Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa?

Msingi wa maendeleo ni demokrasia:

1. Itatupa mawazo bora kabisa
2. Itatupa mawazo bora kabisa.
3. Itatupa uamuzi bora zaidi.
Jee demokrasia ndiyo msingi wa kufikiri kwetu??
Mapambano yanataka watu wanaohesabika hata kama ni wachache siyo maneno matupu.
Hao watu wachache wanapatikana kwa kutumia vigezo gani??
Tuwekeze kwenye mashirikiano si mafarakano.
Kila ushirikiano si unahitaji kuwa na kanuni za ushirikiano huo. Nini kinatuongoza kuingia kwenye huo ushirikiano na malengo yake ni nini?
Anayejipa mamlaka ya kutilia mashaka nani huyo? Tuachane na ramli chonganishi hizi ambazo aghalabu ni kwa manufaa ya CCM.
Shaka ni sehemu inayotumika pia kujenga tahadhari chanya.
Mengine ni visingizio tu ndugu.
Kwa miaka karibu ya 20 Sasa nimekuwa kwenye harakati hizi, hii ni hali halisi na wala si visingizio.
 
Bwana Pascali, sheria wala Katiba haviwezi kumsaidia Mtanzania..

Vipo bado vipengele vya sheria na katiba ambavyo vikifuata na kuheshimiwa bado nchi inaweza kabisa kujikomboa na kusonga mbele.

Tanzania inahitaji series of good dictators wenye uzalendo na ndoto yakuiona kesho bora na kuacha heshima nyuma ambao hawatasita kuua na kupoteza wajinga wengie wanaokwamisha kesho ya Tanzania.
Hawa good dictators wenye maono hawaji kupitia mifumo hii ya sheria na katiba bali huzuka kupitia chances zinazojitokeza kwenye mivurugano ya kisiasa.
 
Ngoja brazaj nitoe kidogo mawazo yangu kwa mfano kuhusu njia mojawapo shinikizi, njia ya maandamano.

Ni vizuri tuwe na mjadala mmoja. Ukiandika mingi inakuwa shida. Unajua tena wengine hatuna ma typists. Tukiwa twaenda fupi fupi kama hizi itakuwa vyema zaidi.

Kuhusiana na maandamano niseme kuwa ndiyo lugha pekee anayoielewa CCM. Hii tutake au tusitake.

Kuna watu wanakurupuka tu kusema tufanye maandamano. Maandamano ni sanaa tena ni sayansi kwenye kuyaandaa kwake.

Mkuu hawakurupuki. Nani alijua HAMAS wataingia Israeli wachukue maeneo?

Kulikoni kutokuwaacha waandae? Kwani nani analazimishwa?

Ila nikwambie watu wamechoka na inawezekana. Zingatia wala haihitaji watu wengi na hasa wenye agenda binafsi.

Watu 100 tu kwenye wilaya Moja hawako na magereza ya kuwaweka.

Huwezi kuwa na maandamano yatakayofanikiwa bila ya kuyapanga kisayansi na kuyahamasisha kisanaa.

Hizi ndiyo zile hadithi CCM na vibaraka wao kwa kujua au kutokujua wangependa tuamini.

Anayesema akianza na 10 namwelewa sana ukizingatia hata dunia inaangalia.
 
Kuhusiana na maandamano niseme kuwa ndiyo lugha pekee anayoielewa CCM. Hii tutake au tusitake.
Hakuna anayebisha. Lakini ili yafanikiwe inabidi yaratibishwe. Huo ndiyo ukweli.
Mkuu hawakurupuki. Nani alijua HAMAS wataingia Israeli wachukue maeneo?
Unataka kusema HAMAS waliamka tu asubuhi bila ya mpangilio na kuanza kuvamia maeneo wanayoishi waisrael?
Kulikoni kutokuwaacha waandae? Kwani nani analazimishwa.
Sawa.
Ila nikwambie watu wamechoka na inawezekana. Zingatia wala haihitaji watu wengi na hasa wenye agenda binafsi.
Watu wamechoka tangu 1995, Lakini wanafanya nini kuonesha kuwa wamechoka??
Watu 100 tu kwenye wilaya Moja hawako na magereza ya kuwaweka.
Hao watu 100 kwenye kila wilaya wanapatikanaje??
Hizi ndiyo zile hadithi CCM na vibaraka wao kwa kujua au kutokujua wangependa tuamini.
Siyo hadithi bali ni sayansi ya Siasa. Maandamano ni lazima yaratibiwe.
Anayesema akianza na 10 namwelewa sana ukizingatia hata dunia inaangalia.
Mwanzo wa mwisho huonekana kwa kuwa na uvivu wa kupanga.
 
