Makamba amka! Nusu ya nchi inaelekea kuwa jangwa

Serikali yetu ni mafundi wazuri wa kutunga sera lakini nyingi wazo huishia kwenye makaratasi tu na pesa za mipango zinatafunwa!
Kila uchao ni kubadilisha mawaziri tu na kila anaeingia ana implement sera zake ili avune pesa.
Hakuna mpango mkakati wa kudhibiti wafugaji.
Makamba yupo busy na kufukunyua masrahi ya wafanyabiashara wa vifungashio vya plastic na nylon make huko ndo kwenye ulaji...
Akipewa gawiwo lake, ataextend muda wa ukomo wa matumizi/uzalishaji wa vifungashio vya nylon na plastic.
Baada ya mwaka/miezi tutaletewa waziri mpya naye atatafuta chocho la kutafunia ilmradi afaidi mema ya Nchi!
 
Ni wazo zuri ila ingefaa pia ukajikita zaidi kwenye changamoto.
Kuna baadhi ya wilaya hapa Nchini wamenufaika sana na faida za upandaji miti.
Wilaya kama Sengerema, Mafinga, Njombe na Makete wamehamasika sana na upandaji wa miti na ndo imekuwa kama shughuri yao rasmi inayopa uhakika wa kuboresha maisha yao. Wengi wametajirika kupitia upandaji na uvunaji miti.
Kanda zote hizo hakuna muingiliano wa wafugaji waharibifu tofauti kabisa na mikoa mingine kama Morogoro ambapo wananchi wanashindwa kuhamasika na upandaji wa miti kutokana na ufugaji holela wa mifugo ambao kwa kiasi kikubwa umechangia sana kufifisha jitihada hizi.
Ni gharama kubwa sana kumudu utunzaji wa shamba la miti kwa mikoa iliyozagaa wafugaji holela hasa jamii za kimaasai na baribaig.
Kwa kipindi cha miaka3 niliyoishi Morogoro, nimeshuhudia uharibifu mkubwa sana wa mazingira na mashamba ya miti unaosababishwa na hawa wafugaji.
Wakulaumiwa ni Serikali kwa kukosa program endelevu kunusuru misitu na ufugaji holela.
Ni kweli mkuu kuna tatizo kubwa sana la mifugo kuharibu mazingira ambalo linapaswa kushughulikiwa...

Wakati hilo likifanyika tunaweza kuanza na yale maeneo yasiyo na hayo matatizo, mathalani kuzunguka nyumba zetu.

Umetolea mfano wa Morogoro na kwa bahati nzuri mimi naishi Moro mjini. Nilipewa nyumba ya serikali kuishi mwaka 2008 na niseme hapo nyumbani palikuwa kama "kajangwa"...

Nikaanza tu kama utani kuvuna na kupanda mbegu za 'mikenge' (mijohoro), na miarobani. Majirani walinishangaa na kunicheka lakini leo ukija penye hiyo nyumba pako kama paradiso...lol.

Sikujali kwamba sio nyumba yangu na baadae nikafanikiwa kununua vikiwanja, moto ukawa ni ule ule kupanda mijohoro na miarobani.

Kufikia mwaka 2012 nilikuwa nimepanda zaidi ya miti 200 ukiacha uliyokufa kwenye maeneo ya makazi hapo Moro.

Kwa hiyo wakati tukipambana na changamoto eneo moja tunaweza kuendelea na utekelezaji eneo jingine...
 
Nakumbuka nilipokuwa std six (1996) shule yetu ilipewa kibarua cha upandaji miti kwenye msitu wa serikali.
Wanafunzi tulipanda zaidi ya ekari 300 kwenye ule mradi.
Baadhi tulikuwa tunarudi majumbani na miche kadhaa kwajili ya kupanda makwetu!
Mpaka ukomo wa kibarua kile nilifanikiwa kupanda miche karibu300 kuzunguka shamba letu. Niliendelea na shule hadi chuo nikamaliza. Wakati huo nishasahau kabisa kama nilipanda miti huko nyumbani enzi nikiwa mdogo!
Baada ya chuo kwenye mchakamchaka wa kusaka ajira, maisha yalikuwa tight sana ndo kumpigia simu Mama walau aniwezeshe kidogo mambo ya mlo! Nikashangaa baada ya siku4 Mama ananiambia nichungulie a/c yangu... nikakuta kadepost 1000000/= kumuuliza ndo akanambia kapasulisha mbao ile miti yangu ya syprus na kupata zaidi ya milioni3!!!
Dah nilisitaajabu sana na ndo ikawa mwanzo wa upandaji miti!
Mpaka hivi sasa nina ekari nyingi sana za syprus na teak. Hii ni hazina yangu ya baadae!!
Vijana pandeni miti...
 
