Masanja: Nimenunua BMW X6 kama mtu mwingine anavyonunua baiskeli

Nilisikia mahojiano toka mwanzo mpaka mwisho na alikuwa anavunja mbavu hasa toka watizamaji mpaka waliokuwa wanamhoji,wala hakujibu kwa kujigamba kama watu wanavyotaka kuaminisha hapa
 
Masanja...waoneshe na combine harvester zako ndipo watajua wewe nani ktk kusaka pesa ktk kilimo. Big up!
 
hilo BMW lake mbona halijamsaidia kupata ubunge huko kwa Filikunjombe? ajue halina thamani yoyote kwa jamii na asubiri tu mirija yake kuzibwa na Magufuri
 
Mjinga sana, maneno yanafaa kutamkwa na Dr. Mengi, Bkharessa na & Gwajima, profesa tibaijuka(BIBI wa pesa ya mboga), chenge,(babu wa vijisenti) na mzee wa msoga na watu wa kaliba hiyo....

Sio yeye. Masanja hana hela ya kununua BMW kama anavyonunua baskeli.

Gari zina charge nyingi sana. Baskeli na gari tofauti sana katika ununuzi, kuanzia kutoa hela benki nk na ikipata ajali anaweza kukesha miaka kuikarabati.

. You never know..Hope alikua anachekesha watu, manake ndo kazi ya ze komedian kama yeye.

Maskini akipata mata** ulia mbwata.
Hiyo methali hapo mwisho haihusiani na Masanja. Masanja habweteki.
 
Mtumishi wa mungu akijivuna na kujitapa!!
Dini imekuwa manukato now days, ninavyojua mimi watu hawa wanatakiwa wawe humble na wenye kujinyenyekeza.
Rejea hotuba ya yesu mlimani.
 
Hatuchukii mafanikio yake ila Ana majivuno akiwabeza vijana waliosoma na kukosa ajira.Anakosea majivuno Tu.
Kwani uongo? Vijana wengi tuliosoma hatupendi kujichanganya katika kazi tofauti na za kuvaa tai, ndo maana mpaka kesho msomi atakuwa mtumwa wa mwenye pesa kwan matajiri asilimia kubwa hawana elimu tunayojigamba nayo. Acha Masanja awe mfano kwetu
 
vijana ngwasuma.
wanasema "wale wale tumeshajua wale..
NIKINUNUA GARI WANICHUKIA OOOH!"
 
Wakuu, hapa Bongo hamna hata msanii anaejisifia.. Wasanii wa Bongo ni wapole kinyama lakini sometimes tunawaonea..kuna watu wanajisifu kwa mkwanja wao bhana... Kina Prezzoo, Jaguar... Hivi wabongo tungekuwa marekani ambako mtu kama Birdman na Rick Ross wanaandika album nzima kujisifia tu sijui tungekuwa tunajiskiaje..
Mi naona msanii ye ajivunie tu success yake.. Iwe chachu kwetu wengine tuendelee kuhustle...
 
Masanja hajawahi kuigiza mambo hayo, wakati huo alikua kwenye kikundi cha Sanaa cha mtaani Tabata!
Masanja ndio anayepondea wengine. Nani alimuuliza atutajie kua anaweza kununua Gari. Haituhusu.
Wasanii wa bongo njaa tu. Wengi walijipendekeza kwenye mfumo. Ndio maana wameinuka.
 
Huyu ni mfano wa kuigwa maana ni msanii anafanya..sanaa ila katka maisha jamaa haigizi% keep moving mazee
 
Watu watamponda sana ila siku zote ukimshirikisha Mungu, ukiwa na nidhamu na ujafanya kazi kwa bidii mafanikio hayajifichi.
Namkumbuka Masanja wa miaka ile alipokuwa mambo hayo na akina Joti na Mpoki, leo tunaona mafanikio yao
Mambo hayo ipi hiyo? Kama ni ya akina Bishanga, Rich na kundi lao siyo kweli, hakuwahi kuwepo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom