Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa?

Lakini kufanya mabadiliko ya sheria zilizotokana na katiba, bila kutanguliwa na mabadiliko ya katiba, ni superficial changes
Kweni kufanya kwanza marekebisho madogo ya Katiba ya 77 kunahitaji Bilioni ngapi na Miaka mingapi?.

Hata tukisubiri baada ya Uchaguzi kama Watawala hawana dhamira ya dhati ni kupoteza muda tu.

Hakuna political will huko Green Snakes
 
Kumkumbusha hilo CCM ni sawa na Mimi hapa kukumbusha wewe kuwa:

"CCM inajifanya kama vile hakujawahi kuwapo kwa mchakato wa kupata Katiba mpya, wakati siyo kweli."

Unadhani wanahitaji kukumbushwa jambo wanalolijua na ambalo kwa hakika wamedhamiria kutoriridhia (kirahisi)?
Kila jambo linajadilwa kwa wakati wake. Nini Sasa kifanyike na kifanyike vipi ni mjadala mwingine kabisa.

kuchanganya hoja ni kuuparaganyisha mjadala wenyewe!!

Hoja ya Mayalla inahitaji tafakuri jadidi hasa kwenye kuwaza watu wa kuibeba hiyo dhima ya marekebisho ya Katiba kabla ya uchaguzi wa 2025.
 
Kwangu mm nikiona kitu fulani kinafanyika hua nawaza hatua 3 Miele,hii ninayoiona nimaanisha nini huko mbeleni.
Kwa mtazamo wangu ukiona kunabadiliko la jambo la kisheria kazini kwako or serikalini jua kuna jambo wanatakakulifanya na hio sheria ndio itawalinda/kinga kwao soma vzr sana hayo mabadiliko uyaelewe nakuyafanyia kazi otherwise kuna siku yatakudhuru.
In short hio ni kinga Kwa wakubwa kaka Pascal Mayalla

In other words watafanya changes if only inawafaidisha wao
 
Wanabodi
Hii ni makala ya Jumapili ya leo.
Hili ni bandiko mwendelezo wa bandiko hili Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
View attachment 2775208

Kufanya mabadiliko yoyote ya sheria iliyotokana na vifungu vya katiba, bila ya kufanya kwanza mabadiliko ya katiba, no sawa na kula bila kunawa!. Je Watanzania tuna njaa sana, na tuna haraka sana na uchaguzi ujao, hadi tukimbilie kula bila kunawa?​

Dini zote zinatufunza kuwa na shukrani kwa yote, hivyo kikao cha Bunge kijacho, kitapokea miswada kadhaa ya mabadiliko ya sheria za Uchaguzi, Tume ya uchaguzi na Ofisi ya Msajili wa vyama, japo bado sijajua ni sheria zipi zitafanyiwa mabadiliko, hivyo hatua ya kwanza ni kushukuru kwa mabadiliko hayo.

Lakini kufanya mabadiliko ya sheria zilizotokana na katiba, bila kutanguliwa na mabadiliko ya katiba, ni superficial changes!.

Kwa muda mrefu, tumepigia sana sheria kandamizi za uchaguzi na sheria batili zilizochomelewa kiubatili ndani ya katiba yetu!, maadam sasa something is going to be done, let's be appreciative for whatever is going to be done regardless how little it is.

Hapa ni baadhi ya sheria hizo
  1. Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?
  2. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
  3. Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
  4. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
  5. Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza?
  6. Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
  7. Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
  8. Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
  9. Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
  10. Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
  11. Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?
  12. Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa
  13. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  14. Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!

Paskali

Uondoe unafiki wako, chawa wahedi.
 
Ndeeeeeefuuuuu! Ukifika mwisho unajikuta yale uliyoaanza nayo yote yamefutwa hapo katikati, a maze of contradictions. Mgombea binafsi anabebweaaaa halafu katikati anatupwa pale inspokataza udikteta, I mean Rais binafsi atadhibitiwa na nani? Inakuja dhana ya kuwa lengo la Katiba ni haki na maendeleo, sawa, gafula unakuja ule ugoro wa TLS eti bandari isiendelezwe. Hamna kitu hapa, Ndg Njaa nadhani alikuwa anawahi deadline ya article kabla gazeti kwenda kwa Printer.
 
