mwita ke mwita
JF-Expert Member
- Aug 13, 2010
- 7,918
- 3,613
MAKAMBA ANAPENDA AWE WAZIRI WA MAMBO YA NJE SIO HII MAZINGIRA
Wanalipia gesi kiongozi, sema gharama ni ndogo mno. Kama 150 rubles kwa mwezi. Kwa wenzetu gesi, maji na umeme ni vitu vinavyopatikana almost bure.Urusi wananchi wanagawiwa gesi bure majumbani, sisi ya kwetu wala hatujui anakula nani! Wale mamalishe wa feri walikomea kupata ahadi gesi ikagoma.
Labda wa Kilindi!MAKAMBA ANAPENDA AWE WAZIRI WA MAMBO YA NJE SIO HII MAZINGIRA
Kuhusu namba moja, una maana gani kuwa miradi yote iliyowahi kufanywa ilifeli. Imetolewa mifano hai hapa kuwa akiwa mkuu wa mikoa ya Morogoro na Dar Mh Yusufu Makamba alihamasisha na kuwezesha upandaji wa miti zaidi ya 100,000 kwenye hiyo miji. Hadi nusu ya miti hiyo ilipona na kukua na hadi leo mingi ipo, inaonakena ukitembelea hiyo miji.
Kuhusu mengine yote unataka kusema kuwa upandaji miti hauna faida?!!! Kwamba kwa sababu sayansi haijafikia muafaka juu uhusiano wa miti na mvua basi hakuna faida kupanda miti.
Unataka kusema "tusubiri" hadi siku sayansi ikithibitisha huo uhusiano ndio tupande miti?!!!
Unataka kusema hakuna haja miti kupandwa maana miti inajiotea yenyewe, kwa hiyo sisi tusubiri ijiotee tukakate kuni, tukachome mkaa, tukapasue mbao tu huko porini?!!!
Unataka kusema misitu kama ya Saohil, KDC na mingine mingi humu nchini inayotoa mbao tunazojengea nyumba na thamani "haikuwa na maana kupandwa" maana ecologically ingejiotea yenyewe?!!!
Unataka kusema nini?!
elaborate pls, thanks
Mkuu Zungu Pule tunakuomba utoe michango yako bila kuhamaki wala kimashambulizi.
Mkuu Tuko kaleta hii mada kwa nia njema na lengo ni kuchochea jitihada za utunzaji mazingira na wakati huo huo kuiamsha serikali juu ya usimamizi wa sera zake.
Ulitakiwa uoneshe uweledi wako postively ila sio kwa namna uliyokuja nayo ya kubeza pasipo uchambuzi wa nini kifanyike ilhali unaonekana unao ufahamu mkubwa kwenye masuala haya.
Toa mchango wako mkuu...
Huwa inaniuma sana maana nasafiri mara kwa mara nashuhudia mapori yanavyopukutika. Ukiangalia barabara ya dar to Arusha ndio utaelewa na viongozi wako kimya tu. Magari ya serikali ndio utakuta yamebeba magunia ya mkaa na kuni, nchi hii bwana. Waziri yupo busy kuvunja nyumba za watu badala ya kuhangaika na climate changeTanzania ndio nchi pekee duniani ambako mtu anaamka asubuhi na mtaji wa baskeli na panga anaingia msituni anakata miti na kuchoma mkaa anarudi jioni na kuuza kujipatia mlo wake wa siku bila kupanda mti mwingine au kuulizwa kwa nini unaharibu maliasili ya watanzania wote. Huwezi kuachia maliasili ikateketezwa hovyo namna hii wakati wazungu walituletea miradi ya participatory forest management ikatupwa mara baada ya wazungu kuondoka na serikali kulala. Acha tuwe jangwa
Tatizo
1. Tafiti zinaonyesha kati ya 55-65% ya archi ya Tanzania ipo hatarini kuwa jangwa miaka 20-30 ijayo. Ni tatizo ambalo lipo pia nchi nyingine za Africa
2. Namna pekee ya kunusuru mazingira kwa faida ya kizazi hiki na kijacho ni kwa kupanda miti
3. "Mahubiri" ya upandaji miti yamekuwa kama nyimbo zisizo na wasikilizaji wala wachezaji. Utekelezaji umekuwa sifuri.
4. Mwezi April mwaka 1999 raisi Mkapa alizindua programu ya upandaji miti iliyplenga kuandwa kwa miti milioni 10. Hata hivyo lengo la milioni kumi halikufikiwa hata kwa 20% na hata ile iliyopandwa zaidi ya 80% inasemekana ilijifia kwa kukosa matunzo. It was a failure to say so...
