Mafanikio ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) chini ya Juliet R. Kairuki

Nimeisoma taarifa yako kwa makini sikiona "specific achievements" za huyo mama. Kwa kuwa ulisema amefanikisha miradi mingi kuliko watangulizi wake wawili, mafanikio ya TIC ungeonyesha 1997 to 2012 na 2013 todate tuweze kulinganisha unachozungumza
 
My Brother Pascal:
Nikushukuru kwa andiko kubwa sina uwakika kama walimu wako wakipitia hapa watakumbuka insha moja kama hii....umewahi kuandika ukiwa shuleni.. Mimi sina shida na utetezi wakooo sanaa ila najiuliza why Julieth? katika wote walioondolewa hakuna aliyefanya kama Julieth?
Umepata wapi hizi record zote ulikuwa unafanya PHD ya TIC? .......
Ameondolewa Simba TCRA ambaye alikuwa na miezi 10 hukuja hivi kaka? Umesema rais anaweza fanya kitu sahihi kwa njia isiyo sahihi umeonyesha ubinadamu wako na wewe hapa.... please tueleze umewezaje kupata all these data in two days only and why Julieth?

Pia nichukue nafasi hii kumpongeza julieth kwa kazi alizofanya kama ulivyosema....Mr president anamuitaji sehemu nyingine kama atakuwa tayari najua kwa moyo wake wa kuchapa kazi nafasi nyingine ataonyesha ubora wake....ila nchi lazima iendeshwe kwa principle .....

Tuendelee kumwombea rais wetu afya na hekima zitokazo kwa Mungu ili aweze kutuongoza kwa haki na mafanikio badala ya kukaa na kusubiria akosee for sure ni mwanadamu atakosea ila tusimame kwenye zamu zetu kwa ajili ya nchi yetu.
Mkuu umeandika vyema lakini kuuliza why Julieti
utakuwa unafanya kosa.... kama wewe una Data za Simba basi zilete, kaeleza kwamba alikuwa mwandishi wa TIC tangu inaanza enzi za mzee wetu 6.... njoo na hoja na sio personality mkuu...
 
Halafu eti watu wanataka watanzania wa Diaspora warudi kufanya kazi nchini.Na mijitu isiyostaarabika na kuheshimu taaluma za watu kama hii?

Wamemuonea sana huyu Dada. Sio haki hata kidogo.
 
Kwa mfano huu wa aliyekuwa mkurungezi wa TIC wataalam wengi wa Tanzania wanaofanya vizuri nje ya nchi wataogopa kurudi Tanzania kuisaidia nchi yao kwa kuogopa aibu kama aliyoipata Bibi Julliet Kairuki.

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Kwa mfano huu wa aliyekuwa mkurungezi wa TIC wataalam wengi wa Tanzania wanaofanya vizuri nje ya nchi wataogopa kurudi Tanzania kuisaidia nchi yao kwa kuogopa aibu kama aliyoipata Bibi Julliet Kairuki.

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
bora wabaki huko huko kama wanataka mshahara mkubwa wakati perfomance ni zero wabakie huko huko tu .kuna watanzania wengi wasomi wanaweza kufanya hizo kazi
 
Wanabodi,
Hitimisho.
Pamoja na yote haya huyu mama aliyoyafanya, yamemkuta ya kumkuta, wakati sisi tunanyanyapaa kwa mshahara wa milioni 5, sasa subirini wenzetu watakavyo mgombania!, japo hakutendewa vema, lakini you never know, everything happens for a reason, na kuna majanga mengine huwa ni blesing in disguise!.
Nampongeza kwa kazi nzuri TIC, Mungu ambariki. Paskali.

Hata ajikoshe vipi, kujilipa posho ya 400m/- kwa muda wa miaka 3 kwa nchi maskini kama yetu ni hela nyingi mno, lazima atumbuliwe tu, na kila mwezi kukaa siku 10 nje ya nchi?!
Wacha arudi SA wamlipe mabilioni, kwa uwezo wetu hatuwezi, na aende kwa usalama, bye...
 
