Marekebisho 1.5bilion
Hajui kuwa JF ndio expansion Joint yetu??JF ndio chakula na maji kwetu!Itafungwa kwa sababu zipi??funguka mkuu
Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua matengenezo ya makazi ya muda yanayotarajiwa kutumiwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan atakapohamia Dodoma.
Waziri mkuu amefanya ukaguzi huo leo Jumatano, Desemba 6, 2017 mchana katika eneo la Kilimani mjini Dodoma ambako yalikuwa makazi ya mkuu wa mkoa.
Akitoa taarifa ya ujenzi, Waziri wa Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Wenye Ulemavu na Vijana, Jenista Mhagama amesema kikosi kazi cha kuratibu kazi ya Serikali kuhamia Dodoma kilibaini mahali alipokuwa akiishi awali si sahihi kwa ajili ya makazi ya kudumu ya Makamu wa Rais.
“Pale palikuwa panafaa kwa ajili ya ziara za kikazi alipokuwa akija Dodoma, kwa hiyo tumeamua tufanye ukarabati hapa ili aweze kuishi kwa viwango vinavyostahili,” amesema katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Amesema kazi ya matengenezo itagharimu Sh1.5 bilioni wakati kazi ya kutenganisha ofisi za watumishi na wasaidizi wa Makamu wa Rais itagharimu Sh680 milioni.
Waziri mkuu pia amekagua matengenezo ya ofisi inayotarajiwa kutumiwa na Makamu wa Rais ambayo itakuwa eneo la Ndejengwa.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dodoma, Steven Simba anayesimamia ujenzi huo amesema wanataraji kazi itakamilika kabla ya Desemba 30, 2017.
Watanzania tunaonekana maboya na wenye PhD feki na bashite,na aslani walomchagua no punguaniMatengezo tu ambao sio ujenzi mpya ni 1.5 Bln, Ghorofa zile hostel Mpyaaaaaaaaa 10Bln? Haya Tutafanyaje sasa.
Ha ha ha aana expansion joints zenye hadhi ya makamu wa rais
Mwezi wa 7 2018 JF itafugwa viongozi wao mjipange!!
Hapo ina maana kama tungekuwa tunajenga hostels kama zile za Magu tungejenga hosteks 3 Hao inaonekana hawajengi ila wanarepair!!! Hata yale naghorofa ya Dr. Shika hayajafika gharama hizo. Labda watwambie wanachimba tunnel kuelekea Singida kwaajili ya dharura ya kujiokoaMatengezo tu ambao sio ujenzi mpya ni 1.5 Bln, Ghorofa zile hostel Mpyaaaaaaaaa 10Bln? Haya Tutafanyaje sasa.
Kaenda kuangalia. Kukagua kunataka utaalamu. Kama siyo mtaalamu hawezi kukagua.Sasa hapa ameenda kutembelea au kukagua, Kama kukagia anautalam Gan wa ukaguzi
Ili iweje?kati ya vitu vilivyompandisha hadhi magufuli na kuwazidi maraisi waliomtangulia ni kuipeleka serikali kati kati ya nchi yaani Dodoma.
Kazi hiyo si angefanya mhandisi wa mkoa tu. Au kwa sababu ni ya 1.5bn?
Mkiambiwa ccm ni ile ile mnasema ni mpya!!!