Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 46,838
- 67,234
Karne ya 18 hadi 20 huko Ulaya na Marekani kanisa Katoliki huko Ulaya na Marekani walikuwa na vituo vya kurekebisha tabia kwa wanawake hasa mabinti wa makundi mbalimbali wakiwemo single mothers, makahaba, wanawake walioonekana wajeuri na walioonekana mzigo kwa familia zao.
Wanawake wengi waliopelekwa katika hivyo vituo walikuwa mabinti. Walikuwa wanafanyishwa kazi za sulubu za udobi, ushonaji na usafi kama malipo ya dhambi zao wakisimamiwa na masisita wakali mchana na usiku. Walikuwa wakipata mapumziko kidogo sana, kwa ujira kiduchu au bila ujira wowote. Walifanya kazi katika mazingira magumu sana.
Baadaye hivi vituo vilikujwa kufungwa mwishoni mwa karne ya 20 na kuna baadhi ya wanawake huko Ireland walilipwa fidia.