Kwanza serikali ingetafuta chanzo mbadala wa kuni na mkaaa
Gesi ilitakiwa iuzee bei ndogo ili mkaa ukose thamani na watu wahamie kwenye gesi
Hapo miti itasalimika tofauti na hapo tutakuwa twapigia mbuzi gitaa
Serikali isiyo na mikakati gesi inazidi kukwea juu,tunachoangalia Kwa sasa ni kodi tu hayo mengine haryana umuhimu
 
Wazo mjarabu ila maeneo ya upandaji ya hivyo vitalu vitapatikana vijijini tuu mijini nina shaka
 
Point ni upandaji miti tuu coz huwezi kuzuia uchomaji wa mkaa na kilimo ni vitu vinavyogusa maisha ya kila cku ya watu
 
Nakumbuka nilipokuwa std six (1996) shule yetu ilipewa kibarua cha upandaji miti kwenye msitu wa serikali.
Wanafunzi tulipanda zaidi ya ekari 300 kwenye ule mradi.
Baadhi tulikuwa tunarudi majumbani na miche kadhaa kwajili ya kupanda makwetu!
Mpaka ukomo wa kibarua kile nilifanikiwa kupanda miche karibu300 kuzunguka shamba letu. Niliendelea na shule hadi chuo nikamaliza. Wakati huo nishasahau kabisa kama nilipanda miti huko nyumbani enzi nikiwa mdogo!
Baada ya chuo kwenye mchakamchaka wa kusaka ajira, maisha yalikuwa tight sana ndo kumpigia simu Mama walau aniwezeshe kidogo mambo ya mlo! Nikashangaa baada ya siku4 Mama ananiambia nichungulie a/c yangu... nikakuta kadepost 1000000/= kumuuliza ndo akanambia kapasulisha mbao ile miti yangu ya syprus na kupata zaidi ya milioni3!!!
Dah nilisitaajabu sana na ndo ikawa mwanzo wa upandaji miti!
Mpaka hivi sasa nina ekari nyingi sana za syprus na teak. Hii ni hazina yangu ya baadae!!
Vijana pandeni miti...
Nimeipenda hii,sana.
Hongera mkuu.
 
waziri wa mzingira hajui wala hajawahi hata kuwa na passion ya mazingira..
kuna vijana wazuri wa env. engineering na env. management wanazalishwa SUA na ARDHI UNVERSITY wanaweza toa elimu nzur ya utunzaji mazingira na kujiepusha na magonjwa kama kipindu pindu kila wilaya na kata hapa Tanzania lakini waziri na rais wake wamelala tuu haya ndo majipu ya kutumbua
 
Mkuu kwa wapenda mazingira kama sisi,tumefarijika sana na makala yako

Ni ukweli ulio wazi,serikali ikiamua,hakuna gharama yoyote kubwa kwenye utekelezaji wa mpango huo wa upandaji miti.

Kama mtakumbuka Mzee makamba alipokuwa mkuu wa mkoa wa Dar,alilazimisha kila mtu apande miti nyumbani kwake,watu tunaopenda mazingira tuliitikia wito tukapanda miti,hata kama zoezi halikufanikiwa sana kutokana na viongozi wengi hutoa matamko kisiasa zaidi,lakini Leo hii Dar ina uafadhali wa miti na kupendezesha mji tofauti na miaka ya nyuma.

Katika kutekeleza zoezi hilo la upandaji miti,Serikali inaweza kuwatumia wafungwa wenye makosa mepesi ambao wapo mikoa yote.Pia kuna majeshi kama JKT,migambo hawa wakitumika vizuri zoezi lisingekuwa na gharama.

Na katika kufanya watu wote washiriki kwenye kampeni hiyo,inatakiwa viongozi wa dini washirikishwe kwa wao kuhamasisha waumini,mfano mzuri ni kanisa la KKT Kilimanjaro, askofu wao ametoa agizo,kila mtoto anayepokea kipaimara ni lazima apande miti 20,ambapo serikali haijahusika hata chembe.

Na sisi wenye uchungu na jambo hilo tuhamasike kuwa mfano kwa kupanda miti mahali tulipo.Mimi kwangu nilitengeneza bustani ya miti,ambapo hadi leo majirani zangu wanatumia kufanya vikao mbalimbali,hivyo tusiishie kuiambia serikali peke yake,bali tuonyeshe mfano.Ahsante naomba kuwasilisha!
Mkuu nafikiri ulipanda miti ya kivuli na matunda!! Jamaa wakifanya mkutano wanachuma na matunda wanakula ili kuijenga miili yao!!
 
Sasa hata akiamka atafanyaje Mkuu wakati gesi yenyewe wamepandisha kodi, lazima miti iendelee kufyekwa tu kuni zipatikane Mkuu
 
Nimeipenda hii,sana.
Hongera mkuu.
Yeah really interesting!
Nakuomba sana mkuu kama una mwanao mrithishe tabia na mambo kama haya. Yatamfaa sana baadae..
Siku napokea ile hela kiukweli roho iliuma sana ndo ikabaki ningejua ningepanda hata ka ekari kamoja!!
Dah, ntangia hapo sikurudi nyuma tena na wazo la kuajiriwa taratiibu lilianza kufifia!
Baadae niliajiriwa ila sikudumu sana huko nikaamua kukomaa kivyangu na focus kubwa ilikuwa ni kupanda miti na shughuri nyingine za kiuzalishaji. Haikua jambo dogo kuchukua maamuzi haya, ila baada ya miaka3 mbele i tell you ntaanza kunufaika hatari hatari..!!!
 
