JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
775
947
Hivi karibuni kumezuka mijadala mingi juu ya uwepo wa zaidi ya watu zaidi ya laki Moja kuishi hifadhi ya Ngorongoro kuwa ni njia Moja wapo ya KUVUTIA UTALII ni ujinga na upuuzi usio vumilika hata kidogo.

Tumeshudia Waandishi wa habari Maulid Kitenge na Oscar Oscar Mzee wa Kaliua wakiwa wanaripoti kutoka Hifadhi ya Ngorongoro na kueleza ualisia unaoendelea hapo Hifadhini.

Kumejitokeza kundi la wajinga flani kwa maslahi yao binafsi bila kuangalia hali ilivyo wameanza kampeni ya kuwashambulia waandishi hao.

Tuangalie uhalisia, taarifa ni kuwa kuna jamii ya watu wachache ni wanufaika na shida za watu walio wengi maskini, huko Ngorongoro Tuendako watoto wanakufa, hakuna barabara, hakuna huduma za kijamii nk ndo maana MECIRA tunasema hatua za haraka zichukuliwe kuondoa hali ya hatari zaidi baadaye na sasa.

Shida inayoonekana hapo ni wafugaji kuingilia hifadhi, kwa ajili ya malisho na Taifa linaweza kukosa watalii kwani watakuwa wanafika kwenye hifadhi badala ya kuona pundamilia, au Twiga wanakutana na Ng'ombe na Taifa kukosa mapato yatokanayo na utalii.

Lakini pia kizazi Cha Sasa kitaona mazingira rafiki kwa malisho ni kwenye hifadhi kwani kitaona hakuna katazo lolote, kama wanahabari tunapaswa kuishauri serikali njia sahihi za kuepukana na hili tatizo, kazi iendelee.

Hakika mapendekezo ya Kitenge na Oscar* yanatakiwa kuchukuliwa haraka hatua za makusudi kwa ajili ya kuokoa kizazi ambacho kinaishi maisha hatarishi, na kuokoa hifadhi kuondokana na hatari ya kuwa jangwa.

Screenshot_20220207-130321.jpg

Screenshot_20220207-130306.jpg

Screenshot_20220207-130253.jpg
 
Maswali muhimu kujiuliza.

1. Idadi ya watu na mifuko hifadhini inaongezeka au la?

2. Kuna idadi ya watu au mifugo ikifikiwa hifadhi itakuwa hatarini kuharibika au hata kutoweka?

3. Idadi hiyo ikifikiwa nini kifanyike?
 
4.kipi ni muhimu kati ya binadamu na wanyama
 
(4/4).Nendeni field,watoto wanakufa. Hali ni mbaya.

Hakika mapendekezo ya Mshambuliaji na Oscar yanatakiwa kuchukuliwa haraka hatua za makusudi kwa ajili ya kuokoa kizazi ambacho kinaishi maisha hatarishi, na kuokoa hifadhi kuondokana na hatari ya kuwa jangwa. https://t.co/ONGXa0oTyh
 
Wazungu wanawapenda wamasai lakini na kuwaona huko pia ni fahari kwao!

Sasa we endelea na upambe tu mkimalizana nao muende na kwa Wahandzabe mkawafurushe nao maana hii ni awamu ya kumnyanyasa mwananchi wa kawaida
 
Umenena vyema Sana mkuu, kimsingi wale wamasai walitakiwa waondolewe Mara tu baada ya Ngorongoro kutangazwa kuwa hifadhi.

Hakukua na haja ya kuwaacha pale, Ngorongoro kama Ngorongoro inajitangaza yenyewe bila hao wamasai.

Narudia kusema Ngorongoro imekuwa ya kipekee kutokana na uwepo wa wamasai na mifugo yako ni upuuzi wa kiwango cha SGR.

