Maisha, Mapenzi na Utajiri wa Alikiba; Kuna mengi ya kujifunza

View attachment 650126
Naan kama ilivyo kwa wengine pia mimi ni mpenzi mkubwa sana wa BongoFlavor, Na leo nilikua nafatilia kwa kina kuhusu lifestyle ya mwanamuziki ALIKIBA ambae kwa kawaida ni ngumu kujua details zake kutokana na usiri wake, nilishawahi kuandika hapo nyuma kuhusiana na msanii DIAMOND PLATNUMZ maisha yake na mafanikio yake katika muziki, na leo nikashawishika kumfuatilia ALIKIBA na kusema ukweli kuna mengi ya kujifunza kupitia huyu bwana mdogo,

Melezo katika video


Alikiba pia ni moja ya wasanii wenye mkwanja mrefu kuliko boss wako (napendaga kusema hivyo) na mafanikio yake yalianza kuonekana kuanzia mwaka 2014 alipoamka rasmi na kurudi kwenye game kwa kishindo na ngoma yake ya "MWANA" hapo ndipo milango yake ya mafanikio ikaanza kufunguka na matuzo ya kila pembe ya dunia hii yakaanza kumsogelea, pia ni katika kipindi hichi alikiba alijizolea mamilioni ya mashabiki japo wengi wa mashabiki zake wamemfuata kutokana na chuki walizonazo kwa mpinzani wake, yani DIAMOND PLATNUMZ,

Mafanikio ya alikiba pia yaliongezewa nguvu na ile deal aliyopata ya kujiunga na label kubwa kabisa ya muziki duniani yani "SONY MUSIC" hakuna anaejua amechota kiasi gani katika deal hii lakini kwa hakika ni mpunga mrefu,

Maisha yake ya mapenzi wengi wanafahamu ana watoto wanne na inasemekana kila mtoto na mama yake

Sitaki kuweka maneno mengi lakini mwisho niseme tu inapendeza na kutia moyo kuona vijana wetu wanapata mafanikio makubwa kutokana na kazi zao inatia moyo sana ukilinganisha na kipindi cha nyuma, kwasasa mziki wa tanzania unazalisha mamilionea kila kukicha ni kitu kizuri sana





Tutajenga viwanda kwelii...
 
Kwaio ali kiba habari zake haziwezi kuandikwa bila kumhusisha Diamond nadhani alikiba atakua ni kishazi tegemezi...
wote ni wasanii wakubwa hivyo ukimuongelea Diamond lazima umtaje ali na ukimuongelea ali lazima umtaje diamond
 
Anautajiri gani? Wakati anakaa kijumba kibovu pale segerea chama! Tena cha kupanga! Peleka propaganda zako hapa!
Naskia anaishi na ndgu zke wote humo ndani wkti nyumba ni ndogo tu,sebule yke ni pale kwetu pazuri utamkuta kule lounge na wauza sura wke
 
Back
Top Bottom