Mi nadhani hatua anazochukua Magufuli ndio kurekebisha mfumo kwenyewe ambako wananchi wengi na hasa humu jamvini wamekuwa wakililia. Kwa kisanga hiki, mfumo unataka mtu aajiriwe na apewe mkataba. Sasa kama mtu hakubaliani na mshahara maana yake aache hiyo kazi. Hiyo ndiyo kanuni na mfumo unajengwa na kanuni.

Alipotumbuliwa Kilango kuna watu walilaumu. Lakini ili kuwa na mfumo ambao ni imara maana yake watendaji wanatakiwa kusimamia kanuni na hawatakiwi kupepesa macho katika maamuzi yao. Ndiyo maana Magufuli alisema anasikitika kwamba Mkuu wa Mkoa hakutoa taarifa sahihi na hivyo akamwajibisha. Hivyo ndivyo mfumo unavyotakiwa kusimamiwa. Kwamba kiongozi anaweza akakwambia, "I am sorry, but I can't help it, you have to go!" Na wakati mwingine kama wazungu wafanyavyo, "with a smile". Kwamba nakupenda lakini samahani.

Majuzi pia bosi wa TCRA alipotumbuliwa baadhi ya watu walitaka kulaumu. Kwa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, kabla ya uamuzi wa kumsimamisha Dkt Simba, kulifanyika kikao Ikulu kilichowahusisha rais na viongozi wa wizara ya mawasiliano, fedha na TAKUKURU. Bila shaka na Ndugu Simba alikuwepo ili atoe utetezi wake.

Pia wengi wetu tunasahau utumbuaji huu, kwa sehemu kubwa unatokana na taarifa mbalimbali za nyuma zikiwemo zile za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) za miaka ya nyuma. Ninavyofahamu mpaka sasa JPM hajaanza rasmi kutekeleza mapendekezo ya taarifa za CAG za karibuni (2014/2015). Hivyo tujiandae kupokea taarifa zaidi za utumbuaji kwa maana ya utekelezaji wa mapendekezo ya CAG hasa baada ya Bunge la bajeti kumaliza kujadili pia taarifa za CAG.
 
Paschal imekuuma sana,kuwa muangalifu na maneno yako,unaposema kakomolewa mwandishi nguli ka wewe huweki ushahidi, unatupa mashaka magufuli ana nyenzo nyingi za kupata habari za Tic kuliko wewe mzabuni tu.

Leo kwa kutetea ugali wako umeandika dibaji ndeefu,siku zote ulikua wapi au mtu wa Tic wa Pr alikua wapi.

Tupo vitani, atakaejaribu kutukwamisha "tutampasua" kichwa!

Mkuu Pascal hatakiwi kuja na ushahidi kuwa huyu mama hana hatia ......... ndiyo maana barua ya kutengua post yake inasema atapangiwa kazi nyingine kama anataka kuendelea kufanya kazi serikalini!!

Tatizo ni Rais kutengua uteuzi bila kuto sababu zenye mashiko!! Nitasupport hii design ya utumbuaji kama hawa watu wangekuwa wanatumbuliwa na siku hiyo hiyo wanakamtwa na kufunguliwa mashtaka!!

Personally, simsupport huyu Mama kwa kwa vile ali apply mwenyewe na akapitia interview kibao na kuibuka mshindi. Kwa maana hiyo alijua kabisa maslahi ya hiyo post. Otherwise, hiyo interview ilikuwa ni gelesha tu na mipango ilikuwa ishafanywa nyuma ya pazia na huenda hata hakushinda!!
 
Halafu eti watu wanataka watanzania wa Diaspora warudi kufanya kazi nchini.Na mijitu isiyostaarabika na kuheshimu taaluma za watu kama hii?

Wamemuonea sana huyu Dada. Sio haki hata kidogo.
hao diaspora wamesaidia nini nchi hii..Tanzania wasomi wako wengi watafanya hizo kazi...posho milioni 25 kwa mwezi ni ufisadi tu tena amechelewa sana kutumbuliwa
 
Makala ndefu sana, nitaendelea kuisoma ila mpaka nilipofika, ni kwamba umeandika article ya kumtetea, haujawa neutral. Nina uhakika TIC kuna madudu pia, ungeweka pande zote humu, mwandishi nguli kama wewe hutakiwi kuandika stori ya kuegemea upande mmoja, maana ulichoandika hapo ni article.
 
Nchi hii haina shukrani kabisa wala staha katika kushughulikia mambo ya kiutumishi kwa sasa,sheria zipo lakini kuna baadhi wanafikiri wakidhalilisha watu nafsi zao zinatulia,kuna haja gani ya kuita magazeti na televisheni ili umdhalilishe mtu wakati sheria imekupa njia za staha za kuachana naye? Yaani ina maana hakuna jema lililofanyika? Hata shukrani kwa utumishi wake hakuna? Alifanya kosa gani?kusubiri mshahara uongezwe?
Wanapoguswa ndugu zetu, punguzeni jazba. Sielewi staha gani inayotakiwa kuwaondoa madarakani wanaovuruga kazi. Kama ni wema, hata walio kifungoni siyo kwamba hawajawahi fanya mambo mema. Unahukumiwa kwa matendo mabaya siyo kwa mema ya zamani.

Ukisoma historia ya nchi hii, tangu mwalimu kuna watu walifukuzwa kazi pale mnazi mmoja. Akina Mtei walifukuzwa na maandamano juu yake kibao kwa nchi nzima. Mambo yako hivyo hata enzi za Mwinyi, Mkapa na hata Kikwete. Sasa eti munaandika Magufuli kazidi.

Kuna jambo moja la ajabu sana linajitokeza. Kwa uwazi watu wanashambulia mbinu ya Rais, lakini enzi za Kikwete hakuna aliyethubutu. Hiyo ni ishara ya wema wa Rais wa sasa. Hata anajibizana na watu wanaolalamika magazetini. Enzi iliyopita nasikia watu walikuwa wanafuatiliwa kimyakimya.
 
Mkuu Pascal Mayalla, shukran kwa andiko zuri nimekuelewa sana ila wapo watu ambao wakisikia fulani kapata tatizo kwao ni furaha utadhani wanakula wali nazi.

Ukweli ni kwamba mwenendo wa Rais Dr Magufuli na inner circle yake wanaweza kuipeleka nchi ambao siko kabisa iwapo hawatakuwa tayari kusikiliza ushauri na maoni ya wananchi wenye upeo mkubwa na si hawa wapiga debe.
Prof Ngongo

Huyu Rais Magufuli siyo mswahili bana muache afanye kazi yake hii siyo serikali dhaifu hata kidogo.
 
Huyu Pascal Mayalla ni mwandishi wa habari na moja ya kazi ya waandishi ni mambo ya PR.

Hata wewe ukitaka kusafisha jina lako mnapatana bei ya kufanya hiyo kazi halafu anatunga atakusafisheje anatafuta takwimu za hapa na pale za kuunga unga anazichapisha iwe kwenye blog gazetini au popote kisha unamlipa chake.

Biashara inaishia hapo.Ukitaka aendelee unaongeza dau

Tatizo letu kubwa ni kusahau sahau mambo kirahisi; huyu Pasco ndio yule yule aliyekuwa anampigia jalamba Lowassa wakati wa kiny'ang'anyiro cha URAIS!!! Alimtetea sana Lowassa na wote sie tunajua kuwa Lowassa alikuwa ameweka fungu maalum la watu kama huyu; hivyo unaposoma mabandiko yake ni lazima uelewe kuwa nyuma yake kuna bahasha ya khaki!!! Huyu hana tofauti na Manyerere aliyehongwa safari moja ya kwenda Cuba enzi za mkweree halafu wakamsahau na akawa mkali kweli dhidi ya utawala wa JK!!!
 
Andiko hili linanikumbusha wakati ukiwa kwenye msiba/mazishi!

Utaona watu wanasoma taarifa ndefu na kuelezea kuhusu wasifu mzuri wa marehemu kama kwamba atawakumbuka kuzimuni. Honestly, It's just a waste of my time.

Huyu Dada is gone and finished kwenye kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Kusema alikuwa mfanyakazi mzuri haisaidii lolote labda kama unataka akukumbe atakakoenda.
 
Ukiona Pascal kajitokeza Mzima namna hii...ujue Dada kajiandaa...!(Natania)
=======================================================
Pascal Asante sana kwa kutumia muda wako kutujuza juu ya Mafanikio ya Julieth Kairuki , kama mkurugenzi wa TIC.

Lakini, nadhani kunavitu umevirudika ama kwa makusudi ama kwa kutokujua juu ya mafanikio ya TIC kiasi cha kuonekana mazuri yote yamefanywa na Julieth.Kwa uandishi huu yawezekana ukaonekana unapotosha umma kwa makusudi ama la. Umeeleza vizuri jinsi TIC ilivyoanza, majukumu yake na walioongoza TIC kama wakurugezi (Sitta, Ole, Jully(aliyetenguliwa)). Kwa msisitizo kabisa ukasema Uongozi wa Jully umekuwa na mafanikio maradufu kuliko watangulizi wake. Na hii ndiyo hasa lilikuwa lengo lako kutujuza wanajukwaa.

Chakusikitisha Pascal, kwa kutumia majukumu ya TIC, umeshidwa kuonyesha kwa uwazi namna wakurugezi hao waliotangulia walichokifanikiwa kufanya kulingana na majukumu yao ambacho ni kidogo kulinganisha na Jully alichokifanya kwa kutumia majukumu hayo hayo. Tena ulitakiwa kutuonyesha, moja baada ya lingine; toka Jully ameingia kazini (2013) amefanya jambo gani ,siku gani,mwezi gani na mwaka gani. Ulitakiwa kufanya hivyo hivyo na kwa wakurugenzi waliomtangulia (Sitta, Ole). Ungefanya hivyo ungemtendea haki Jully na wakurugenzi waliomtangulia. Kwa kukukosekana unyambulisho huo ndiyo nasema ama ulikusudia ama hukujua!!!!

Pia nime"vutiwa" na maelezo yako haya.

1...Utoaji huduma za vibali na leseni mbalimbali kwa wawekezaji chini ya mfumo wa “One Stop Shop”.
Katika kipindi cha cha 2005 hadi 2014 Kituo kimeendelea na maboresho katika kuhudumia wawekezaji ili kupata vibali mbalimbali kwa haraka wakati wa utekelezaji na uendeshaji wa miradi. Katika maboresho hayo Wizara ya Kazi na Idara ya Uhamiaji imeteua maofisa kuidhinisha vibali hivyo kwa niaba ya Makamishna wa Kazi na Uhamiaji. Mpango wa baadae ni kuhakikisha kuwa huduma nyingine zote zikiwepo za Kodi, ardhi, kufungua kampuni n.k zinatolewa ndani ya TIC kwa mfumo huo hapo juu nakuanza kutumia mitandao ili kurahisisha utoaji wa vibali.


2...Katika kipindi husika kitengo cha ardhi kiliendelea kutoa huduma za ushauri kwa wawekezaji katika masuala mbalimbali ya ardhi pamoja na kuainisha maeneo yenye ardhi kwa ajili ya uwekezaji katika maeneo mbalimbali ya Tanzania. Kitengo cha Ardhi Kilifanikiwa kilishughulikia jumla ya maombi 15,969 ya kumilikishwa ardhi, na jumla ya hati zisizo asili Derivatives /Leasehold title 39 zimekamilika na kukabidhiwa wawekezaji.


