Magufuli: Nimeigawa MV Dsm kwa JWTZ, wale wanaoiandika andika, wajue wanaandika "mzinga wa JWTZ"

You Gotta Love Bongo!!!

Watetezi wa huyu mtu wana kazi sana. Akiongea anazua jambo juu ya jambo. Sasa hiyo MV DSM ilikuwa chini ya ofisi ya Rais kiasi kwamba anaweza kuigawa tu!

Temesa iliyotoa Shs. bilioni nane kununua hicho kivuko italipwa au ndiyo washaharibu bajeti? Bongo raha sana kuwatawala watu wake.
 
Haaaah sometimes inabidi kucheka tu ......

Kuna muda Rais namwelewa sana lakini kuna muda nashindwa kumwelewa kabisa kwa kauli zake............

Hivi JWTZ ndio watumie vitu vibovu na wananchi wasiseme kisa kuogopa?...................

Siku kikiwamwaga kwenye maji na wakafa itakuwa ni faida ya nani?...........

Kaburi la KInondoni hilo amesema hataki kufukua MAKABURI
 
Daaah!!
Imenistaajabisha sana.
Hivi watanzania tunaelekea wapi ?
Au ni urithi gani tunawaachia watoto/wajukuu zetu kwa akili hizi.

Hata kama mtu unaficha madhambi yako naona bora angenyamaza yapite tu kuliko hiki alichokifanya kwa sababu ni aibu ya karne na karne.

Mlidhani aliposema hafukui MAKABURI mlifikiria nini??Ni bora na Barabara nazo azipeleke Jeshini ili tusizijadili
 
kwa hiyo hata kama ni kibovu maadam ni cha jeshi kisijadiliwe.
Ukijadili ubovu wa meli ya jeshi ndo utakua unatengeneza?

Jadili Facebook kule ukiwa na jina lako halisi baada ya siku chache utatuambia alipo 8 o'clock.
Asante kwa msaada wako
 
Daaah!!
Imenistaajabisha sana.
Hivi watanzania tunaelekea wapi ?
Au ni urithi gani tunawaachia watoto/wajukuu zetu kwa akili hizi.

Hata kama mtu unaficha madhambi yako naona bora angenyamaza yapite tu kuliko hiki alichokifanya kwa sababu ni aibu ya karne na karne.

Ha ha ha, wanadhani bado akili zetu ni za miaka ile.

Ndiyo maana hata hawataki kuboresha mifumo ya elimu ili tuendelee kuwa wajinga, tuendelee kutowachallenge, tuwe wazee wa ndiyo mzee, wajanje wao.
 
Kwani si nilisikia kinatengenezwa then kitakua kinafanya safar za mafia duh basi siendi tena mafia mzigo unaenda jeshini tena
 
Back
Top Bottom