Acha porojo zako. Hakuna "Good dictators"

Na hakuna mahali madikteta wamewahi kuleta maendeleo kwa wananchi wao.

hahahaha, umenifurahisha sana.

nionyeshe wapi Democrasia imewahi kuleta maendeleo.

Udikteta umeleta maendeleo China, Russia, Italy, Germany, Singapore, Malyasia, UAE, Saudia Arabia, Misri, Rwanda nk.

Hata huko unakoona leo kumeendelea na watu wanapractise democracy, sijuia katiba na sheria walianza kwanza kuteswa, kuumizwa, kushurutishwa nk. walipokaa sawa ndio hiyo democracy ikawa introduced.
 
Wanabodi
Hii ni makala ya Jumapili ya leo.
Hili ni bandiko mwendelezo wa bandiko hili Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
View attachment 2775208

Kufanya mabadiliko yoyote ya sheria iliyotokana na vifungu vya katiba, bila ya kufanya kwanza mabadiliko ya katiba, no sawa na kula bila kunawa!. Je Watanzania tuna njaa sana, na tuna haraka sana na uchaguzi ujao, hadi tukimbilie kula bila kunawa?​

Dini zote zinatufunza kuwa na shukrani kwa yote, hivyo kikao cha Bunge kijacho, kitapokea miswada kadhaa ya mabadiliko ya sheria za Uchaguzi, Tume ya uchaguzi na Ofisi ya Msajili wa vyama, japo bado sijajua ni sheria zipi zitafanyiwa mabadiliko, hivyo hatua ya kwanza ni kushukuru kwa mabadiliko hayo.

Lakini kufanya mabadiliko ya sheria zilizotokana na katiba, bila kutanguliwa na mabadiliko ya katiba, ni superficial changes!.

Kwa muda mrefu, tumepigia sana sheria kandamizi za uchaguzi na sheria batili zilizochomelewa kiubatili ndani ya katiba yetu!, maadam sasa something is going to be done, let's be appreciative for whatever is going to be done regardless how little it is.

Hapa ni baadhi ya sheria hizo
  1. Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?
  2. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
  3. Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
  4. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
  5. Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza?
  6. Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
  7. Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
  8. Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
  9. Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
  10. Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
  11. Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?
  12. Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa
  13. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  14. Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!

Paskali
Ukibanwa na njaa hutasubiria kunawa vinginevyo utakuta msosi umeisha.
 
Jee demokrasia ndiyo msingi wa kufikiri kwetu??

Demokrasia Ina maana kushawishiana kwa hoja na kuchukua yaliyo bora. Ni kama tunavyo jadili hapa kistaarabu, nadhani.

Mfano: tuta share mawazo na kushindana kwa hoja, bora zaidi zitatamalaki.

"Ninaamini kama ilivyo hapa, tunapiga hatua."

Hao watu wachache wanapatikana kwa kutumia vigezo gani??

Mkuu, watu wapo. Kama wewe au yule hamwezi wala si shida. Si mnakaa pembeni tu?

Ukombozi una gharama zake. Inafahamika wengine wanataka kuvuna bila Kupanda. Wala si shida. Ukombozi unataka sacrifice. Mbona kina Biko, Mahlangu wanakumbukwa hadi leo?

"Wala haina shida. Nikutoe shaka, waliodhamiria wapo."

Kila ushirikiano si unahitaji kuwa na kanuni za ushirikiano huo. Nini kinatuongoza kuingia kwenye huo ushirikiano na malengo yake ni nini?

Kanuni ni kutafuta maslahi binafsi tu, ndugu. Tutahangaika na kanuni badala ya kutafuta katiba mpya? Kanuni ipi ya muhimu hiyo yenye kuiweka agenda ya katiba mpya rehani?

"Kumbuka Chris Hani (PAC) alikuwa mkuu wa majeshi (ANC). Vyama tofauti, sera tofauti adui mkuu mmoja."

Sisi tumerogwa na nani?

Shaka ni sehemu inayotumika pia kujenga tahadhari chanya.

Shaka inayotufanya tusielekee kupata katiba mpya, haina maana yoyote. Tambua CCM wangependa tuishi na shaka hizo milele ikiwezekana.

