ulioko Mbezi Luis ambako wafanyabiashara hao, wanadaiwa kuuawa.

Kutokana ombi la wakili Mzikila, kesho Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, mawakili na waandishi wa habari watakwenda kutembelea maeneo ambayo, shahidi huyo, amezungumzia jana mahakamani.

Jaji Kiongozi Salum Massati alikubali na kuahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea tena.



Source: Mwananchi
 
Tukio la jana nilipojing'ata ulimi wakati natafuta nyama 😬😬😬
 
Back
Top Bottom