5. Tokea wakati huo hakujawa na plan zozote za maana za upandaji miti na hali ya mazingira inazidi kuwa mbaya
Suluhisho
1. Kwanza nisikitike kusema tangu apewe nafasi hiyo miezi takribani 6 iliyopita sijawahi kumuona waziri anayeshughulika na mazingira hata akipanda mche mmoja wa mti. Hii ni ishara mbaya juu ya uwepo wa azma yeyote ya serikali kuokoa mazingira
2. Kwa hiyo namshauri wazi mhusika Bwana J. Makamba "aamke" aanzishe program ya "kufa na kupona" ya upandaji miti. Natambua wizara yake inajishughulisha na masuala mengi ya mazingira lakini naomba suala la upandaji miti lipewe uzito wa kipekee
Ushauri
Najua zipo namna nyingi za kufanya program endelevu za upandaji miti. Naomba nipendekeze hii moja.
Shule zote za msingi na sekondari nchini zitakiwe kuwa sehemu ya program. Kila shule, chini ya usimamizi na ushauri na msaada wa halmashauri ianzishe kitalu cha miche ya miti shuleni. Waziri husika (makamba) awe ndiye mwezeshaji na mhamasishaji mkuu kwa kuandika hiyo program, kuigawa kwenye halmashauri zote na kutembelea kila halmashauri kuhakikisha program inatekelezeka.
Plan iwe kila shule ipande miche angalau 10,000 kwa mwaka na kila mwanafunzi ahusike moja kwa moja na upandaji na utunzaji wa angalau miche 100 kwa mwaka. Miche inayopandwa mashuleni igawiwe kwa wananchi wanaozinguka shule na hasa wazazi wa wanafunzi, na kuwe na uhamasishaji na usimamizi wa miti hiyo kupandwa na kutunzwa
Faida
1. Program ya kuhusisha shule itasaidia kutoa mafunzo na hamasa juu ya upandaji na utunzaji miti
2. Tanzania kuna jumla ya shule ziadi ya elfu kumi za msingi na sekondari (za serikali). Kama program hii ikifanikiwa kwa angalau 50% ya shule, ina maana miche 50,000,000 itapandwa kwa mwaka. Hii ina maana kama miche hiyo ikipona kwa ngalau 50% miche 25,000,000 itapandwa kwa mwaka, na kama hiyo ikifanikiwa kutunzwa na kukuzwa, ina maana miti milioni 12.5 itapandwa kwa mwaka.
3. Program hii ikifanyika kwa miaka 10 ina maana miti zaidi ya milioni 125 itakuwa imependwa.
Sustainability
1. Najua "kikwaz0" cha kwanza mtu atasema program ya namna hii inahitaji fedha nyingi na hazipo kwa sasa. Lakini hebu tujiulize fedha kiasi gani zitahitajika kuanzia hatua ipi ya mradi. Kwa mfano Programu itahusisha hatua zifuatazo
i. Kuandika program
ii. Kusambazwa program kwenye mashule
ii. Kuandikisha shule zinashoshiriki
iv. Shule kutenda eneo la kitalu
v. Kulimwa na kutengenezwa vitalu
Hadi hapa naweza kusoma ni 0 cost.
Kwa maana hiyo utaweza kuona kinachohitajika ni azma, nia, na uwajibikaji tu. Gharama ndogo ndogo kama stationeries na gahrama za mawasiliano na ufuatiliaji ni gharama za kawaida za ofiri wala hazihitaji bajeti maalumu.
Gharama za vifaa kama vifuko vya kupandia mbegu nina uhakika shule zinaweza kujipanga na zikapata hivyo vifaa ambavyo havizidi Tsh 20,000 wa shule moja.
Wanafunzi wanahamasishwa kuleta mbegu za miti mbalimbali kutoka kwenye mazingira yao na pale zitakapohitajika mbegu za kununua halmashauri zinaweza kusaidia kupitia ofisi za misitu na wakala wa miti wa taifa...
Nawasilisha
Tanzania ndio nchi pekee duniani ambako mtu anaamka asubuhi na mtaji wa baskeli na panga anaingia msituni anakata miti na kuchoma mkaa anarudi jioni na kuuza kujipatia mlo wake wa siku bila kupanda mti mwingine au kuulizwa kwa nini unaharibu maliasili ya watanzania wote. Huwezi kuachia maliasili ikateketezwa hovyo namna hii wakati wazungu walituletea miradi ya participatory forest management ikatupwa mara baada ya wazungu kuondoka na serikali kulala. Acha tuwe jangwa
Huwa inaniuma sana maana nasafiri mara kwa mara nashuhudia mapori yanavyopukutika. Ukiangalia barabara ya dar to Arusha ndio utaelewa na viongozi wako kimya tu. Magari ya serikali ndio utakuta yamebeba magunia ya mkaa na kuni, nchi hii bwana. Waziri yupo busy kuvunja nyumba za watu badala ya kuhangaika na climate change
Hebu wape a,b,c,d namna ya kudhibitiWaziri wa mazingira wa sasa aamke lakini pia uwepo mkakati wa wizara za mazingira na nishati kumaliza kabisa biashara kichaa ya mkaa.