Magufuli atafia ufisadi, mimi nitafia demokrasia

Wewe na mabwana zako mnashindwa kuelewa kuwa penye demokrasia ya kweli hakuna ufisadi?

Tunashindwa kuwasaidia kwani mmepungukiwa akili, mngepungukiwa damu tungejitolea tukawapa!
Demokrasia kwa Zitto anaona ni bora, lakini yeye aendelee kupiga hela za PAC na mikataba fake, kwake ni poa tu, watu waibe wagawane hela za nchi, wafanye watakacho wawe wazembe kazini, so far kuna Demokrasia kwake Zitto ni poa tu! Huyu ameshavurugwa kwa sasa, hana tena maono!
 
Unaweza ukasema unapunguza Bajeti ya CAG na wakati huo huo unataka kupambana na ufisasi?!!!!
 
ninachowapongeza viongozi wengi wa upinzani ni kuilinda katiba japokuwa inalalamikiwa. kwa upande wa ccm kuvunja katiba ni jambo la kawaida kwao. hongera mh. zitto.
 
Zitto kaongea mengi na ya ukweli kabisa. Rais awe wamwisho kutoa kauli tene baada ya kujiridhisha kwa 100%.
 
Ni unafiki wa hali ya juu Mkuu. Huku ukijifanya ni mpambanaji dhidi ya ufisadi uliokithiri nchini na wakati huo huo ukikata bajeti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa more than 50%.

Tangu lini mkaguliwa akapanga bajeti ya anayemkagua? Kamati ya Bunge ilipanga bajeti ya shilingi bilioni 69 kwa CAG lakini serikali ( mkaguliwa ) imeipiga panga mpaka shilingi bilioni 32.

Unaweza ukasema unapunguza Bajeti ya CAG na wakati huo huo unataka kupambana na ufisasi?!!!!
 
Nasema ZZK uwezo wake wakufikiria umeshuka kama wa panzi!
  1. Si ndiyo ninyi mulimuita JK na serikali yake ni dhaifu???
  2. Mkasema hawashughulikii mafisadi??
  3. Sasa ufisadi siyo ajenda???
  4. Na hayo mambo ya bunge na taratibu zenu za kibunge zinatuhusu nini sisi na demokrasia???
  5. Je si mumesimamishwa kwa kanuni??
  6. Mbona wewe hujaweka kifungu kinachosema ulisimamishwa kimakosa??
Bora kuendelea na CCM yangu kwa raha na mustarehe.

Rudia kusoma maana una kila dalili za kukurupuka, hivi pande hiyo kukurupuka ishakuwa contagious?
 
hivi ZITTO kabwe ulimuunga mkono JMP kwa nini,na leo kwa nini unampinga
Msome Zitto vizuri utaona bado kuna mambo anamuunga mkono JPM na ameyaweka wazi. Yapo pia anayoyapinga, na ameyaweka bayana. Tunakuwa wavivu wa kusoma lakini wepesi wa kutoa maoni.
 
  • Thanks
Reactions: 911
Upinzani una wakati mgumu sana utawala wa Magu
Ni kweli kabisa hasa kwa mkakati wa makusudi wa kubaka demokrasia ndani na nje ya bunge. Wembee, udhalimu wa serikali hii una mwisho. Hapa hapa ambapo upinzani una wakati mgumu ndipo upinzani utaibuka triumphant kwa sababu serikali inaanza kujenga usugu si kwa wana siasa wa upinzani peke yaka bali kwa wapenda democrasia wote.

Wakati utasema!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ni unafiki wa hali ya juu Mkuu. Huku ukijifanya ni mpambanaji dhidi ya ufisadi uliokithiri nchini na wakati huo huo ukikata bajeti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa more than 50%.

Tangu lini mkaguliwa akapanga bajeti ya anayemkagua? Kamati ya Bunge ilipanga bajeti ya shilingi bilioni 69 kwa CAG lakini serikali ( mkaguliwa ) imeipiga panga mpaka shilingi bilioni 32.
Bahati mbaya watanzania wengi hawajui kinachoendelea na zaidi si wafuatiliaji wa mambo ingawa ndio wapiga kura.
 
