Tarakilishi
JF-Expert Member
- May 19, 2013
- 2,181
- 2,448
Hili suala linahitaji maamuzi magumu mkuu. Enzi za ukoloni walikuwa wanachapa vibokoNdugu nataka tutambue kuwa hawa watu wanaoishi katika bonde la mto Msimbazi si wale waliondolewa awali kwa asilimia 100, bali wengi ni waliolowea kwa kuepuka adha za kulipia kodi za nyumba, wengine ni watu waliojikatia tamaa hawana dira wamepeleka makazi yao hapo, na wengine ufinyu wa mawazo umewadanganya kuwa watahamishwa na kutendewa fadhili kama wale wa awali.
Hawa watu mpaka unawaonea huruma, ukisema watumwe polisi wakawapige virungu ili wahame bado kuna ukakasi, ukiwaacha pia ni sawa na kumruhusu mtoto achezee moto, ukiwapa fadhila za kuwahamisha kistaarabu kwa kuwapa viwanja ndo utakuwa mchezo wa wengi.