Hifadhi ya Ngorongoro ni ya kipekee bila hao wamasai na ng'ombe zao...PERIOD
 
Umenena vyema Sana mkuu...kimsingi wale wamasai walitakiwa waondolewe Mara tu baada ya ngorongoro kutangazwa kuwa hifadhi...hakukuwa na haja ya kuwaacha pale...ngorongoro kama ngorongoro inajitangaza yenyewe bila hao wamasai. Narudia kusema ngorongoro imekuwa ya kipekee kutokana na uwepo wa wamasai na mifugo yako ni upuuzi wa kiwango cha SGR. Hifadhi ya ngorongoro ni ya kipekee bila hao wamasai na ng'ombe zao...PERIOD
Mkimaliza muende na kwa Wahadzabe mkawafurumushe
 
Wazungu wanawapenda wamasai lakini na kuwaona huko pia ni fahari kwao! Sasa we endelea na upambe tu mkimalizana nao muende na kwa Wahandzabe mkawafurushe nao maana hii ni awamu ya kumnyanyasa mwananchi wa kawaida

Nani kakudanganya hvo....wamasai wapo pale kwa sababu Kuna watu wananufaika na uwepo wao Wala sio watalii
 
Wafugaji gani wameingilia hifadhi ya Ngorongoro, Wameingilia wakitokea wapi?
Nitajie Mkoa ambao una wakazi ambao hawakuingilia hifadhi. Huko mijini mnajenga hadi kwenye fukwe za bahari, mito na maziwa nani amewazuieni?

Hata jiji la Dar kabla lilikuwa ni poli la minazi na wanyama, lkn watu ni zaidi ya kuwa na wanyama na minazi..leo Dar imejaa majengo hakuna anaeuliza.

Hao jamii ya Wamasai wachache ndo wanaonekana tatizo kisa kuna mabwana zenu wametamanishwa mabilioni ili kuwamilikisha wachache ardhi yenye utajiri?

Punguzeni Ujinga. Hata wilaya ya Serengeti ipo kwenye hifadhi. Lkn umewekwa utaratibu wa wapi watu waishi na kufuga, na wapi ibakie shughuli za hifadhi. Ngorongoro pia ina utaratibu wake.

Hao wanahabari wawili wanaijua hifadhi ya Ngorongoro kwa ufasaha? Kwenda kutalii siku moja huku wakitumwa kubeba ajenda halifu kwa jamii ya Wamasai ndo wanajifanya wanaijua Ngorongoro kuliko Dunia unayotumia mabilioni ya pesa kulinda uasili wa eneo hilo?

Mwenyezi Mungu hakuiumba Dunia na watu wake ili waishi wakiwa chini ya Twiga na Pundamilia. Aliumba wanadamu wakaitawale Dunia na kila kilichomo.

Kuna Nchi hazina Wanyama wala hifadhi zenu, lkn zinavutia watalii kuliko nyie wenye kila aina ya vivutio. Kuamini Utalii ndio njia pekee ya kuleta mapato ni ujinga na udumavu wa akili.

Sasa hivi uchumi wa Dunia unajengwa kupitia technology, pambaneni huko, wala hamtowaona Wamasai kuwa ni kikwazo.

Hakuna Nchi Duniani iliyo tajiri kiuchumi sababu ya mbuga za wanyama.

Mnakwenda shuleni lkn hamuelimiki.

Mnataka kuwaondoa Wamasai kwenye asilia yao ili muwalete Waarabu wajenge mahoteli, mkiamini mahoteli hayawezi kufukuza Wanyama.

Wamasai ni Watanzania kama wale waliopo Dodoma ama Zanzibar. Kama hawana maji safi, ni jukumu la Serikali kuwapelekea maji safi, sio kuwabeza utu wao.

Kama watoto wao wanaliwa na Simba, wekeni mazingira rafiki kwa usalama wa watoto wao. Mijini hakuna Simba, lkn watu wanafia vituo vya polisi, nao wahamishwe?

Kama watoto wao hawaendi shule, wapelekeeni shule karibu yao mbona magari ya watalii wenu yanakwenda kwao kila siku na mnapata mabilioni?

Kati ya hao Wamasai na magari yenu ya watalii kipi kinaweza kufukuza Wanyama waliopo?
Wanaowaona Wamasai kuwa ni tatizo ni watu wenye uchu wa utajiri huku wakiumiza wenzao.

Hawana tofauti na mashetani.
 
4.kipi ni muhimu kati ya binadamu na wanyama
Hili linaingia kwenye namba 3. Unapoamua hatima ya hifadhi na wakazi wake lazima upime jambo gani litakuwa na manufaa kwa pande zote. Sio zero sum game, si lazima mmoja apoteze ili mwingine apate.
 
