Mahakama ya ICSID: Professional bullying anayofanyiwa Profesa Mruma inafedhehesha jamii ya Wanazuoni

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
1,038
4,752
Profesa Mruma amepata pigo kubwa sana kwa umri wake; waliomtuma huko Duniani wamedhamiria adhalilishwe na lengo limetimia . Anaulizwa kwa fedheha " haya ndiyo unawafundisha wanafunzi wako wa UDSM?

Muuliza swali ni mtoto wake wa kumzaa. Kwanini tumeruhusu wasiojiweza watusimamie?

---
Winshear Gold Corp. Vs. United Republic of Tanzania (ICSID Case No. ARB/20/25).
Kesi hii ipo chini ya Rais Gabrielle Kaufmann Hohrer kutoka Uswizi.

Mashahidi wetu huko ni Prof. Mruma na Mwanasheria wa Serikali bwana Igenge.


---
Video 1: Profesa Mruma akihojiwa


Video 2: Mkurugenzi wa Huduma za Sheria(Wizara ya Madini) Edwin Igenge akihojiwa na Robert Denison

---
WASIFU WA PROFESA MRUMA

Dkt. Mruma ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye kwa sasa ni Profesa wa Jiolojia. Profesa Mruma kwa sasa anahudumu kama Kamishna wa Tume ya Madini nchini Tanzania.

Mwaka 2017 Hayati Rais Magufuli alimteua Prof. Abdulkarim Mruma kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta (TIPER)

Profesa Mruma alijizolea umaarufu 24 Mei, 2017 baada ya kuongoza Kamati maalum iliyondwa na Rais Magufuli kuchunguza mchanga ulio katika makontena yenye mchanga wa madini (makinikia) yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania

-
Dkt. Abdulkarim Hamisi Mruma Ph.D. M.Sc. B.Sc. ni Mkurugenzi wa Kujitegemea wa Tanzania Royalty Exploration Corporationration. Dkt Mruma ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako kwa sasa ni Profesa wa Jiolojia.

Masomo yake ya Uzamili yalijumuisha tafiti katika vyuo vikuu na taasisi za Serikali nchini Ujerumani, Ubelgiji, Zimbabwe na Ufini.

Ameandika ripoti za kiufundi kuhusu mada mbalimbali za kijiolojia na kuchangia katika majarida kadhaa ya kiufundi na yasiyo ya kiufundi juu ya anuwai ya masomo ya Jiolojia.

Orodha ya machapisho hayo ni pamoja na Jarida la UNESCO la Sayansi ya Ardhi ya Afrika na Jarida la Tanzania la Sayansi ya Dunia.

Mbali na majukumu yake ya kitaaluma, Dk. Mruma ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania nafasi ambayo ameitumikia tangu Oktoba 2004.

Pia anahudumu kama Mjumbe wa Bodi ya Chuo cha Sayansi za Ardhi cha Williamson Diamonds Limited cha Chuo Kikuu cha Dodoma na Shirika la Madini la Taifa la Tanzania mshirika wa ubia wa Kampuni ya Uboreshaji wa Mradi wa Buckreef Gold Mine.
 
Hivi Mruma ni mtaalamu wa Sheria ama yule ni Geologist?

Why serikali inawatuma watu wa miamba wakalitetee taifa kwenye maswala ya Kisheria?

Muda mwingine unaweza kufikiria kuna baadhi ya watu wanataka Tanzania ishindwe, idaiwe Mabillion kisha nao wapate mgao.

Hilo ndio Tatizo letu Tanzania, tunataka mambo ya Miamba basi heads wa idara lazima awe geologist au Head wa Idara ya Afya head awe MD.

sasa case kama hiyo si bora angeenda lawyer kuwakilisha.
 
Kadhalilika wapi? au ujinga wa watu kujiona wanajua sana .

Rais anafanyiwa bullying sembuse huyo wengi wanamnanga Kwa ishu ya kisasa ,kwani kushindwa ni kosa ..yatapita tu na atabaki na familia yake ni maneno tu.


Kusoma hekima ndo maana watu wanafanya bullying ,kukosea kawaida mbona Mwakinyo alienda nje akapigwa alizomewa na kupewa kejeli ila sasa kashasahau na maisha yanaendelea
 
Hivi Mruma ni mtaalamu wa Sheria ama yule ni Geologist?

Why serikali inawatuma watu wa miamba wakalitetee taifa kwenye maswala ya Kisheria?

Muda mwingine unaweza kufikiria kuna baadhi ya watu wanataka Tanzania ishindwe, idaiwe Mabillion kisha nao wapate mgao.
Kwamba ukienda pale ndo utatetea kwanini ulifuta RL ambayo ilitakiwa isha 2023?

Wangeachiwa Leseni wakae nayo maana ilikuwa yaisha mwaka huu, badala yake 2018 tukaifuta kwa sheria ya 2017
 
Kuna MAFALLA WA NCHI HII WALIMTUKANA LISU SANA ALIPOTOA TAHADHARI HII LEO IMEJIBU
Screenshot_20230724-123434_Instagram.jpg
 
Profesa Mruma amepata pigo kubwa sana kwa umri wake; waliomtuma huko Duniani wamedhamiria adhalilishwe na lengo limetimia . Anaulizwa kwa fedha " haya ndiyo unawafundisha wanafunzi wako wa UDSM?

Muuliza swali ni mtoto wake wa kumzaa.....kwanini tumeruhusu wasiojiweza watusimamie?
Nimejisikia vibaya sana
Law is not for everyone
 
Back
Top Bottom