SoC03 Mapungufu yaliyopo katika malezi ya watoto na nafasi ya wataalam

Stories of Change - 2023 Competition

Adam Irembe

New Member
Jul 16, 2023
1
1
Malezi ni jambo ambapo Kila mtu/mwanajimii anapaswa kulitimiza. Malezi pia hutafsiria kwa namna tofauti kulingana na mtazamo wa wahusika, ngazi za elemu na pia aina za kazi au kipato hivyo kutupatia aina za malezi ambazo ni kulingana na maisha yetu na utamaduni.

Mara nyingi tumekua na kawaida ya kuchanganya aina za malezi ambazo tunazisoma Kwenye vitabu na hatuzingatii utamaduni wetu halisi. Hivyo Malezi ni namna ambavyo mtoto anakuzwa kwa lengo la kupatiwa misingi sahihi Ili aweze kujitegemea hapo baadae.

Zipo asasi mbalimbali ambozo zinajihusisha na malezi ya watoto kama ifuatavyo.

Wazazi, hilo kundi muhimu sana katika malezi ya watoto na kundi hilo ndilo kibailojia hutupatia mtoto. Wazazi pia lich kuwa wao ndio wahusika wakuu lakini naonpia wamegawanyika katika makundi tofauti tofauti. Lipo kundi la wazazi ambao ni wanandoa kwa namna moja ama nyingine Hawa wanakua wamefata taratibu zote za kijami hivyo hupelekea kua na ukaribu katika malezi kutokana na heshima na lengo la ndoa pia ni kupata mtoto. Hivyo kundi Hilo hujikita zaidi katika malezi ya watoto kwa kuelemea zaidi katika mapenzi dhidi ya watoto wao na hivyo baadhi Yao kushidwa kuwaonya hata pale wanapokosea vile vile lipo kundi la wazazi ambao siyo wanandoa likijumuisha wapenzi, au mimba zisizo tarajiwa ambapo kundi Hili hutawaliwa na migogoro baina ya pande mbili katika utimazaji wa majukumu y ulezi na kumtunza mtoto.

Walezi, Hilo kundi la pili katika ulezi wa watoto ambapo siyo wazazi halisi wa mtoto husika, mara nyingi walezi huweza kua baba mkubwa, baba wadogo, mjomba shangazi, ndugu au watu wa karibu na wenye huruma. Katika kundi la walezi pia wameganyika katika makundi madogomadogo, wapi walezi amboa ni wa kukabidhiwa, wapo walezi wa kujitolea.kundi Hili hutawaliwa zaidi utimazaji wa stahiki na mahitaji ya mtoto. Hivyo kipaumbele katika kundi Hili n kumpatia mtoto husika mahitaji yake yote kama vile elimu chakula na mavazi.

Vituo vya kulelea watoto, hizi ni sehemu ambazo zimetegwa mahususi kwaajili ya kulea watoto wakiwa katika kundi lenye idadi ya namba flani, katika kundi Hili watoto hukusanywa kutoka maeneo mbalimbali na kuwekwa sehemu moja ambopo inapaswa waishinkama familia, na pia katika kundi Hili limejikita zaidi katika kuwatia watoto huduma ikiwa ni pamoja na elimu, maadilii, afya makazi na mavazi na pia uendeshaji wa vituo hivi maranyingi hukubwa na changamoto mbalimbali kama uhaba wa fedha miundombinu na idadi ya wahudumu kuto kuwiana na idadi ya watoto.

Wadada wa kazi,(Yaya) Hawa ni wasichana au wanawake ambao Huajiriwa kwaajili ya kumtunza na kumlea mtoto na pia siyo wazazi Wala wataalamu katika sekta ya malezi Bali ni wafanyakazi ambao mwisho wa siku watahitaji mshahara hivyo wao lengo lao ni kumtunza mtoto kulingana na matakwa ya wazazi wa mtoto husika. Kundi Hili pia Kuna mda hufanya kazi katika mazingira magumu na manyanyaso hivyo kupelekea mda mwingine kuwadhuru watoto au kukimbiaa majukumu ya malezi hivyo wao hawana kipaumbele katika malezi Bali huwakilisha mawazo ya wazazi na matakwa katika malezi.

