Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 214
- 290
UTANGULIZI.
👉Kuboresha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania kunahitaji mabadiliko na maboresho kadhaa ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa haki, huru, na uwazi.
👉NEC inaweza kuongeza uaminifu na uadilifu katika mchakato wa uchaguzi na kusaidia kujenga demokrasia ya kweli nchini Tanzania.
MAWAZO BINAFSI KUHUSU MICHAKATO HII YA TUME YA UCHAGUZI.
👉Kuimarisha ushirikishwaji wa vyama vya siasa vyote vya siasa ( CCM, CHADEMA,CUF,ACT-WAZALENDO,CHAUMA,TLP,UDP na vyama vinginevyo) ,asasi za kiraia, viongozi wa dini na jumuiya za kimataifa katika mchakato wa uchaguzi. Ushirikishwaji huu unasaidia kujenga imani na kuondoa hisia za ubaguzi au upendeleo,kuanzia kwenye mapendekezo ya wagombea ,michujo yao ,kampeni na kutangaza matokeo ,ikibidi na nyakati za kuapishwa washindi kushika hatamu za uongozi.
NB: picha kwa hisani ya mtandao
👉Kutumia teknolojia ya kisasa katika uandikishaji wa wapiga kura na upigaji kura ili kuondoa udanganyifu na makosa ya kiufundi. Hii inajumuisha kutumia mifumo ya biometriki kuwatambua wapiga kura na kutangaza matokeo kwa njia ya kielektroniki.
Nini kifanyike hapa Kwenye Biometric.
1. Kitambulisho cha Alama za Vidole.Inahakikisha kila mpiga kura anatambuliwa kwa alama za vidole, kuzuia uandikishaji mara mbili.
2. Kutumia mashine za kielektroniki ambazo zitapunguza makosa ya kibinadamu na zitatoa matokeo haraka na kwa usahihi.
3. Kupiga Kura kwa Njia ya Mtandao. Kuruhusu wapiga kura walio nje ya vituo vya kupigia kura, kama vile walioko nje ya nchi, walioko mbali na vutuo vyao walivyojiandikishia ili waweze kupiga kura kupitia mtandao (online).
👉Kuwa na tume huru ya uchaguzi isiyoingiliwa na yeyote mwenye mamlaka ni muhimu sana kwa kuhakikisha uchaguzi huru, wa haki, na wenye uwazi.
Tunaweza kuzingatia yafuatayo,
1. Kuweka utaratibu wa uteuzi wa wajumbe wa tume ya uchaguzi,ambao wako huru na wazi hawana maagizo ya yeyote. Wajumbe wanaweza kuteuliwa kupitia kamati maalum inayojumuisha wawakilishi kutoka vyama vya siasa, asasi za kiraia, na taasisi za kitaaluma. Uteuzi unaweza kuthibitishwa na Bunge ili kuhakikisha kuwa wajumbe wanapata ridhaa ya uwakilishi mpana wa wananchi.
2. Wajumbe wasiwe na uhusiano wa karibu na vyama vya siasa au serikali ili kuepusha mgongano wa maslahi.Pia suala la uzoefu linapaswa kuzingatiwa.
3. Tume inapaswa kuwa na bajeti inayojitegemea na isiyoweza kuingiliwa na serikali. Bajeti hii inaweza kupitishwa na Bunge na kuwekwa kwenye mfuko maalumu utaosimamiwa na tume yenyewe. Isitegemee ufadhari wala hisani kutoka popote wala Kwa yeyote.
4. KUTUNGA sheria mpya za nchi juu ya masuala mazima ya uchaguzi Kwa kuweka bayana wajibu na mamlaka ya tume pamoja na kinga dhidi ya kuingiliwa na yeyote au vyevyote vile.
👉Kuruhusu matokeo yote ya uchaguzi wa Rais, Mbunge, na Diwani kupingwa mahakamani ni hatua muhimu katika kuhakikisha uhalisia na uwazi wa mchakato wa uchaguzi. Sheria za uchaguzi zinapaswa kufanyiwa marekebisho ili kuweka bayana haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais, Mbunge, na Diwani. Hii inaongeza Imani Kwa Umma pamoja na Uhuru na uwazi wa mchakato.
👉Sheria za uchaguzi zinapaswa kufanyiwa marekebisho ili kuruhusu wagombea binafsi kushiriki katika uchaguzi. Hii inajumuisha kuondoa vikwazo vyote vinavyohitaji wagombea kuwa wanachama wa chama cha siasa.
BINAFSI KUHUSU HILI
-Wagombea binafsi wanaweza kuwakilisha maslahi maalum au vikundi maalum vya kijamii ambavyo havijawakilishwa vizuri na vyama vya siasa. Hii itasaidia kuleta sauti tofauti katika mijadala ya kisiasa na kufanya maamuzi ya sera kuwa jumuishi zaidi.
👉Kuondoa wabunge wa viti maalum ni muhimu kuelekea kwenye mfumo wa uwakilishi unaowajibika zaidi na unaoweka msisitizo kwa ushindani huru na uwazi katika uchaguzi. Hii itaweza kusaidia kujenga demokrasia inayojali zaidi mahitaji na maoni ya wananchi wote.
-Marekebisho ya katiba na sheria za uchaguzi yanaweza kufanyika ili kuondoa viti maalum na kuweka msisitizo zaidi kwa uchaguzi wa majimboni pekee.
TUJIKOSOE.
👉Kupita bila kupingwa katika uchaguzi hasa Kwa nafasi za udiwani na Ubunge ni suala linalozua mjadala na linapunguza ushindani na uwazi katika mchakato wa kidemokrasia. Katika zama hizi ambapo watu wengi ni wasomi na wana uelewa mzuri wa masuala ya kisiasa, ni muhimu kuhakikisha kuwa kila nafasi ya uongozi inapatikana kwa njia ya ushindani wa haki.
👉Kuweka sifa za kigezo cha elimu kwa wabunge ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa viongozi wanakuwa na uwezo wa kuelewa na kushughulikia masuala ya kitaifa kwa ufanisi. Kuwa na kiwango cha chini cha elimu ya kidato cha nne na kuendelea, pamoja na kumiliki fani fulani ya kitaaluma, kunaweza kusaidia katika kuboresha ubora wa uongozi na utendaji wa bunge,isibaki Ile ya kujua kusoma na kuandika 😃,ni huzuni.
👉Kuwapa wananchi haki ya kupitisha uamuzi wa kumwondoa mbunge au diwani wao kabla ya muda wake wa miaka mitano kuisha, ikiwa hawaridhishwi na utendaji wake, ni muhimu kuimarisha uwajibikaji na demokrasia. Hii itaweza kufanywa kwa kuweka utaratibu wa kura ya kutokuwa na imani.
👉Kuwahimiza wapiga kura kuwa na uwezo wa kusoma na kuandika ni hatua muhimu katika kuimarisha demokrasia na kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unakuwa na matokeo yenye tija kwa maendeleo ya taifa.
MWISHO:
👉MAWAZO ya kuhakikisha uhuru wa tume ya uchaguzi ni muhimu sana katika kudumisha demokrasia na kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unakuwa wa haki, uwazi, na wenye uhalisia. Ingawa imani katika mamlaka ya juu ni muhimu kwa watu wengi, ni muhimu pia kuhakikisha kuwa taasisi za serikali zina uhuru wa kufanya kazi zao kwa uwazi na bila kuingiliwa na upande wowote.
~mwanazuoni.