ITEGAMATWI
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 5,338
- 4,083
Nilikuwa naongelea hoja ya kujua lugha ya kabila kwa mtoto kabla ya kujua kiswahiliau kiingereza naona umekwepa hilo umerukia kwenye majina ya watoto kitu ambacho sikukipinga ndiyo maana nikasema kuna mazuri yake kwenye hilo japo mabaya ni mengi kuliko mazuri.Kwahivyo Baba akiwa Mhaya na Mama Mluguru, ndio inahalalisha watoto wao kuitwa James Michael David na Ann Michael David? Umesikia lini hao ngozi nyeupe mnaowaiga wakiitwa majina kama Mungai, Kunle au hata Kaguta? Aliyekuambia Kenya watu wa makabila tofauti huwa hawaoani ni nani?
Nchini Kenya kuna makabila ambayo yana muingiliano mkubwa sana, tena tangia jadi kabla ya ukoloni. Kwa mfano utapata watu wenye majina ya Kikikuyu ila lugha na tamaduni zao ni za kimaasai. Kuna hadi makabila ambayo yalimezwa kabisa na makabila mengine na yakapotea kabisa. Kwa mfano wakikuyu walimeza kabisa makabila mawili madogo yaliyoitwa Gumba na Athi.
Haya kwasababu umehamia kwenye suala la kuona makabila tofauti Kenya basi twende huko. Hivi unataka kusema kuwa kuoana makabila tofauti siyo jambo la nadra kenya? Kama wewe ni mtanzania hebu fikiria jamaa zako wa karibu ni wangapi wameoa au kuolewa na watu wa makabila yao? Yaani ni wa kumulika kwa tochi.