Mambo 6 kuhusu Majeruhi ajali ya Wanafunzi Arusha waliofatwa na Ndege kupelekwa Marekani

Screen-Shot-2017-05-13-at-11.41.41-PM.png

Ajali ya basi dogo la Wanafunzi Karatu Arusha iliua 32 weekend iliyopita na kuacha Majeruhi watatu ambao wamekua wakitibiwa kwenye Hospitali ya mkoa wa Arusha, Mount Meru.

Mbunge wa Singida kaskazini Lazaro Nyalandu amekua mstari wa mbele kuhakikisha watoto hawa wamesaidiwa kimatibabu pamoja na kisaikolojia ambapo juzi May 11 aliongea na AyoTVna millardayo.com Arusha.

1. ‘Ninapenda kutangaza kwa furaha kubwa sana kwamba tumefanikiwa kupata Ndege kubwa inayoweza kutumika kama ‘AMBULANCE‘ angani na inaondoka North Carolina Marekani kuja moja kwa moja Kilimanjaro Tanzania kuwachukua hawa majeruhi’ – Nyalandu

2. Baada ya taarifa hizo, Ndege hiyo yaSamaritan Purse DC 8 N782SP imewasili Kilimanjaro Tanzania leo May 13 2017 ikiwa na Marubani wanne na Wahudumu wake 7 tayari kuwabeba Majeruhi hao ambao wataambatana na wazazi wao mpaka Marekani kwenye matibabu.

Screen-Shot-2017-05-13-at-10.45.14-PM.png

Mmoja wa Marubani wa Ndege hiyo akiwa na Mbunge Lazaro Nyalandu kwenye uwanja wa Ndege KIA.

Rubani wa Ndege hiyo amewaambia Waandishi kwenye uwanja wa ndege Kilimanjaro (KIA) kwamba wataondoka kesho na watasimama Cape Verdekuweka mafuta na kisha kuelekea Marekani moja kwa moja na wanatarajia kuingia kesho yake usiku.

Screen-Shot-2017-05-13-at-10.54.08-PM.png

Tayari Wazazi wa watoto hao watatu wameshapata VISA za kuingia Marekani pamoja na watoto wao na wako tayari kwa safari.

3. Ndege hii imetolewa na shirika laSAMARITAN’S PURSE (mfuko wa Msamaria) linalosimamiwa na mtoto wa Mwinjilisti mkubwa wa Marekani Franklin Graham, familia yao baada ya kupelekewa habari za kilichotokea kwenye ajali ya Karatu walikubali kuituma ndege hiyo kutoka Marekani kuja kuwachukua Majeruhi Tanzania.

Screen-Shot-2017-05-13-at-11.31.51-PM.png

Mwinjilisti Franklin Graham

4. Kwenye Ndege hiyo kuelekea Marekani itawabeba Mama wa watoto hao watatu, itawabeba pia Nesi mmoja na Daktari mmoja wa Kitanzania ambao wataendelea kuwahudumia watoto hao ndani ya ndege hiyo yenye uwezo wa kutoa huduma kama Ambulance pia.

5. Ndege hiyo ikishatua North Carolina,SAMARITAN’S PURSE wameandaa Ndege nyingine ambayo pia inaweza kufanya kazi kama AMBULANCE angani iitwayo AIR AMBULANCE na kuwachukua hadi jimbo la Iowa ambako Hospitali ya Mercy imekubali kuwatibu Wagonjwa hawa bure kwa muda wote watakaohitaji matibabu.

Screen-Shot-2017-05-13-at-11.38.20-PM.png


6. ‘Tukiwa Marekani tutakua na haki ya kuangalia kinachoendelea ambapo Watanzania na marafiki wa Tanzania wataopenda kuchangia kwa M-PESA na njia nyingine wataruhusiwa, tayari shule 3 za Arusha Braeburn Internation, St. Costantine na International School of Moshi zimejiunga kuandaa mfuko ambao utatumika kuwachangia’ – NYALANDU
Amina Mungu ni mwema.
 
kwani Bombardier isingeweza kuwasafirisha hawa watoto kuliko ndege hii ikawafuata kwa gharama kubwa, any way mungu akubariku mh nyalandu kwa
msaada wako. pia mungu awaponye haraka majeruhi hawa
Hiyo ndege imekuja kama msaada,
Halafu bombadia ni ya abiria hiyo ndege ni ambulence
 
Kingwangala wala hana story.... Yupo kwenye mikakati madhubuti ya kupambana na vita ya mashoga kwanza......

Serikal haijatoa hata mia na wamepiga hela ya rambi rambi....
Hii Serikali inatumia majanga kupatiapo Pesa ni aibu sana,na imesababisha Watu kutokuwa na nia kwenye uchangiaji kwa waliopata matatizo,jambo ambalo lilikuwa siyo Utamaduni wetu
 
Mungu mkubwa, naamini kwa jitihada hizo na mwenyezi Mungu atawafanyia wepesi kurudi katika hali yao ya kawaida.
Na ingependeza sana kwa wao kubaki huko huko hadi wahitimu elimu juu; huku bongo wawe wanakuja kusalimia tu.
 
Ha ha ha haaaa...kwa jinsi asivyokuwa na subra, ataenda kuwajulia hali siku akitaka magazeti yamuandike tena
Aombe lifti aongozane na wangonjwa, vitanda naona vipo vingi ndani ya ndege alalie kimoja mpaka Marekani
 
Tunahitaji kutumia akili,nguvu nyingi na rasilimali fedha kuimarisha hospitali zetu,ziwe na wataalam na vifaa vya kisasa ili huduma muhimu zipatikane humu nchini,kuliko kutegemea misaada na kutumia fedha nyingi kufata matibabu nje ya nchi.
Hao majeruhi wamepelekwa MOI wakaonekana hawawezi kuhudumiwa?Nawasiwasi na Agenda nyingine nyuma ya pazia juu ya swala la majeruhi hawa.Nawaombea Mungu wapone,ila naona gharama zinazotumika zingeweza kuimarisha kitengo kimoja wapo kwenye hospitali zetu,na kuwasaidia wahanga wengi zaidi (najiuliza mwenyewe)
Ukumbuke gharama si za serikali.
Serikali haijatoa chochote hapo labda kuruhusu hiyo ndege ITUE KIA
 
nadhani Nyalandu amesaidia sana katika hilo, sina hakika. Kama ndivyo Mungu ambariki huyo Mbunge
 
Siasa ndugu inaharibu sana tena alietoa hii Killard ayotv unategemea proffesionalism kweli? Ni vururu vururu tu ilimradi nyalandu kasifiwa
Kadri nilivyoisoma habari,ni kama maneno ya nyalandu mwenyewe akiwa anahojiwa
 
Franklin Graham ndiye yule 'NABII' wa 'mwisho' ambae wanaomwamini wanadai alitabiriwa Katika agano la kale kwenye Biblia!?
Hili ni fumbo kubwa sana kwenye ulimwengu wa roho! Mwenye Enzi Mungu muumbaji wa vyote! Awabariki watoto wetu watatu awalinde kwa ulinzi wote! Shukrani kubwa imwendee Franklin Graham na family yake yote Mola amzidishie pale alipotao kwa ajili ya watoto wetu wakitanzani! Ni baraka kubwa sana kwa kweli, AMUN RA
 
Tuwabariki na kuwaombea safari njema! Kuliko kukebehi
 
Watu vichwa kama Nyalandu wanatupwa porini halafu majitu ya ajabu ajabu ndio yanapewa mashavu
 
Tunahitaji kutumia akili,nguvu nyingi na rasilimali fedha kuimarisha hospitali zetu,ziwe na wataalam na vifaa vya kisasa ili huduma muhimu zipatikane humu nchini,kuliko kutegemea misaada na kutumia fedha nyingi kufata matibabu nje ya nchi.
Hao majeruhi wamepelekwa MOI wakaonekana hawawezi kuhudumiwa?Nawasiwasi na Agenda nyingine nyuma ya pazia juu ya swala la majeruhi hawa.Nawaombea Mungu wapone,ila naona gharama zinazotumika zingeweza kuimarisha kitengo kimoja wapo kwenye hospitali zetu,na kuwasaidia wahanga wengi zaidi (najiuliza mwenyewe)
Hapo hakuna hata senti ya Tz.
 
Back
Top Bottom