Na washauri wa Baba J.esca (kama anao) wanamuhofia kumwambia kweli kwamba huko anakotaka kuipeleka nchi siko kabisa, huko anakoelekea ni mwanzo wa majanga makubwa nchini.

Aisee siasa za kinafiki Ni hatari Leo unamsifia msaliti zito kabwe kwa kuwa msaliti katofautiana na mh rais , ha ha ha ,

Unachotakiwa kuelewa , nchi hii itaenda huo ushauri mpatie MZEE wenu fisadi aliyegeuka malaika

Nyie hamna jema hata mkiambiwa hapa tuko peponi na rais toka CCM hamtakubali lazima muhamie jehanam
 
Na washauri wa Baba J.esca (kama anao) wanamuhofia kumwambia kweli kwamba huko anakotaka kuipeleka nchi siko kabisa, huko anakoelekea ni mwanzo wa majanga makubwa nchini.
Watakuja kushituka wakati wameshachelewa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Zitto hana lolote, ufisadi ka u ditch. Ha ha ha ha
Yani bora ufisadi .Duuu sasa huyu mtu anafikiria nini, ya kwamba unaweza kuwa na nchi yenye demokrasia ambayo ina ufisadi? Sasa utapata je demokrasia kama kuna ufisadi, maana ktk nchi ya kifisadi unaweza nunua demokrasia. Yani nchi ya kifisadi unaweza nunua haki ya mtu bila tatizo ama unaweza nunua kura za wapiga kura bila tatizo ama unaweza nunua uhuru wa mtu kujieleza. sasa Zitto anaongelea demokrasia gani ktk nchi ya kifisadi? Zitto should check with his doctor , ASAP.
Wewe ni sawa na yule aliyesema kuwa hana haja ya kudoma uzi wa ZZK; ye yuko na JPJM. kuna siku utakuja kuuliza eti zzk alisema nini siku ile!!!! We endelea na mtakatifu wako.
 
Hujitambui wewe hivi huu ubakaji demokrasi nchini hadi sasa umemuathiri Zitto tu!? Tafakari kwa kina acha kukurupuka.

Jema lipi hapa unalozungumzia? La kuwakwepa mafisadi wa Lugumi, escrow, UDA, Pride, MV Dar au Rais kukwepa kulipa kodi!?

Aisee siasa za kinafiki Ni hatari Leo unamsifia msaliti zito kabwe kwa kuwa msaliti katofautiana na mh rais , ha ha ha ,

Unachotakiwa kuelewa , nchi hii itaenda huo ushauri mpatie MZEE wenu fisadi aliyegeuka malaika

Nyie hamna jema hata mkiambiwa hapa tuko peponi na rais toka CCM hamtakubali lazima muhamie jehanam
 
Hujitambui wewe hivi huu ubakaji demokrasi nchini hadi sasa umemuathiri Zitto tu!? Tafakari kwa kina acha kukurupuka.

Jema lipi hapa unalozungumzia? La kuwakwepa mafisadi wa Lugumi, escrow, UDA, Pride, MV Dar au Rais kukwepa kulipa kodi!?

Hivi wewe unajielewa kweli , uvunje sheria uachiwe kwa misingi ya demokrasia hivi unaijua demokrasia kweli ? Au unafikiri demokrasia Ni mikutano ya siasa , yaani hujui hata Uhuru ulionao wa kuandika humu Ni demokrasia , na kila ulifanyalo kwa Uhuru hujui Ni demokrasia , kutukana viongozi wa nchi na kuwaita majina ya kejeli hujui Ni demokrasia ?

Au umekaririshwa demokrasia Ni kupayuka kwenye majukwaa na kuvunja sheria , nyie ukawa sijui huwa mnawaza nini?
 
Back
Top Bottom