Nesto E Monduli
JF-Expert Member
- Jun 6, 2016
- 247
- 155
Ha ha ha haaa..Labda Kuna Sheria ya OmbaOmba....!!Watawafunga jela kwa kutumia sheria gani?
Ha ha ha haaa..Labda Kuna Sheria ya OmbaOmba....!!Watawafunga jela kwa kutumia sheria gani?
Hahahaha, we jamaa umenifurahisha sanaNa tanzania nayo itolewe duniani ipelekwe huko mbinguni nauli iko USA maana nayo imezidi kuombaomba.
Kuna namna ya kudeal na hili suala kuliko kuwapa nauli, Mh Makonda ulishawahi kukaa nao wakakwambia tatizo nauli?? Je na ombaomba ambao wanatoka dar es salaam, Je wakisharudi mikoani ndio tutakuwa tumemaliza tatizo??
Issues ya omba omba sijaona tatizo maana ata nchi inaomba, kwangu issue ni kuwatumia watoto kuomba omba wakati walitakiwa kwenda shule
Amesema anawaondoa "OMBA OMBA" na sio "WALEMAVU" uwemwelewa pia unapotokwa na povu. Pia walemavu wanavituo vyao vya kuwalelea so hajakosea pia, kingine ulemavu sio ugonjwa wengi tu wapo wanafanya kazi na kijiingizia kipato.Nafikiri ni bora wakawauwa tu kama ishara ya kutokubarika kwao katika jamii ya kitanzania.Kubaguana kutokana na kasoro zetu kimaumbile ni jambo la hatari na lisilovumilika,mlemavu hakuchagua awe hivyo alivyo,ni matokeo ya majanga ya kidunia na maumbile,sasa wanapoanza kuwatenga na kuwafukuza mjini wanataka waowaishi wapi?
Ni mkoa gani uliotengwa na serikali uwe mkoa maalumu wa walemavu?Katiba yetu inatoa haki ya mtu kuishi popote ili mladi asivunje sheria,ni sheria gani sasa inayotumiwa na serikali ya mwendokasi unaokadiliwa kuwa na kasi ya division 4.30km/saa ya ccm inayotumiwa kuwabagua Watanzania kwa vigezo vya utimilifu wa viungo?
Mlianza kuwabagua washindani wenu kisiasa na kuwafanya waonekane Kama watu wa daraja la Mwisho nchini kwa kuwanyima haki za kusikilizwa,kukusanyika na kutoa mawazo yao,sasa mmehamia kwa walemavu.Baba wa Taifa aliwahi kuonya kuwa dhambi ya ubaguzi haiishi,ni sawa na kula nyama za watu,sasa naona mmenogewa na "nyama" za wapinzani wenu kisiasa,sasa mnatamani na nyama za walemavu,tukiuita utawala huu ni utawala wa "Giza" mnakimbilia kuzingira makazi yetu kama si ufedhuri ni nini?
Kama ulemavu umekuwa kero,waundieni mkoa wao ili waishi kwa amani kuliko kuendelea kunyanyaswa ndani ya nchi yao wenyewe.Mnaojinasibu na kujiapiza kufa kwa kuwaletea Maendeleo masikini wa Taifa hili,hao masikini mnaowatafutia maendeleo ni wakina nani?
Acheni unyanyasaji na ubakaji wa haki za msingi za kiraia,wewe unayejiona mzima leo ni mlemavu mtarajiwa,kesho ukipata ulemavu nasi tukufurushe katika uongozi wako na tukufungashe na kukurudisha kijijini kwenu Sitimbi?Acheni viburi vya uzima hii ni nchi yetu sote.
Kauli za kienyeji zisizo na chembe ya ucha Mungu ni kauli hatarishi na za kichochezi kuliko uchochezi wenyewe,kuendelea kuzinyamanzia kauli za kuwashusha matajiri waishi kama mashetani,kuwaita wananchi villaza,kuwaambia watu wapige mbizi na nyingine nyingi,si kauli za kiungwana na hazileti picha nzuri.Tunaomba viongozi wetu wachague kwa makini maneno ya kuyaongea badala ya kuongea kimizuka.Ulimi ni kiungo kidogo sana lakini matatizo yake ni makubwa,ulimi wa kiongozi wetu unaweza kuwa chanzo cha maangamizi ya Taifa kama hatakuwa makini katika uchaguzi wa maneno yake kabla ya kuyatamka.
Kwahiyo hawastahili kuishi Darwengi wametoka mkoani
Amesema anawaondoa "OMBA OMBA" na sio "WALEMAVU" uwemwelewa pia unapotokwa na povu. Pia walemavu wanavituo vyao vya kuwalelea so hajakosea pia, kingine ulemavu sio ugonjwa wengi tu wapo wanafanya kazi na kijiingizia kipato.
So acha umureree.
watoto kutoka mkoani kuja kuomba omba ndio hairuhusiwiKwahiyo hawastahili kuishi Dar