Hivi karibuni kumezuka mijadala mingi juu ya uwepo wa zaidi ya watu zaidi ya laki Moja kuishi hifadhi ya Ngorongoro kuwa ni njia Moja wapo ya KUVUTIA UTALII ni ujinga na upuuzi usio vumilika hata kidogo.

Tumeshudia Waandishi wa habari Maulid Kitenge na Oscar Oscar Mzee wa Kaliua wakiwa wanaripoti kutoka Hifadhi ya Ngorongoro na kueleza ualisia unaoendelea hapo Hifadhini.

Kumejitokeza kundi la wajinga flani kwa maslahi yao binafsi bila kuangalia hali ilivyo wameanza kampeni ya kuwashambulia waandishi hao.

Tuangalie uhalisia, taarifa ni kuwa kuna jamii ya watu wachache ni wanufaika na shida za watu walio wengi maskini, huko Ngorongoro Tuendako watoto wanakufa, hakuna barabara, hakuna huduma za kijamii nk ndo maana MECIRA tunasema hatua za haraka zichukuliwe kuondoa hali ya hatari zaidi baadaye na sasa.

Shida inayoonekana hapo ni wafugaji kuingilia hifadhi, kwa ajili ya malisho na Taifa linaweza kukosa watalii kwani watakuwa wanafika kwenye hifadhi badala ya kuona pundamilia, au Twiga wanakutana na Ng'ombe na Taifa kukosa mapato yatokanayo na utalii.

Lakini pia kizazi Cha Sasa kitaona mazingira rafiki kwa malisho ni kwenye hifadhi kwani kitaona hakuna katazo lolote, kama wanahabari tunapaswa kuishauri serikali njia sahihi za kuepukana na hili tatizo, kazi iendelee.

Hakika mapendekezo ya Kitenge na Oscar* yanatakiwa kuchukuliwa haraka hatua za makusudi kwa ajili ya kuokoa kizazi ambacho kinaishi maisha hatarishi, na kuokoa hifadhi kuondokana na hatari ya kuwa jangwa.

View attachment 2111203

View attachment 2111204

View attachment 2111205
Hii nchi haina watafiti hadi uchukue mapendekezo ya waandishi makanjanja waliolipwa kufanya ziara siku mbili na kupigapiga picha kufanya maamuzi ya kuwaondoa masai ngorongoro? Unataka kuua cultural heritage ya kabila la masai ambao kwao kukaa kwenye mazingira yao asili ndani ya ngorongoro ni kivutio cha ziada kwenye utalii? Hakuna namna ya kuthibiti ongezeko la shughuli za binadamu ngorongoro badala ya kukimbilia kuondoa hao masai?................unaweza kuwaona wanyama pekee Serengeti, lakini ngorongoro ni pa kipekee ambapo binadamu na mifugo yao wana co-exist na wanyama pori kwa miaka mingi sasa, na hicho ni kivutio kikubwa cha utalii unaotuingizia pato la taifa........
 
Nimelikuta andiko hili sehemu kutoka kwa Joseph Yona, naamini litakuwa na kitu. Tulisome pamoja ndugu zangu...

Maulid Kitenge na Oscar Oscar Mzee wa Kaliua wasishambuliwe, bali tuangalie uhalisia, taarifa ni kuwa kuna jamii ya watu wachache ni wanufaika na shida za watu walio wengi maskini, huko Ngorongoro tuendako watoto wanakufa, hakuna barabara, hakuna huduma za kijamii nk ndo maana MECIRA tunasema hatua za haraka zichukuliwe kuondoa hali ya hatari zaidi baadaye na sasa.

Shida inayoonekana hapo ni wafugaji kuingilia hifadhi, kwa ajili ya malisho na Taifa linaweza kukosa watalii kwani watakuwa wanafika kwenye hifadhi badala ya kuona pundamilia, au Twiga wanakutana na Ng'ombe na Taifa kukosa mapato yatokanayo na utalii, lakini pia kizazi cha sasa kitaona mazingira rafiki kwa malisho ni kwenye hifadhi kwani kitaona hakuna katazo lolote kama wanahabari tunapaswa kuishauri serikali njia sahihi za kuepukana na hili tatizo, kazi iendelee.