Kila jambo linajadilwa kwa wakati wake. Nini Sasa kifanyike na kifanyike vipi ni mjadala mwingine kabisa.

kuchanganya hoja ni kuuparaganyisha mjadala wenyewe!!

Hoja ya Mayalla inahitaji tafakuri jadidi hasa kwenye kuwaza watu wa kuibeba hiyo dhima ya marekebisho ya Katiba kabla ya uchaguzi wa 2025.

Mjadala huu si mpya. Ni mwendelezo wa mijadala ile ile na kukumbushana kule kule kunakoendelea endlessly kwa faida ya CCM na vibaraka wao.

Machi 21, 2023 palikuwa na uzi huu wenye maudhui haya haya:

Uchaguzi 2024/25 wa nini kama hakuna Katiba Mpya?

Kama waungwana hatuwezi logically kuendelea hivi milele hadi kurudi kwa Yesu Kristo.

Kinachopaswa kufanyika ni kuipeleka mijadala hii kunako ufumbuzi badala ya kuendekeza dua za kuku kila leo.
 
Na hao wapinzani watakaokubali utahira huo ndio viini macho vya vyama mbadala... Wtz tunapaswa kupima nafasi ya vyama Kama chadema kupitia hili Jambo!. Kuna kila dalalili ya chadema kuwa "CCM B"
What? Wewe siyo mtanzania? Una-play part gani kwenye kupinga? Au unadhani kuna watu watakutafunia kila kitu? Watanzania bado kabisa. Tunadhani sisi hatuna mchango wowote kwenye mwelekeo wa siasa zetu.
 
brazaj labda inawezekana umechoka kuona tunaendelea tu na mijadala na "kulalamika" bila ya kuwepo Kwa Suluhu la jambo lenyewe.

Lakini hali hiyo imetokana na msingi uliowekwa na TANU na ASP na baadae CCM, msingi ulioweka kanuni ya kuamini zaidi mawazo na maoni ya viongozi dhidi ya watu wa kawaida.

Mpaka sasa watanzania wengi wanaamini kuwa suala la Katiba mpya ni suala la viongozi wa CHADEMA dhidi ya viongozi wa CCM.

Unapoona msomi kama Pasco anaongea mambo ya kuwa na shukrani kwa marekebisho ya Sheria za uchaguzi yatakayofanyika, jiulize watu wa mitaani wanawazaje??

Tatizo Kuu ninaliliona mimi ni uwezo mdogo wa watu wenye mawazo mbadala katika kubadili mawazo na mitizamo ya watanzania wengi kuhusu uwezo wao binafsi katika kuchagiza mabadiliko chanya kwa mustakabli wao na vizazi vijavyo.

Lugha inayotumika kuwasilisha hoja Kwa watanzania wa kawaida mara nyingi inaleta mikanganyiko isiyo na sababu na hakuna muendelezo wa hoja kwenye hiyo Agenda ya kulenda mabadiliko.
 
brazaj labda inawezekana umechoka kuona tunaendelea tu na mijadala na "kulalamika" bila ya kuwepo Kwa Suluhu la jambo lenyewe.

Mkuu imebidi nikujibu kwa urefu kama ulivyokuja:

Kuchoka si mimi tu bali pamoja na watanzania wengi, bila shaka wasiokuwa CCM au vibaraka wao (kwa kujua au kutokujua).

Lakini hali hiyo imetokana na msingi uliowekwa na TANU na ASP na baadae CCM, msingi ulioweka kanuni ya kuamini zaidi mawazo na maoni ya viongozi dhidi ya watu wa kawaida.

Ninadhani hata hao CCM wanafurahi sana tunapolitafuta tatizo letu kwao (au hata TANU) tukiliacha likiendelea kutula nguoni mwetu.

"Ukweli mchungu matatizo yetu tunayo sisi wenyewe."

Kwamba tumekuwa wagumu wa kutumia akili zetu kuchambua mambo? Kwamba tunataka nani kutuamulia sisi lililo jema au baya au nini tufanye?

Hapa ndipo umuhimu wa demokrasia unapokuja, tena across the board hadi vyamani huko. Kungeharibika vipi jambo penye wengi?

"Kwani beberu hadi akawa na primaries hakuyaona haya?"

