Mafuriko Dar: Watu kadhaa wamekwama kwenye maji Jangwani, wengine wapoteza maisha

Sasa watu wangewachangia hawa waathrika wa mafuriko,ila kwa yaliyo tokea kule Bukoba sijui kama wapo wengne wenye moyo wa kuchanga labda wapo lakini mmmmh.
 
hawa watu waliondolewa miaka kadhaa iliyopita wakapewa viwanja sasa hao ambao wamekumbwa na mafuriko kwenye hilo eneo wametoka wapi. jamani mwafaaaa
 
uchange ya nini na kati walipewa viwanja wakayauza si unajitakia matatizo mwenyewe. walitakiwa wapelekwe mahakamani kwa kosa la kutaka kujiua
 
hawa watu waliondolewa miaka kadhaa iliyopita wakapewa viwanja sasa hao ambao wamekumbwa na mafuriko kwenye hilo eneo wametoka wapi. jamani mwafaaaa
Wafe tu.

Wakati mwingine ni bora utoe kafara ili wajifunze hao wengine
 
Ndugu nataka tutambue kuwa hawa watu wanaoishi katika bonde la mto Msimbazi si wale waliondolewa awali kwa asilimia 100, bali wengi ni waliolowea kwa kuepuka adha za kulipia kodi za nyumba, wengine ni watu waliojikatia tamaa hawana dira wamepeleka makazi yao hapo, na wengine ufinyu wa mawazo umewadanganya kuwa watahamishwa na kutendewa fadhili kama wale wa awali.
Hawa watu mpaka unawaonea huruma, ukisema watumwe polisi wakawapige virungu ili wahame bado kuna ukakasi, ukiwaacha pia ni sawa na kumruhusu mtoto achezee moto, ukiwapa fadhila za kuwahamisha kistaarabu kwa kuwapa viwanja ndo utakuwa mchezo wa wengi.
 
Hawa jamaa wajangwani kuna mtu wanamtafuta maneno ngoja tutasikia tu wakianza kulalamika, labda wakae kimya.
 
Dar kuna shida ya mitaro ya maji kwa kweli haikuwa mvua ya kusababisha mafuriko

Ni kweli mkuu, ila pamoja na kupiga marufuku pombe ya kwenye viroba, lakini mitaro bado imejaa viroba vilivyoyumika!!!!!!!!
 
Upumbavu ni kufanya kitu kilekile kwa mbinu zilezile na kutegemea matokeo tofauti, kila mwaka kesi ni ileile ya miundombinu inaachwa kwenye hali duni vilevile na mvua zinaponyesha matarajio ni kuwa maji yatapita vizuri tu bila kusababisha maafa!
Hivi aliyeroga watanzania ni nani jamani?

Nenda pale DIT manyunyu tu mimaji hiyo hata huoni njia jamani jamani ina maana bado anasubiriwa Mwalimu Nyerere aje kufanya haya!
 
Mvua iliyonyesha leo Dar imeleta maafa sana kwani hadi sasa watu kadhaa wamekwama kwenye maji maeneo ya Jangwani Mto Msimbazi.

Jeshi la Uokoaji limeshafika na vifaa maalum vya uokoaji. Ila nashangaa Askari wengi wakiwa na bunduki na magwanda yao bila vifaa maalum
View attachment 478058
Boat inaandaliwa kuingizwa kwenye maji ili kuokoa watu

======

UPDATES: 1330hrs

=> Hadi sasa mtu mmoja ameshaokolewa na Kikosi maalum cha uokoaji. wanatumia boat maalum inayojazwa upepo.
View attachment 478065
=> Mwili uliotolewa kwenye maji ni wa Kijana kati ya Miaka 25 na 32. Sina uhakika sababu hayupo hai.
View attachment 478066
View attachment 478136 View attachment 478137 View attachment 478138
Kikosi Maalum cha Uokoaji kikiendelea na kazi

=> Kwenye maji haya ya Msimbazi kuna watu bado wanaonekana vichwa kwa mbali. Hatujajua hali zao zikoje. Ila shughuli ya Uokoaji inaendelea.

=> Helicopter ya Polisi inaimalisha ulinzi kwa juu huku ikiangalia kama kuna watu zaidi wamekwama majini
View attachment 478067
Chopa ya Polisi
View attachment 478125 View attachment 478126

Kwa hali hii, bora mwaka huu Mvua isinyeshe Dar es Salaam Mwaka huu. Sababu leo Mvua ilinyesha kidogo tu lakini imeleta maafa. Je ikija kunyesha mvua kubwa itakuwaje?

Mungu atuepushie mbali balaa hili.

Naishauri Serikali kutumia mfano huu iwe fundisho kwao, Wazibue mitalo na sisi wananchi tuache kutupa vitu na uchafu kwenye mifereji ya maji.
Gharama na ufundi vilivyotumika kuzibua huo mto tukitajiwa hapa wengine watakufa kwa shinikizo la damu
Kimsingi kilichofanyika ni maigizo tupu na kuitia serikali hasara kubwa! Imagine watu wanatumia gharama kuzibua mwanzoni na katikati halafu wanakuacha mwishoni kwenye matoleo as if unataka kutengeneza bwawa
 
Back
Top Bottom