Mamba huyu mamba gani, mbona hawezi kung'ata?

Swali ulilouliza, jibu nitakupatia,
Tulia nitakujuza, si gumu nakuambia,
Ya mamba unauliza, wa kijiji nachangia,
Mamba asiyeng'ata, si mamba huyo mjusi!

Huyo mamba asong'ata, lazima awe mjusi,
Asiyeweza kunyata, mwenye rangi za tausi,
Mwenye mwendo kama bata, na macho kama mkisi,
Mamba asiyeng'ata, si mamba huyo mjusi!

Macho anavyokodoa, kama kabanwa mlango,
Mjusi kajipodoa, na nyororo yake shingo,
Kelele anazotoa, na mwendo wenye malingo,
Mamba asiyeng'ata, si mamba huyo mjusi!

Beti nne nazifunga, jawabu nimemaliza,
Kama gwiji nimepanga, msije kuniuliza,
Mjusi nimemnanga, nang'ata sijapuliza,
Mamba asiyeng'ata, si mamba huyo mjusi.

Na. M. M. Mwanakijiji (Tarumbeta ya Kijiji).
Uhamishoni USA
 
Swali ulilouliza, jibu nitakupatia,

Mamba asiyeng'ata, si mamba huyo mjusi!

Beti nne nazifunga, jawabu nimemaliza,
Kama gwiji nimepanga, msije kuniuliza,
Mjusi nimemnanga, nang'ata sijapuliza,
Mamba asiyeng'ata, si mamba huyo mjusi.

Na. M. M. Mwanakijiji (Tarumbeta ya Kijiji).
Uhamishoni USA
Kama si mamba mjusi, hatufai abadani,
Anitia wasiwasi, kaziye ya kazi gani,
Anamaliza ukwasi, wa kumtunza majini,
Mjusi kafata nini, Nasi tulitaka mamba.

Anaucheza mchezo, wenye swali lisojibu
Anipatia mawazo, yupi wa kumuadhibu
Kushindwa kazi ni kwazo, kwa tulompa wajibu.
Mjusi kafata nini, Nasi tulitaka mamba.

Kongole kwa kunijibu, nimeupata mwangaza
Hana sauti ni bubu, kwa wanokula kusaza,
Maovu hawezi tibu, kabaki kutushangaza.
Mjusi kafata nini, Nasi tulitaka mamba.
 
Ni kubwa sana kiumbo, ikiwa kwenye hadhira,
Ni Mamba kama wa Mombo, Sema ye hana madhara,
Yakichambuliwa mambo, yatakutia hasira,
Mamba huyu mamba gani, mbona hawezi kung'ata?
Labda kwasababu ni Mamba wa baharini
Liinganisha na mamba jamii ya ziwani
 
Huyo ndie yule mamba, mwendapole atakavyo.
Hana haraka ya timba, mfanowe wa tsavo.
Atembea kwa kutamba, visa wakenya wanavyo.
Dharau mzifanyavyo, awaona majipamba

Awaona mwajipamba, kwa rangi za hovyohovyo.
Myajuayo kwa namba,mwanvisha asonavyo.
Dume ameshaliramba, bakini kusonya ovyo.
Aogele atakavyo,bara pwani akitamba,

Huyo ndie yule mamba, hashughuliki na nyie kenge.

,
 
Mamba meno anayo ila ni meno ya mpira, kila anapojaribu kula kitoweo meno yake yanakutana kwa mbonyeo wa kuvimba.
 
Back
Top Bottom