Maeneo Yaliyotengwa Kwa Ajili Ya Uwekezaji Katika Halmashauri Ya Manispaa Ya Mtwara

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
157
242
Halmashauri ya manispaa ya Mtwara imetenga maeneo mengi kwa ajili ujenzi wa viwanda, hospitali za kisasa, vituo vya michezo, hoteli za nyota tatu, n.k. Maeneo hayo ni kama ifuatavyo:

(a) Ujenzi wa kiwanda cha kusindika nazi na kiwanda cha kuongeza thamani ya zao la korosho. Mamia ya Mtwara imetenga hekta 202 katika kata za Likombe na Mtawanya.

(b) Ujenzi wa kiwanda cha kusindika chumvi. Manispaa imetenga tofauti katika kata tofauti. Maeneo yaliyotengwa ni:

✓ Eneo la ukubwa wa karibia hekta 3 katika kata ya Mitengo.

✓ Eneo la ukubwa wa hekta 5 katika kata ya Mtawanya.

✓ Eneo la ukubwa wa hekta 12 katika kata ya Ufukoni.

(c) Ujenzi wa kiwanda cha kusindika samaki. Manispaa imetenga takribani hekta 5 katika kata ya Maghalani.

(d) Maeneo ya uwekezaji unaohusiana na utalii. Manispaa imetenga karibiana hekta 91 katika kata za Chuno, Shangani, Kiyanga, Kilimahewa, Ufukoni, na Mikindani. Eneo hili kimetengewa kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa:

✓ Hoteli.

✓ Vituo vya burudani na starehe.

✓ Michezo ya majini.

✓ Vifaa vya michezo ya kiuvuvi.

✓ Vituo vya utalii wa kiutamaduni kama vile mapango, dansi, n.k.

(e) Eneo la ajili ya sekta ya afya. Manispaa imetenga eneo kwa ajili ya mwekezaji wa kujenga hospitali moja ya kisasa na vituo viwili vya afya. Eneo la hekta 6 limetengwa katika kata za Mjimwema na Mitengo.

Nashukuru sana kwa kutenga muda wako wa thamani sana kulisoma andiko hilo. Ninaamini umejifunza mambo yatakayoleta mchango chanya katika safari yako ya kujenga/kutunza utajiri kupitia uwekezaji wa ardhi na majengo.

Ahadi yangu; Kozi Fursa Ya Wilaya (District Real Estate Workshop) ijayo itakuwa ya kipekee sana. Naomba ualike rafiki zako na jamaa zako tuweze kujifunza pamoja.

Kumbuka; Njoo ujiunge bure na makundi yetu ya whatsapp ya TZ Real Estate Team.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

Whatsapp; +255 752 413 711.
 
Back
Top Bottom