Kwa miaka karibu ya 20 Sasa nimekuwa kwenye harakati hizi, hii ni hali halisi na wala si visingizio.

Mkuu hata tukae miaka 100 kwenye harakati hIzi hakumaanishi tumepata katiba mpya.

Kwanini hatujapata? Sababu ni kuwa:

"Hatujaweza kuondoka kwenda Tahrir, mwisho wa matatizo:"

Tunataka haki? Hatutaki tozo? Tukutane Tahrir

Wasiokuwa tayari kwenda Tahrir si wanakaa pembeni tu.

"Kwani tatizo liko wapi?"
 
Hakuna anayebisha. Lakini ili yafanikiwe inabidi yaratibishwe. Huo ndiyo ukweli.

Tuwekeni siasa pembeni. Maneno matupu hayavunji mfupa.

Asiyeweza akae pembeni. Watu wanaoamini watawafikisha watu Tahrir wapewe usukani. Huko ndiko uliko mwisho wa matatizo.

Kama huamini hivyo kaa pembeni. Mtu kwenye usukani atapimwa Kwa deliverables.

Uko kwenye usukani, njia kwenda Tahrir huna au huijui wakati unajua huko ndiko pekee kwenye ufumbuzi? Kumbe upo unafanya nini?

Unataka kusema HAMAS waliamka tu asubuhi bila ya mpangilio na kuanza kuvamia maeneo wanayoishi waisrael?

Mengine yote sasa hapo ni history. Ila ukweli wa mambo wenye kujua namna ya kufanya walishika usukani na wamefanya walichoahidi watafanya.

Tulipo kila siku tunasikia lawama kwa watu kana kwamba kuna siku watu wataamka asubuhi na kuelekea Tahrir.

Vyema, hili limeisha.

Watu wamechoka tangu 1995, Lakini wanafanya nini kuonesha kuwa wamechoka??

Watu wafanye nini bila kuongozwa? Si ndiyo ya HAMAS kwenda Israel? Unadhani wamekwenda baada ya kuamka asubuhi tu bila kuongozwa?

Hao watu 100 kwenye kila wilaya wanapatikanaje??

Tena wala si Kila wilaya, nilikuwa bado ningali nina edit, parejee pale.

Hata hivyo 100 kila wilaya wapo.

"Kumbe wale wanachama 15m+ tunaojinasibu nao here and there, ni wa nini kama hata 100 tu wa kujaza magereza za wilaya moja tu nchi nzima hawapo?

Siyo hadithi bali ni sayansi ya Siasa. Maandamano ni lazima yaratibiwe.

Mwanzo wa mwisho huonekana kwa kuwa na uvivu wa kupanga.

Ninakazia:

Tuweke maneno pembeni. Huwezi kutupeleka Tahrir, tupishe wagombee watu kwa agenda ya kutupeleka Tahrir. Tunawapima kwa deliverables.

"Tatizo liko wapi?"
 
Public space imemezwa na mambo ya ajabu sana. Takwimu zinaonesha uwepo wa Asasi za kiraia "Civil Societies" takribani 8000 ambazo zingewajibika kikamilifu suala la kiongozi kutamka kuwa wananchi hawaelewi Katiba nini nini lisingepata nafasi kabisa.

Leo wananchi tunatakiwa kupewa elimu ya Katiba kwa miaka mitatu huku Asasi lukuki za Kiraia zikizubaa na kuachia wanasiasa kusema chochote wanachotaka.

Kuna ombwe kubwa kwenye "Public space katika Taifa letu kuliko kikundi chochote kile. Tabia za kujipendekeza, uchawa inazidi na sababu moja wapo huenda ombwe hili la nafasi ya umma. Watu wanajipendekeza wanapopaona na panapoonekana kwa haraka ni uwanja wa wanasiasa.
 
....Dini zote zinatufunza kuwa na shukrani kwa yote,

.......maadam sasa something is going to be done, let's be appreciative for whatever is going to be done regardless how little it is.Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?
Beyond ridiculous.

Tushukuru kwa kila jambo kama dini zinavyotufundisha, hata jambo ambalo bado halijafanyika tushukuru tu ile ahadi, na hata kama hawaja specify watafanya nini tunapaswa kushukuru kuambiwa tutafanya "something."

Hizi ndio ukisikia indoctrination, kufubazwa akili, kwa watu wa jamii za kijima. Raia wamepikwa wakatokota kuamini kwamba lolote linalofanywa na serikali ni hisani, na ni la kushukuru.

