Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,715
- 13,467
UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA ILIYOTOLEWA NA HALMASHAURI YA MJI WA IFAKARA KUHUSU VYOMBO VYA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA
Oktoba 10, 2023
Idara ya Habari (MAELEZO) na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali imeona taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii iliyotolewa tarehe 9 Oktoba, 2023 na Halmashauri ya Mji wa Ifakara kuhusu katazo la Vyombo vya Habari vya kujitegemea na Waandishi wa Habari kutoa taarifa, habari na matangazo yanayohusu Serikali.
Taarifa hiyo imeenda mbali zaidi na kusema kuwa ni kosa kisheria, kwa mujibu wa kifungu cha 7(1)(b), (iv) cha Sheria ya huduma za Habari ya mwaka 2016 kwa Chombo cha Habari binafsi au Mwandishi wa Habari kuzungumza masuala mbalimbali ya Serikali (national issues) bila idhini au mwongozo wa Serikali.
Idara ya Habari inapenda kuujulisha umma kuwa tafsiri ya kisheria iliyotolewa kuhusu suala hilo SIYO SAHIHI. Sheria ya Huduma za Habari Sura ya 229 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2023, haijakataza wala kuzuia Vyombo vya Habari vya kujitegemea na Waandishi wa Habari wa kujitegemea kutoa taarifa za Serikali isipokuwa kwa taarifa ambazo zimezuiliwa kwa mujibu wa Sheria.
Kwa mujibu wa kifungu cha 7 (1), Sheria imeweka bayana haki za msingi za Vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari ambazo ni kutafuta, kuchakata na kutangaza au kuchapisha habari. Aidha, Kifungu cha 7(2), (b), (iv) kinaeleza wajibu wa Vyombo vya Habari binafsi katika kutangaza masuala yenye umuhimu kwa taifa na si katazo wala kosa kwa vyombo hivyo kutoa taarifa, habari na matangazo ya Serikali.
Idara ya Habari (MAELEZO) na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali inatoa wito kwa Vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa uhuru na kutoa ushikiriano kwa Serikali hasa katika kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita na vile vile kuzingatia Sheria, Kanuni, weledi na maadili ya uandishi wa habari.
Mobhare Holmes Matinyi
MKURUGENZI IDARA YA HABARI NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI