Ni kubwa sana kiumbo, ikiwa kwenye hadhira,
Ni Mamba kama wa Mombo, Sema ye hana madhara,
Yakichambuliwa mambo, yatakutia hasira,
Mamba huyu mamba gani, mbona hawezi kung'ata?
Hukaa kimya majini, hutoka mwingine mwaka.
Huletwa vingi vitini, kusoma walo potoka,
Vinasomwa kwa makini, imara bila mashaka,

Huishia tu kufoka, kisha huyo huondoka,
Kama mbwa hubweka, kutaja vyao vichaka,
Ila hana mamlaka, kuwaadhibu vibaka,

Wako wapi wahusika, waliopewa dhamana,
Wasotaka kuwashika, walotajwa mwaka jana,
Au nao wahusika, asa tusemaje tena?

Sioni haja kuwepo, bora tukwepe gharama,
Ni kufukuza upepo, siioni yake dhima.
Kuwajibika kuwepo, irudi yake heshima,
Walishayatoa meno, hawahofii kung'atwa!