The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 1,144
- 1,952
Waziri wa kilimo Hussein Bashe kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X.
====
Salaam Ndugu zangu
Watanzania,Serikali imepokea taarifa kuwa Serikali ya Malawi imezuia kuingia kwa mazao ya kilimo kutoka Tanzania, yakiwemo unga, mchele, tangawizi, ndizi, na mahindi. Hatua hii imeathiri moja kwa moja shughuli za wafanyabiashara wetu wanaosafirisha bidhaa hizo kwenda Malawi.
Ni vyema ifahamike kuwa kwa kipindi cha miaka mitano, Serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kufungua soko la ndizi nchini Afrika Kusini bila mafanikio. Hali hii inafanana na changamoto tulizopitia kwa zaidi ya miaka kumi katika kufungua soko la parachichi, hadi pale tulipoamua kuchukua hatua za kulinda maslahi ya nchi yetu.
Kutokana na hali hii, na baada ya juhudi zote za kidiplomasia kufanyika bila mafanikio, ninapenda kuwataarifu yafuatayo:
1.Iwapo Serikali ya Malawi na Afrika Kusini hazitabadilisha msimamo wao kufikia Jumatano ijayo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo itazuia uingizwaji wa mazao na bidhaa zote za kilimo kutoka nchi hizo mbili.
2.Mizigo ya bidhaa za kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini haitaruhusiwa kupita ndani ya mipaka ya Tanzania, kuelekea bandari ya Dar es Salaam au nchi nyingine yoyote, hadi zuio hilo litakapoondolewa.
3.Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, ikiwa ni sehemu ya hatua za kulinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara wa Kitanzania.
Wafanyabiashara wote wenye mizigo ya kuelekea Malawi wanashauriwa kuacha mara moja kupakia bidhaa hizo, hadi hapo taarifa rasmi itakapotolewa kulingana na msimamo wa nchi husika.
Ninathibitisha kuwa kama Waziri mwenye dhamana, nimewasiliana kwa njia mbalimbali na Waziri wa Kilimo wa Malawi bila mafanikio ya kupata majibu rasmi.
Hatua hizi ni za kulinda heshima ya nchi yetu, uchumi wa wakulima wetu, na usawa katika biashara za kikanda