Mabinti ndio sababu ya vijana wengi kusema uongo

Kwann Wadada mnapendaga kuuliza mwanaume anafanya kazi gani?? Yaani ile umemwona tu unamwuliza anafanya kazi gani..

Ni kwasababu baadhi yetu mnaontuona tuna sura mbaya ivo mnaona hatuna cha kuwapa zaidi ya hela? Leejay49
Yani hii tabia inabidi niache,, sometimes tunauliza tu sio kwa nia mbaya jamani😃😃😃
 
Kijana wa kiume anapokutana na binti kwa mara ya kwanza, swali la kwanza ambalo binti huuliza ni:
"Unafanya kazi wapi?" Jamaa akisema anafanya kazi kwenye kampuni ya mafuta, binti huyo atakubali haraka kudate na kijana huyo.

Lakini kama kijana huyo akisema yeye ni saidia fundi kwenye shughuli za ujenzi, binti huyo atakunja sura yake na baada ya wiki moja atakata mawasiliano.

Tusiwalaumu watu wanaosema uongo.
Mabinti ndio sababu ya vijana wengi kusema uongo.

Kijana atamdanganya binti kwamba anafanya kazi benki ili tu kumfanya binti huyo akubali kuwa nae. Lakini hii ni mbaya sana..

Mabinti, usiingie kwenye mahusiano na mtu kutokana na kazi yake. Usianzishe mahusiano na kijana kwa sababu anafanya kazi kwenye kampuni kubwa na usimkatae mwanaume kwa sababu hafanyi kazi kwenye kampuni kubwa.

Aina ya kazi yake haijalishi. Kilicho muhimu ni tabia ya mtu mwenye upendo na kujali na maono.

Unaweza kudate na mtu wa benki na akawa bahili na anaweza asikuhudumie vizuri. Lakini kijana aliye na kazi duni anaweza kukutunza ipasavyo kwa mshahara wake mdogo zaidi ya yule wa benki.

Kwa hiyo sio suala la kazi, ni suala la upendo, kujali, kuthamini na kujitoa.
Hii ni sahihi kabisa mkuu🤝
 
Shemeji/wifi yenu nilimpata nikiwa nashusha matofai kwenye site ya babaake alikuja kuhesabu yaani kuhakiki mzigo uloshushwa, alifanya kosa kubwa sana kunipa namba zake, swali la kuulizwa kazi yangu halikuwepo sababu alishaifaham na kuiona live nikiifanya, mwaka jana nilimwagiza akahakiki matofali yanayoshushwa kwenye site yetu over:
 
Kama una mpango wa kuhit n run danganya kuwa wewe ni mshauri mkuu wa bakhresa kumbe ni fundi tiles ili upate mbususu kirahisi usepe.

Kama unatafuta mke danganya kuwa wewe ni fundi tiles kumbe ni mshauri mkuu wa Bakhresa na mwanamke atakayekukubali bila kujali umasikini wako huyo ndie mke.

Mnawadanganya ndio mana ndoa zenu zinaishia na kuchomana na magunia ya mikaa sbb misingi ya ndoa zenu haijajengwa kwa UPENDO bali UONGO na TAMAA za mali.



Ciao
 
Mwanaume mwenzangu usije ukamwambia ukweli Mwanamke.
Wanawake 99% wamejaa na tamaa za mali,mudanganye OSHA lungu-chapa lapa.
Kama unatafuta kwa ajili ya kuoa mdanganye pia,kama una kipato cha 1M mwambie una 400K kama 2M mwambie una 800K.
 
Shemeji/wifi yenu nilimpata nikiwa nashusha matofai kwenye site ya babaake alikuja kuhesabu yaani kuhakiki mzigo uloshushwa, alifanya kosa kubwa sana kunipa namba zake, swali la kuulizwa kazi yangu halikuwepo sababu alishaifaham na kuiona live nikiifanya, mwaka jana nilimwagiza akahakiki matofali yanayoshushwa kwenye site yetu over:
Ilikuwa unashusha au ilikuwa unasimamia washushaji?
Kuna vitu 2 hapo,labda aliona wewe ndio meneja unasimamia washushaji.
 
Kuna. Mmoja juzi kaja ofisini kadanganywa wajeda wanapewa kilo3 kama allowance ya BIA. TULICHEKA ila yeye aliamini.
 
Back
Top Bottom