Mahakamani: Aliyemchoma mkewe kwa magunia mawili ya mkaa anatajwa kuwa mlemavu wa akili

Temporal insanity au permanently insane?, ila hata hao madokta wa Milembe waliompima, akija mtu akawapima, na wao watakuwa na matatizo ya akili. Mazingira hum-shape mtu.

Haya, na yule padri aliyeua mwanae Albino kule kagera mahakama imesema akapimwe akili.

Though that is just an expert opinion, not binding to the court. The court will have an opportunity to make an evaluation of its own.

Kazi ya defence ni kutoboa ushahidi wa upande wa mashitaka, and in criminal cases, proof is beyond reasonable doubt.

Tatizo la insanity inapimwa kwa observation ya behaviors tu, hamna empirical test au biological test ya kupima akili kwa kuwa akili sio physical. So plotting inaweza kufanyika na deliberate planned recording inawezekana tu then conclusion ikafanyika then judge atachukua expert opinion na akamaliza. But km kuna mauaji lazima mtu atakaa Isanga muda wa kutosha tu hata kama atakuwa acquitted
 
Mahakama imfutie mashitaka aachiwe huru mara moja kwaajili ya matibabu
Sasa unataka Mahakama imrudishe mtu mwenye tatizo la afya ya mtaani, si atauwa na wengine huko kitaani kwao!? Bora ishi milembe for life! Maana once a kichaa,always a kichaa,ni swala la muda tu!!
 
Dan kweli marehemu hana haki na hana hatia pia
Huyo jamaa mke alikuwa ana mcheat....mke akawa na kiburi..
Jamaa ashajitoa sana kwa mke
Si unajuwa tena mke kawezeshwa
Na ikitokea jamaa akatoka ndugu wa mke wataliaaa 😄

Ova
 
Shida ya akili inatokea muda wowote kwenye maisha yako ,kwenye sheria inachoangaliwa wakati unatenda tendo ovu je ulikuwa na akili timamu?
Akili ya miaka iliyopita,inapimwaje mwaka huu!? Na unazitofautisha vp akili za mwaka jama na mwaka huu!!?
 
Akili ya miaka iliyopita,inapimwaje mwaka huu!? Na unazitofautisha vp akili za mwaka jama na mwaka huu!!?
generally ili mtu aweze kuwa na hatia lazima tujiridhishe kama kosa alifanya akiwa na akili timamu au la
Na vile vile hata kuhukumiwa hatuweI kumhukumu mtu ambaye akili yake haipo timamu, anatakiwa apeleke akatibiwe ,kwa sababu mtu aliyekuwa hayupo sawa kichwani hata kujitetea hawezi
 
Tuwe waangalifu sana tunaenda kuoana na nani. Ndoa nyingi zimekuwa sehemu ya kufanya mambo ambayo ni ya kikatili kupitiliza
 
Kumuhukumu mtu yeyote kwa makosa ambayo hujui chanzo,hali ya mtuhumiwa au kichocheo chake ni ubatili sana wa fikra.Tuombe yasitukute.

Kwahiyo mtu akifanya kosa kama mauaji asihukumiwe hadi mjue chanzo chake kwa lugha nyingine kuua ni sawa so long as chanzo ni halali?
 
Tupe hizo tofauti tuzijuwe wote pls!!
Chukulia kwa mfano wakati wa makaburu wa Afrika kusini kulikuwa na Sheria ya waafrika weusi kutokutembea mitaa ya wazungu. Ukishikwa unakamatwa na kushtakiwa. Hiyo siyo haki lakini sheria inasema usipite.
Hata Tanzania Kuna sheria nyingi zenye kunyima wananchi haki
 
RIPOTI kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili, Mirembe imeeleza kuwa mfanyabiashara Khamis Luwonga (38) anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa wakati anafanya tukio hilo la mauji alikuwa ana shida ya akili.

Taarifa hiyo, imetolewa leo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mwasiti Athuman mbele ya Jaji Hamidu Mwanga wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya usikilizwaji.