Mkuu umanikumbusha ile mikakati ya JK... itabidi nijaribu kufuatilia machapisho kama ilitekelezwa na ilishindwa wapi...

Kwa kweli suala la upandaji miti inabidi lipewe muamko mpya na nguvu ya kipekee...
Mkuu niliipenda sana ile mikakati lakini kwa bahati mbaya iliishia kwa hotuba nzuuuri ya JK na kisha hotuba nzuuuri ya Makamo wa Rais. Nilichokiona mwanzoni ni mkaa kuuzwa kama nyara ya serikali. Ukipita huko njiani/barabarani ulikuwa ukikuta kipande cha mkaa kimetundikwa kwenye mti, basi unajua eneo hilo panauzwa mkaa u asimama na wanakuja wanakuangalia wanakupeleka kichakani u achukua gunia lako unasonga mbele. Ikaenda hivyo ila baada ya mwaka ikaishilia mbali. Biashara ya mkaa ikarudi kama kawaida hadi sasa. Sikuona uhamasishaji wa kupanda miti. Afadhali hata Dr. Omar Juma alikuwa akihamasisha kupanda iti lakini Dr. Shein na Dr. Bilal sikuona juhudi hizo.

Kwa kuwa sasa tuna suala la usafi wa mazingira ambalo linasisitizwa basi liendane na uhamasishaji wa upandaji miti kila kona ya nchi. Bei ya gesi ishuke, majiko ya gesi yawe bei rahisi ili iwe ni ghali kutumia mkaa na umeme (japo kuna waswahili utawasikia wanasema wali uliopikwa kwa mkaa ni mujarab kuliko wali uliopikwa kwenye gesi ama umeme!!).
Makamba aje na mikakati ya kutunza mazingira ya nchi hii.
 
Sasa hata akiamka atafanyaje Mkuu wakati gesi yenyewe wamepandisha kodi, lazima miti iendelee kufyekwa tu kuni zipatikane Mkuu
Mkuu hapo ndipo penye tatizo. Huenda Makamba hakuwepo kwenye kikao cha Baraza la Mawziri wakati wanapendekeza tozo kwenye gesi. Kwa kuwa kama waziri wa mazingira, yeye angetetea badala ya kupandisha gharama za gesi wangeshusha gharama hizo na hata kuweka ruzuku ama kutoa kodi kabisa kwenye majiko ya gesi. Hii ingemsaidia sana katika Wizara yake.
 
Mkuu kwa wapenda mazingira kama sisi,tumefarijika sana na makala yako

Ni ukweli ulio wazi,serikali ikiamua,hakuna gharama yoyote kubwa kwenye utekelezaji wa mpango huo wa upandaji miti.

Kama mtakumbuka Mzee makamba alipokuwa mkuu wa mkoa wa Dar,alilazimisha kila mtu apande miti nyumbani kwake,watu tunaopenda mazingira tuliitikia wito tukapanda miti,hata kama zoezi halikufanikiwa sana kutokana na viongozi wengi hutoa matamko kisiasa zaidi,lakini Leo hii Dar ina uafadhali wa miti na kupendezesha mji tofauti na miaka ya nyuma.

Katika kutekeleza zoezi hilo la upandaji miti,Serikali inaweza kuwatumia wafungwa wenye makosa mepesi ambao wapo mikoa yote.Pia kuna majeshi kama JKT,migambo hawa wakitumika vizuri zoezi lisingekuwa na gharama.

Na katika kufanya watu wote washiriki kwenye kampeni hiyo,inatakiwa viongozi wa dini washirikishwe kwa wao kuhamasisha waumini,mfano mzuri ni kanisa la KKT Kilimanjaro, askofu wao ametoa agizo,kila mtoto anayepokea kipaimara ni lazima apande miti 20,ambapo serikali haijahusika hata chembe.

Na sisi wenye uchungu na jambo hilo tuhamasike kuwa mfano kwa kupanda miti mahali tulipo.Mimi kwangu nilitengeneza bustani ya miti,ambapo hadi leo majirani zangu wanatumia kufanya vikao mbalimbali,hivyo tusiishie kuiambia serikali peke yake,bali tuonyeshe mfano.Ahsante naomba kuwasilisha!
Mkuu umenikumbusha mzee Makamba

Niliwahi kumsikia mzee mmoja Morogoro akisema Makamba "akiwatesa" sana kupanda mijohoro na miarubaini kipindi akiwa mkuu wa mkoa pale.
Ila leo ndio wanaona matunda ya uhamasishaji ule maana kiukweli mji, hasa maeneo yaliyokaliwa zamani kidogo yana miti sana...
 
Urusi wananchi wanagawiwa gesi bure majumbani, sisi ya kwetu wala hatujui anakula nani! Wale mamalishe wa feri walikomea kupata ahadi gesi ikagoma.
 
Back
Top Bottom