Baadaa ya kutizama baadhi ya makundi/taasis na mapuufu yaliyopo katika zinazoshughulika na malezi pamoja na majukumu Yao ya msingi ambayo huyatimiza katika malezi majokwa moja tunabaini nafasi ya wataalamu wa malezi kama ifuatavyo.

Kwanza ufuatijiaji wa kanuni za msingi katika malezi na makuzi ya mtoto, endapo mtaalaamu wa malezi atashiriki moja kwa moja katika malezi atakua na uwezo wa kutuwekea wazi ni kipi kifanyike katiki umri sahihi wa mtoto mfano suala kumuadhibu mtoto wazazi pamoja na walezi hutoa adha u kwa kuangalia upande wa kosa na hawaangalii umri wa mtoto hivyo kupelekea kumuumiza mtoto kimeili na kiakili hivyo katika maendelea ya kiakili humjengea mtoto kutokijiami, kuogopa na pia kutokua na uwezo wa kueleza Yale yanayo msibu pamoja na kukosa uhuru. Pia suala la kumpongeza na kumpatia zawadi ni miongoni mwa vitu muhimu hivyo mtaalamu kutokana taaluma aliyokua nayo lazima atatubanishia ni wapi adhabu inastahiki na katika umri gani na kwa kiasi gani na ni katika mazingira gani pongezi na zawadi zinahitajika.

Pili, utambuzi wa hatua za ukuaji na mabadiliko ya ukuaji kimwili, kiakili na kihisia. Uwepo wa wataalamu utachagiza kutambua na kubaini hatua na mabadiliko anayotakiwa kupitia na anayopitia mtoto tutaweza kutambua ni katika umri gani mtoto ataanza utambuzi binafsi, utambuzi wa wanao mzunguka sambamba na Hilo pia ufanyaji kazi wa viuongo vya mwiki kawma mikono katika kazi za mikono,pamoja na shughuli kama kukimbiaa. Hivyo kutoka na uwezo wa mtaala endapo kutakua na changamoto yeyote ataweza kuibaini na kuitatatua kabla haijawa sugu na kumletea shida mtoto na mzazi katika kutimiza majukumu yake.

Tatu, kutoa tathimini juu ya maendelea ya ukuaji wa mtoto, Ili malezi yaweze kufanikiwa kwa usahihi lazima tathimini juu ya uelekeo na ukuaji wamtoto itolewe Ili kuweza kutambua maendelea ya mtoto yapo katika upande chanya au upande hasi tathimini itajikita katika kusitiza vitu vya muhimu kwa mtoto kama vile lishe, mda wa kupumzika, uwiano wa baadhi ya majukumu na kucheza.

Nne, ushirikiswaji wa wataalamu katika malezi utasaidia utambuzi wa haraka wa baadhi ya changamoto kutoka na tabia ambo mtoto atakua anazionesha, maranyingi changamoto huweza kutoka na matatizo kama vile kutosikia vizuri, kutokuaona vizuri ambopo baadhi wa watoto wenye changamoto hizi huweza kuitwa wa jeuri na hivyo kukosa haki ya malezi stahiki.

Tano, ushirikiswaji wa wataalamu katika malezi, utasaidia kuwaweka watoto katika makundi stahiki kutoka na kile wanachoweza kufanya, kupenda hususan vipawa na vipaji wataalamu wa malezi wanayotaaluma ambayo huweza kutambua undani wataabia na uhusiano uliopo na kipaji husika cha mtoto hivyo itapunguza wimbi la kuwalazimisha watoto kufanya vitu wasivyo penda na badala kuwahimiza katika vile wanavyopenda na kupelekea kuwa watulivu wafuatiliaji na wasikivu hivyo kurahisisha malezi kwa wahusika.

Hivyo basi Ili kujenga jamii iliyo bora katika wakati huu tulionao (mabadiliko ya Sayansi na technolojia) lazima tuwape nafasi wataalamu katika ngazi zote za malezi na makuzi ya mtoto kwa sababu wao wanayo taaluma ambayo imefata hatua za kisayansi kwa kuthibitishwa na tafiti katika mapenzi na makuzi ya watoto.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom