N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,320
- 10,706
Tangu maonesho ya 2021 SabaSaba yaanze hapa Kilwa Road Dar es salaam hapa kwenye Banda la Karume wafanyakazi wa TANTRADE wanachelewa sana kufungua mabanda/Maholi makubwa wanafungua saa nne au saa tatu na dakika zilizozosonga sana.
MADHARA YA KUCHELEWA KUFUNGUA
PIA Rekebisheni miundombinu kwa kweli imechakaa sana kuanzia mabanda makubwa, toilets na hata walk ways...hivi ni kweli kwamba TANTRADE kwa kushirikiana na WIZARA hamuwezi kupiga Pavers kwenye Walkways zote za humu uwanjani? vumbi linachafua bidhaa za waoneshaji na kupunguza ubora...uwanja huu ni tunu katika kukuza BIASHARA hapa nchini...Tafadhali rekebisheni. TUNAONA.
MADHARA YA KUCHELEWA KUFUNGUA
- Waonyeshaji wanakosa muda wa kutosha kuandaa mabanda yao
- Ni usumbufu mkubwa kwa waonyeshaji ikizingatiwa kuwa waonyeshaji wengi wanafika kwenye mabanda mapema sana
- Mamlaka inawapora waonyeshaji muda wao stahiki wa kuanza maonesho ikizingatiwa kuwa muda wenyewe ni mchache yaani saa 4 asubuhi hadi saa 12
- Kama issue ni usalama kwa ambao hawajafika tafuteni modality nzuri ya kuhakikisha angalau saa 3 asubuhi watu wanaingia kwenye mabanda yao ili kuanza kuonyesha
- Imarisheni ulinzi ndani ya mabanda wakati wa asubuhi kulinda assets za wale ambao bado hawajafika. Kazi hii vijana wa Skauti mlio nao wanaweza kuifanya vizuri.