1....Kwamba wawekezaji..wamerahisishiwa kupata vibali. Sina hakika kama hili ndilo lililofanya tuanze kuona "wawekezaji wa kuchuuza kandambili" jiji Dar es Salaam!!? Na sema sina hakika, yawezekana TIC ilishindwa kutofautisha wawekezaji Mikwara na wawekezaji Makini. Sasa Pascal hukuweka mtiririko wa matukio ndani ya TIC, hivyo tunashindwa hili la wawekezaji mikwara tumbebeshe Sitta, Ole ama Jully!!!
2....Ardhi ama ya wakulima, wafugaji nakadhali ama iliyo'mbich' imepata wawekezaji. Heh..! tumesikia malalamiko mengi juu ya uporaji wa ardhi kiasi cha kusababisha migogoro ya ardhi kati ya wawekezaji na wananchi...Hili pia tunashindwa kumbebesha Ama Jully, Ole ama Sitta, maana Pascal hukutoa chronological order ya matukio kulingana na mkurugenzi aliyehusika.

Kama una nafasi ebu tupe nyambulisho wa mafanikio ya Jully, Ole, na Sitta. Uwezo huo unao maana unatakwimu za kutosha kulingana na Post namba moja ya uzi huu.

===TUJITEGEMEE
 
Halafu eti watu wanataka watanzania wa Diaspora warudi kufanya kazi nchini.Na mijitu isiyostaarabika na kuheshimu taaluma za watu kama hii?

Wamemuonea sana huyu Dada. Sio haki hata kidogo.
Nawe mkuu hebu tumia uzoefu wako JF vizuri. Huyo mdada achana naye. Diaspora wanaweza kurudi kwa manufaa ya Taifa. Unatetea mtu anayerudi toka diaspora kwa social interactions na mtu mmoja tu! Let her go forever!
 
My Brother Pascal:
Nikushukuru kwa andiko kubwa sina uwakika kama walimu wako wakipitia hapa watakumbuka insha moja kama hii....umewahi kuandika ukiwa shuleni.. Mimi sina shida na utetezi wakooo sanaa ila najiuliza why Julieth? katika wote walioondolewa hakuna aliyefanya kama Julieth?
Umepata wapi hizi record zote ulikuwa unafanya PHD ya TIC? .......
Ameondolewa Simba TCRA ambaye alikuwa na miezi 10 hukuja hivi kaka? Umesema rais anaweza fanya kitu sahihi kwa njia isiyo sahihi umeonyesha ubinadamu wako na wewe hapa.... please tueleze umewezaje kupata all these data in two days only and why Julieth?

Pia nichukue nafasi hii kumpongeza julieth kwa kazi alizofanya kama ulivyosema....Mr president anamuitaji sehemu nyingine kama atakuwa tayari najua kwa moyo wake wa kuchapa kazi nafasi nyingine ataonyesha ubora wake....ila nchi lazima iendeshwe kwa principle .....

Tuendelee kumwombea rais wetu afya na hekima zitokazo kwa Mungu ili aweze kutuongoza kwa haki na mafanikio badala ya kukaa na kusubiria akosee for sure ni mwanadamu atakosea ila tusimame kwenye zamu zetu kwa ajili ya nchi yetu.


Smart Mwananchi,

nimekupenda kabisa. Umeandika masuala ya msingi sana mwanzo mwisho. Maswali yako ni ya msingi sana kwa Pascal. Tunategemea ayajibu hapa jamvini.
 
Paschal imekuuma sana,kuwa muangalifu na maneno yako,unaposema kakomolewa mwandishi nguli ka wewe huweki ushahidi, unatupa mashaka magufuli ana nyenzo nyingi za kupata habari za Tic kuliko wewe mzabuni tu.

Leo kwa kutetea ugali wako umeandika dibaji ndeefu,siku zote ulikua wapi au mtu wa Tic wa Pr alikua wapi.

Tupo vitani, atakaejaribu kutukwamisha "tutampasua" kichwa!
Huyu jamaa kalogwa. Makala ndefu ya utetezi wa figure za makaratasi, uhalisia zero.
 
Back
Top Bottom