Malawi yazuia unga na mchele kutoka Tanzania, Serikali yaitaka nchi hiyo kufungua masoko, yatishia kuzuia bidhaa za kilimo za Malawi

Huyu Msomali katumwa au kajituma? Malawi wanaweza tumia Bandari ya Msumbiji na walisha peawa Bandari fulani na Msumbiji waiendeleze.
Kutoka Malawi hadi ilipo bandari hiyo ya Msumbiji kuna umbali gani kaka? Miundo mbinu ya barabara je? What about security ya mzigo from there to Maputo?
Au, ulikua na pendekezo gani kwa mhe waziri, alitakiwa afanye nini ili Malawi waache dharau?
 
Waziri wa kilimo Hussein Bashe kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X.
====

Salaam Ndugu zangu

Watanzania,Serikali imepokea taarifa kuwa Serikali ya Malawi imezuia kuingia kwa mazao ya kilimo kutoka Tanzania, yakiwemo unga, mchele, tangawizi, ndizi, na mahindi. Hatua hii imeathiri moja kwa moja shughuli za wafanyabiashara wetu wanaosafirisha bidhaa hizo kwenda Malawi.

Ni vyema ifahamike kuwa kwa kipindi cha miaka mitano, Serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kufungua soko la ndizi nchini Afrika Kusini bila mafanikio. Hali hii inafanana na changamoto tulizopitia kwa zaidi ya miaka kumi katika kufungua soko la parachichi, hadi pale tulipoamua kuchukua hatua za kulinda maslahi ya nchi yetu.

Kutokana na hali hii, na baada ya juhudi zote za kidiplomasia kufanyika bila mafanikio, ninapenda kuwataarifu yafuatayo:

1.Iwapo Serikali ya Malawi na Afrika Kusini hazitabadilisha msimamo wao kufikia Jumatano ijayo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo itazuia uingizwaji wa mazao na bidhaa zote za kilimo kutoka nchi hizo mbili.

2.Mizigo ya bidhaa za kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini haitaruhusiwa kupita ndani ya mipaka ya Tanzania, kuelekea bandari ya Dar es Salaam au nchi nyingine yoyote, hadi zuio hilo litakapoondolewa.

3.Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, ikiwa ni sehemu ya hatua za kulinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara wa Kitanzania.

Wafanyabiashara wote wenye mizigo ya kuelekea Malawi wanashauriwa kuacha mara moja kupakia bidhaa hizo, hadi hapo taarifa rasmi itakapotolewa kulingana na msimamo wa nchi husika.

Ninathibitisha kuwa kama Waziri mwenye dhamana, nimewasiliana kwa njia mbalimbali na Waziri wa Kilimo wa Malawi bila mafanikio ya kupata majibu rasmi.

Hatua hizi ni za kulinda heshima ya nchi yetu, uchumi wa wakulima wetu, na usawa katika biashara za kikanda
View attachment 3308278
Kifupi ni kwamba TISS na Polisi wapo makini sana kudhibiti wapinzani wa SASHA kuliko wanavyosaka intelijensia kusimamia uchumi!
Ni aibu kwamba wizara ilikosa briefings hadi wananchi walipoanza kuumia na kupost kwenye mitandao ya kijamii!
Inafikirisha zaidi kwamba wizara hailezi ni hatua zipi zilichukuliwa na zimekwamia wapi na kwanini?!
 
Huyu Msomali katumwa au kajituma? Malawi wanaweza tumia Bandari ya Msumbiji na walisha peawa Bandari fulani na Msumbiji waiendeleze.Yupo sahaihi

Huyu Msomali katumwa au kajituma? Malawi wanaweza tumia Bandari ya Msumbiji na walisha peawa Bandari fulani na Msumbiji waiendeleze.
Kwa hiyo wewe unashaurije?
Malawi wameshazuia bidhaa zetu na mazungumzo hayajazaa matunda.
 
Kutoka Malawi hadi ilipo bandari hiyo ya Msumbiji kuna umbali gani kaka? Miundo mbinu ya barabara je? What about security ya mzigo from there to Maputo?
Au, ulikua na pendekezo gani kwa mhe waziri, alitakiwa afanye nini ili Malawi waache dharau?

Swali zuri hapo ndipo masuala ya geo politiki na usalama. Tanzania inasaidia Mozambique itulie huku Malawi inatumia utulivu huo kufika bandari za Nacala na Beira.

Swali kuu je Tanzania ijiondoe huko Mozambique ili Malawi isipate nafasi ya kutumia miundo-mbinu ya barabara na reli ya Mozambique au la

Malawi imepewa eneo bandari ya Nacala hivyo siyo tena nchi isiyo na bandari ni partially landlocked, kuondokana na 'ubeberu' wa miaka mingi wa Tanzania iliyokataa kutoa gati likawa ni eneo la nchi ya Malawi katika bandari ya Dar es Salaam ikawapa bandari yote kwa DP World nchi ya mbali isiyo jirani:

Mradi wa Ukanda wa Barabara ya Nacala - Awamu ya I (Mkopo kwa Msumbiji) kukamilika December 2027​

Matunda ya mradi yaanza kuiva, bandari ya Nacala yapata mteja wa kuaminika

View: https://m.youtube.com/watch?v=ZTgeuT_T6s0

Mradi wa Ushoroba wa Nacala corridor kujinasua na utegemezi wa bandari ya Dar es Salaam​

Uendelezaji na uboreshaji wa Ukanda wa Barabara ya Nacala upo ndani ya miradi ya kipaumbele ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ambayo umejumuishwa katika programu ya NEPAD-STAP unaotazamiwa kukamilika kabisa December 2027.