Wakili Athuman amedai kuwa katika kikao cha mwisho Mahakama ili ekelekeza mshtakiwa apelekwe kwenye Hospitali ya Afya ya akili kuangalia akili yake wakati anafanya tukio hilo alikuwa ana akili timamu au la.

Amedai ripoti ya kitababu ya hospitali hiyo ya Septemba 26, 2024 katika ukurasa wake watatu inaeleza kuwa baada ya mshtakiwa kufanyiwa uchunguzi wakitaalamu walioona anaugonjwa wa kifafa ambapo alipewa dawa.

Pia, amedai kuwa ilionekana mshtakiwa huyo wakati anafanya tukio hilo alikuwa ana shida ya akili, kutokana na ushahidi huo ni wa upande wa utetezi wapo tayari kuendelea na usikilizwaji na wana mashahidi wawili.

Katika kesi hiyo ya muaji namba nne ya mwaka 2019, mshitakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.

Nipashe
Ndo chimbo jipya la kujinasua kwenye kesi za mauaji.

Hivyo siyo ajabu.

Vyombo vya habari vililipoti hivi,,l

Aliandaa mashimo siku tofauti,

Akaandaa tanuru la kumchomea mke wake, Akaenda akatafuta magunia mawili ya mkaa akatanguliza gunia Moja la mkaa Kisha mwili wa mkewe Kisha gunia jingine, Kisha akamchoma, na baada ya siku chache Kubeba mabaki na kwenda kuyafukia shambani kwake na kupanda mgomba.

Haikutosha na alienda polis kuripoti mkewe kapotea.

HIVI HUO MLOLONGO WOTE HUO BADO TUAMINI ALIKUWA NA UGONJWA WA AKILI?
 
Mipango yoote matayarisho yoote yale, mpaka kuzika vipande kule shamba. Mmh sidhani akili iliruka labda huko gerezani ndiyo ilifyatuka.
Unadhani waliorukwa akili wote hawavai nguo? Hawakwepi magari barabarani? Hawajitafutii kipato?

Anyways, sitetei upande wowote. Najaribu kuwaza kumsauti tu, mkuu.
 
Ndo chimbo jipya la kujinasua kwenye kesi za mauaji.

Hivyo siyo ajabu.

Vyombo vya habari vililipoti hivi,,l

Aliandaa mashimo siku tofauti,

Akaandaa tanuru la kumchomea mke wake, Akaenda akatafuta magunia mawili ya mkaa akatanguliza gunia Moja la mkaa Kisha mwili wa mkewe Kisha gunia jingine, Kisha akamchoma, na baada ya siku chache Kubeba mabaki na kwenda kuyafukia shambani kwake na kupanda mgomba.

Haikutosha na alienda polis kuripoti mkewe kapotea.

HIVI HUO MLOLONGO WOTE HUO BADO TUAMINI ALIKUWA NA UGONJWA WA AKILI?
Duh
 
Tuwe waangalifu sana tunaenda kuoana na nani. Ndoa nyingi zimekuwa sehemu ya kufanya mambo ambayo ni ya kikatili kupitiliza
Wakati mwingine hata uangalifu hausaidii kwani watu hubadilika kitabia au huficha tabia. Sikupingi suala la uangalifu ila naweka tu angalizo. Na kuongezea: ukishaona kwenye ndoa vi-ugomvi haviishi ni bora mkaachana mapema. Kwa experince yangu, hivi vi-ugomvi vidogo vidogo vya kila siku vinapalilia jambo baya sana. Hasa ikiwa ni juu ya mwanamke kuwa na kiburi au kuchepuka.
 
Ajabu huu ugonjwa wa akili, unatambulika baada ya tukio la mauaji, kabla hakuna alietambua, na alikua anaendesha biashara yake vizuri tu.
Tule hela ila tuhurumie Dunia, wakati mwingine tuwe tayari kukosa, kwa ajiri ya amani ya kesho, dah inasikitisha sana.
Naskia aliemdhulumu nafsi mtoto, Asimwe nae anapimwa akili.
 
Uchochoro wa kutokea unaandaliwa yote kheri akalee watoto sasa
 
Back
Top Bottom