Hakika mapendekezo ya Kitenge na Oscar yanatakiwa kuchukuliwa haraka hatua za makusudi kwa ajili ya kuokoa kizazi ambacho kinaishi maisha hatarishi, na kuokoa hifadhi kuondokana na hatari ya kuwa jangwa.
 
Hivi karibuni kumezuka mijadala mingi juu ya uwepo wa zaidi ya watu zaidi ya laki Moja kuishi hifadhi ya Ngorongoro kuwa ni njia Moja wapo ya KUVUTIA UTALII ni ujinga na upuuzi usio vumilika hata kidogo.

Tumeshudia Waandishi wa habari Maulid Kitenge na Oscar Oscar Mzee wa Kaliua wakiwa wanaripoti kutoka Hifadhi ya Ngorongoro na kueleza ualisia unaoendelea hapo Hifadhini.

Kumejitokeza kundi la wajinga flani kwa maslahi yao binafsi bila kuangalia hali ilivyo wameanza kampeni ya kuwashambulia waandishi hao.

Tuangalie uhalisia, taarifa ni kuwa kuna jamii ya watu wachache ni wanufaika na shida za watu walio wengi maskini, huko Ngorongoro Tuendako watoto wanakufa, hakuna barabara, hakuna huduma za kijamii nk ndo maana MECIRA tunasema hatua za haraka zichukuliwe kuondoa hali ya hatari zaidi baadaye na sasa.

Shida inayoonekana hapo ni wafugaji kuingilia hifadhi, kwa ajili ya malisho na Taifa linaweza kukosa watalii kwani watakuwa wanafika kwenye hifadhi badala ya kuona pundamilia, au Twiga wanakutana na Ng'ombe na Taifa kukosa mapato yatokanayo na utalii.

Lakini pia kizazi Cha Sasa kitaona mazingira rafiki kwa malisho ni kwenye hifadhi kwani kitaona hakuna katazo lolote, kama wanahabari tunapaswa kuishauri serikali njia sahihi za kuepukana na hili tatizo, kazi iendelee.

Hakika mapendekezo ya Kitenge na Oscar* yanatakiwa kuchukuliwa haraka hatua za makusudi kwa ajili ya kuokoa kizazi ambacho kinaishi maisha hatarishi, na kuokoa hifadhi kuondokana na hatari ya kuwa jangwa.

View attachment 2111203

View attachment 2111204

View attachment 2111205
Ni mpumbavu pekee atakayepingana na bandiko lako. Uzuri limeendana na picha na nimependa uliposema mtalii badala ya kuona pundamilia atakutana na ng'ombe.

Pia ni ukweli usiopingika Masai ni tatizo maana kote wanakohamia huleta hizi fujo naona kabisa walikaa mbugani sababu it was no man's land lakini kwa sasa mwenye nayo hataki waitumie sababu ishu sio hata huduma tu Ila ni wazi kwamba malisho ya wanyama pori yapo hatarini sana .

Tuwe na huruma na vizazi vijavyo.
 
Wewe huwezi ukajua brand ya Ngorongoro imetokana na nini kwakua umezaliwa mwaka 2006.

Na sidhani hata kama umewahi kufika ngorongoro penyewe zaidi ya kuangalia clip za youtube.

Sio ajabu kukuta masai akichunga ngombe crater na simba wapo tu.

Hiyo ndio brand ya Ngorongoro crater kijana.

Ngorongoro imepata sifa kwakua mazingira yale ya porini yameruhusu kuishi pamoja kwa binadamu na wanyama , hicho ndicho kinachoifanya Ngorongoro kuwa mbuga ya kipekee, hivyo ili Mbuga iendelee kuwa na manufaa jamii ya kimasai inapaswa ibaki pale.

Jambo ambalo linatakiwa lifanyike na mamlaka ni kudhibiti ongezeko la watu.

Yaani kuwe na limited number ya watu katika eneo jambo ambalo litakua na faida kwa wanyama na sisi binadamu pia.

Lakini sio namna hii kukashifu watu na kutishia raia wengine.

Serikali itumie busara na sio kuongozwa na kauli zisizoangalia maslahi ya Taifa.

Otherwise tutawaondoa wamasai ndio lakini tutabakia na mbuga ambayo haina faida kwakua tutakua tumeiua Brand ya Ngorongoro crater.
 
Back
Top Bottom