Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,329
- 9,643
Kijana wa kiume anapokutana na binti kwa mara ya kwanza, swali la kwanza ambalo binti huuliza ni:
"Unafanya kazi wapi?" Jamaa akisema anafanya kazi kwenye kampuni ya mafuta, binti huyo atakubali haraka kudate na kijana huyo.
Lakini kama kijana huyo akisema yeye ni saidia fundi kwenye shughuli za ujenzi, binti huyo atakunja sura yake na baada ya wiki moja atakata mawasiliano.
Tusiwalaumu watu wanaosema uongo.
Mabinti ndio sababu ya vijana wengi kusema uongo.
Kijana atamdanganya binti kwamba anafanya kazi benki ili tu kumfanya binti huyo akubali kuwa nae. Lakini hii ni mbaya sana..
Mabinti, usiingie kwenye mahusiano na mtu kutokana na kazi yake. Usianzishe mahusiano na kijana kwa sababu anafanya kazi kwenye kampuni kubwa na usimkatae mwanaume kwa sababu hafanyi kazi kwenye kampuni kubwa.
Aina ya kazi yake haijalishi. Kilicho muhimu ni tabia ya mtu mwenye upendo na kujali na maono.
Unaweza kudate na mtu wa benki na akawa bahili na anaweza asikuhudumie vizuri. Lakini kijana aliye na kazi duni anaweza kukutunza ipasavyo kwa mshahara wake mdogo zaidi ya yule wa benki.
Kwa hiyo sio suala la kazi, ni suala la upendo, kujali, kuthamini na kujitoa.