Inajumuisha jumla ya kilomita 1033 za ujenzi wa barabara na vituo viwili vya Huduma chini ya paa moja ( One Stop Centre) vya mpakani, kimoja kati ya Msumbiji na Malawi na kingine kati ya Malawi na Zambia. Mradi huo unatekelezwa katika Awamu tatu.

La kwanza, somo la usaidizi huu linajumuisha 361km au 35% ya kazi za barabara nchini Msumbiji na Malawi. Itaangazia ukarabati wa barabara ya Cuamba-Muita kaskazini mwa nchi.

Awamu ya Pili inajumuisha 360km au 34.9% ya kazi za barabara nchini Zambia na Awamu ya Tatu ya kilomita 312 au 30.1% ya kazi za barabara nchini Msumbiji na Malawi na vituo viwili vya kituo kimoja cha mpaka kati ya Msumbiji na Malawi na Malawi na Zambia.

Awamu zote hizi ni pamoja na mapitio ya muundo, huduma za awali za mikataba na usimamizi wa kazi za kiraia, usalama barabarani, uzuiaji na uhamasishaji wa vita dhidi ya VVU/UKIMWI, fidia na makazi mapya na ukaguzi.

Malengo ya Mradi Ushoroba wa Nacala corridor​

Madhumuni ni (i) kuzipatia Malawi, Zambia na utumizi wa miundo-mbinu ya ndani ya Msumbiji itakayo wezesha mtandao wa usafiri wa barabara kuunganishwa kwenye bandari ya Nacala na kuboresha huduma za usafiri kwa kupunguza gharama za usafiri na ucheleweshaji katika vivuko vya mpaka (ii) kuboresha uendelevu wa uwekezaji kwa kudhibiti mizigo (iii) kuboresha ufikiaji wa jamii uliopo katika ukanda huo, kusaidia uchipuaji wa masoko mapya na huduma za kijamii na kuchangia katika kupunguza umaskini kwa ujumla.
 
Waziri wa kilimo Hussein Bashe kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X.
====

Salaam Ndugu zangu

Watanzania,Serikali imepokea taarifa kuwa Serikali ya Malawi imezuia kuingia kwa mazao ya kilimo kutoka Tanzania, yakiwemo unga, mchele, tangawizi, ndizi, na mahindi. Hatua hii imeathiri moja kwa moja shughuli za wafanyabiashara wetu wanaosafirisha bidhaa hizo kwenda Malawi.

Ni vyema ifahamike kuwa kwa kipindi cha miaka mitano, Serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kufungua soko la ndizi nchini Afrika Kusini bila mafanikio. Hali hii inafanana na changamoto tulizopitia kwa zaidi ya miaka kumi katika kufungua soko la parachichi, hadi pale tulipoamua kuchukua hatua za kulinda maslahi ya nchi yetu.

Kutokana na hali hii, na baada ya juhudi zote za kidiplomasia kufanyika bila mafanikio, ninapenda kuwataarifu yafuatayo:

1.Iwapo Serikali ya Malawi na Afrika Kusini hazitabadilisha msimamo wao kufikia Jumatano ijayo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo itazuia uingizwaji wa mazao na bidhaa zote za kilimo kutoka nchi hizo mbili.

2.Mizigo ya bidhaa za kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini haitaruhusiwa kupita ndani ya mipaka ya Tanzania, kuelekea bandari ya Dar es Salaam au nchi nyingine yoyote, hadi zuio hilo litakapoondolewa.

3.Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, ikiwa ni sehemu ya hatua za kulinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara wa Kitanzania.

Wafanyabiashara wote wenye mizigo ya kuelekea Malawi wanashauriwa kuacha mara moja kupakia bidhaa hizo, hadi hapo taarifa rasmi itakapotolewa kulingana na msimamo wa nchi husika.

Ninathibitisha kuwa kama Waziri mwenye dhamana, nimewasiliana kwa njia mbalimbali na Waziri wa Kilimo wa Malawi bila mafanikio ya kupata majibu rasmi.

Hatua hizi ni za kulinda heshima ya nchi yetu, uchumi wa wakulima wetu, na usawa katika biashara za kikanda
View attachment 3308278
Yeye ni waziri WA kilimo, mambo ya nchi zingine ni wizara ya mambo ya nje. Je amewasilisha , suala hilo, na pia kujadiliana na Waziri wa Fedha juu ya kumzuia bidhaa za Malawi kupita hapa .
 
Back
Top Bottom