Yote yanawezekana kwa pamoja.La kufurahisha zaidi ni wale ambao jamii inawaona wanafeli kuisaidia nchi wakipandishwa vyeo na kuaminiwa zaidi na zaidi.Ripoti kama hizo kwa sasa nchini kwetu si za kuaminika kwa sababu ya rushwa ilivyotamalaki lakini pia wakati mwingine Wataalamu wetu kukosa weledi wa kutosha.
Zitafungwa ndoa chache mnoo!Sidhani kama vipimo vingeonesha mimi nipo timamu kichwani.😎Kabla ya ndoa tupimwe akili, ripoti za daktari zitumike kuweka pingamizi la ndoa iwapo mmoja dishi bovu......
Dan kweli marehemu hana haki na hana hatia piaRIPOTI kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili, Mirembe imeeleza kuwa mfanyabiashara Khamis Luwonga (38) anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa wakati anafanya tukio hilo la mauji alikuwa ana shida ya akili.
Taarifa hiyo, imetolewa leo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mwasiti Athuman mbele ya Jaji Hamidu Mwanga wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya usikilizwaji.
Wakili Athuman amedai kuwa katika kikao cha mwisho Mahakama ili ekelekeza mshtakiwa apelekwe kwenye Hospitali ya Afya ya akili kuangalia akili yake wakati anafanya tukio hilo alikuwa ana akili timamu au la.
Amedai ripoti ya kitababu ya hospitali hiyo ya Septemba 26, 2024 katika ukurasa wake watatu inaeleza kuwa baada ya mshtakiwa kufanyiwa uchunguzi wakitaalamu walioona anaugonjwa wa kifafa ambapo alipewa dawa.
Pia, amedai kuwa ilionekana mshtakiwa huyo wakati anafanya tukio hilo alikuwa ana shida ya akili, kutokana na ushahidi huo ni wa upande wa utetezi wapo tayari kuendelea na usikilizwaji na wana mashahidi wawili.
Katika kesi hiyo ya muaji namba nne ya mwaka 2019, mshitakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.
Nipashe
Lakini mkuu, Mirembe huwa pia inatumika kama backdoor kwa wahalifu wenye pesa kuepuka gereza, kuna wa kwetu tumehakikishiwa kuwa christmas haimkuti mirembe wala jela.Kumuhukumu mtu yeyote kwa makosa ambayo hujui chanzo,hali ya mtuhumiwa au kichocheo chake ni ubatili sana wa fikra.Tuombe yasitukute.
uliwah kwenda huko mbinguni?Hata padre wa Asimwe majibu lazima yatakua haya haya.!
Kweli pesa haifungwi.!
Dunian haki haipo ipo mbinguni tu.
Iwapo ikitumika hivyo,ni jambo baya sana na dhulma kwa wahanga.Huleta mgagasiko kama si laana na mivurugano kwenye jamii husika.Lakini mkuu, Mirembe huwa pia inatumika kama backdoor kwa wahalifu wenye pesa kuepuka gereza, kuna wa kwetu tumehakikishiwa kuwa christmas haimkuti mirembe wala jela.
Tukipimwa kwenye uchumba lazima akili ziwe safi ila kuanzia miaka 3 ya ndoa kuendelea tukipimwa wote lazima tukutwe na ubovu wa akiliKabla ya ndoa tupimwe akili, ripoti za daktari zitumike kuweka pingamizi la ndoa iwapo mmoja dishi bovu......
Kuna tofauti kati ya haki na sheriaHata padre wa Asimwe majibu lazima yatakua haya haya.!
Kweli pesa haifungwi.!
Dunian haki haipo ipo mbinguni tu.