Na hizi ndio the most eminent think tank editorials zinazotokea kwenye magazeti yetu ya Jumapili. Ndio zitutoe kwenye u third world hizi Pascal Mayalla whitewashed minds hizi! Unawezaje kudai maendeleo kama unaamini kazi ya serikali ni hisani ????
 
Mimi ninachofahamu Serikali ya CCM inafanya tu maigizo na kuwachezea shere wapinzani, na mwisho wa siku hakuna kitakachopatikana.

Na hii yote ni kwa sababu haiko tayari kuruhusu uwepo wa Uchaguzi huru na wa haki, uwepo wa Katiba yenye maslahi mapana kwa wananchi badala ya wao wenyewe na chama chao, nk.

Kiufupi CCM na Serikali yake hawana nia njema ya kuifanya hii nchi kupiga hatua katika nyanja za kisiasa na kiuchumi kutokana na ubinafsi wao uliopitiliza.
Naunga mkono hoja.

Ccm ni mabingwa wa ulaghai na sanaa za kisiasa.
 
Wanabodi
Hii ni makala ya Jumapili ya leo.
Hili ni bandiko mwendelezo wa bandiko hili Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
View attachment 2775208

Kufanya mabadiliko yoyote ya sheria iliyotokana na vifungu vya katiba, bila ya kufanya kwanza mabadiliko ya katiba, ni sawa na kula bila kunawa!. Je Watanzania tuna njaa sana, na tuna haraka sana na uchaguzi ujao, hadi tukimbilie kula bila kunawa?​

Paskali
Hakuna mwana CCM hata mmoja anayethubutu kudai Tume Huru ya Uchaguzi.
Wewe Paskali huwezi kuthubutu kudai Tume Huru ya Uchaguzi, hususan kwenye 'forum' za CCM.
Duh...!, Mkuu fundimchundo , karibu bandiko hili, jee hapa ninadai nini?.
P
 
Wanabodi
Hii ni makala ya Jumapili ya leo.
Hili ni bandiko mwendelezo wa bandiko hili Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
View attachment 2775208

Kufanya mabadiliko yoyote ya sheria iliyotokana na vifungu vya katiba, bila ya kufanya kwanza mabadiliko ya katiba, ni sawa na kula bila kunawa!. Je Watanzania tuna njaa sana, na tuna haraka sana na uchaguzi ujao, hadi tukimbilie kula bila kunawa?​

Dini zote zinatufunza kuwa na shukrani kwa yote, hivyo kikao cha Bunge kijacho, kitapokea miswada kadhaa ya mabadiliko ya sheria za Uchaguzi, Tume ya uchaguzi na Ofisi ya Msajili wa vyama, japo bado sijajua ni sheria zipi zitafanyiwa mabadiliko, hivyo hatua ya kwanza ni kushukuru kwa mabadiliko hayo.

Lakini kufanya mabadiliko ya sheria zilizotokana na katiba, bila kutanguliwa na mabadiliko ya katiba, ni superficial changes!.

Kwa muda mrefu, tumepigia sana sheria kandamizi za uchaguzi na sheria batili zilizochomelewa kiubatili ndani ya katiba yetu!, maadam sasa something is going to be done, let's be appreciative for whatever is going to be done regardless how little it is.

Hapa ni baadhi ya sheria hizo
  1. Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?
  2. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
  3. Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
  4. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
  5. Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza?
  6. Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
  7. Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
  8. Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
  9. Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
  10. Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
  11. Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?
  12. Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa
  13. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  14. Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!

Paskali
Kunawa au kuto kunawa hakuna hoja yoyote tatizo lako mleta uzi ni akili zako ndiyo maana umeshindwa kugundua kuwa chakula kilichopo mezani ni kinyesi sasa kunawa ili ule kinyesi kuna mantiki gani .....kila siku nakufundisha kuwa SHERIA NA HAKI NI VITU VIWILI TOFAUTI.
 
Kufanya mabadiliko yoyote ya sheria iliyotokana na vifungu vya katiba, bila ya kufanya kwanza mabadiliko ya katiba, ni sawa na kula bila kunawa!. Je Watanzania tuna njaa sana, na tuna haraka sana na uchaguzi ujao, hadi tukimbilie kula bila kunawa?
Paskali
Hii ni zawadi yangu kwa Birthday ya Mama leo, nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.

Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
 
Back
Top Bottom