Mpaka sasa watanzania wengi wanaamini kuwa suala la Katiba mpya ni suala la viongozi wa CHADEMA dhidi ya viongozi wa CCM.

Hili si kweli hata kidogo. Tatizo letu ni ubinafsi. Vingine ni visingizio. Tumeshindwa kujifunza kote, hata ambako harakati kama hizi zimefanikiwa au zinashika kazi.

"Kutokuwa na maadui wa kudumu wala marafiki wa kudumu bali agenda, kumeshindwa kueleweka."

Agenda inaweza kuizidi mashiko agenda ya kupata katiba mpya kiasi hata cha kutaka kuiweka rehani, kwa mfano?

Unapoona msomi kama Pasco anaongea mambo ya kuwa na shukrani kwa marekebisho ya Sheria za uchaguzi yatakayofanyika, jiulize watu wa mitaani wanawazaje??

Binafsi nina matatizo na bwana Pasckali kwenye kuuma na kupulizia tu. Japo kiutu uzima ninadhani anafanya hivi kutokana na kuwa ameng'amua kwa mwendo huu, hatutoboi leo.

"Kwamba labda kaamua kumtumikia kafiri apate mradi wake (angalau kwa muda)."

Ni mawazo yangu kuwa bila shaka kukitokea serious movement yenye kuonyesha uelekeo ulio bayana kabisa, anaweza kuwa siyo huyu tunayemwona.

Pia kwenye struggle tusipende kusikia tunayopenda tu. Wakosoaji ndiyo wanao shape uelekeo.

Kumsoma Paskali, ukae uvute fundo kama wala muwa, yakhe. Vinginevyo utamtakia heri na teuzi ambazo kwa hakika akitunukiwa hatakataa na pia labda hatakuwa kama kina nani hii ..

Tatizo kuu ninaliliona mimi ni uwezo mdogo wa watu wenye mawazo mbadala katika kubadili mawazo na mitizamo ya watanzania wengi kuhusu uwezo wao binafsi katika kuchagiza mabadiliko chanya kwa mustakabli wao na vizazi vijavyo.

Sidhani ndugu. Nionavyo tatizo hapa ni kukosekana kwa demokrasia ya kutosha kuhakikisha mawazo na watu walio bora kabisa tunaoweza kuwa nao, wako pote panapostahili.

"Dhana ya kuwa vyama hivi ni vya wanachama haiwezi kupuuzwa."

Lugha inayotumika kuwasilisha hoja Kwa watanzania wa kawaida mara nyingi inaleta mikanganyiko isiyo na sababu na hakuna muendelezo wa hoja kwenye hiyo Agenda ya kulenda mabadiliko.

Mkuu si lugha. Bali Kwa maoni yangu:

"Maneno matupu hayavunji mfupa."

Ni lazima uelekeo uwe ni vitendo:

IMG_20220927_190940_421.jpg

Habari ndiyo hiyo.
 
brazaj huwezi kuweka pembeni ufukarishaji mawazo uliofanywa na CCM kufikia hapa tulipo.

Ni kwa vipi hiyo "movement" mpya itakavyoweza kuzaliwa nje ya tamaduni zetu za kisiasa bila ya uwepo wa uasi wa kifikra??

Hawa kina Pasco wanaouma na kupuliza siyo watu wa kutegemeka hata kidogo.

Misimamo thabiti haijengwi na watu wenye hasira peke yake, bali na watu wenye uthubutu wenye malengo bayana na watu jasiri.

Bahati mbaya hatuwezi kufikia viwango hivyo bila ya kuwa na falsafa tunayoisimamia na kuipigania.

Kuchukia matendo ya CCM pekee hakutoi fursa ya kuwepo kwa hiyo "movement" unayoitamani.

Lakini pia tuna upungufu wa watu wa kuaminiwa uadilfu wao na wenye dhamira zisizotiliwa shaka kuwa wana malengo binafsi.
 
Ngoja brazaj nitoe kidogo mawazo yangu kwa mfano kuhusu njia mojawapo shinikizi, njia ya maandamano.

Kuna watu wanakurupuka tu kusema tufanye maandamano. Maandamano ni sanaa tena ni sayansi kwenye kuyaandaa kwake.

Huwezi kuwa na maandamano yatakayofanikiwa bila ya kuyapanga kisayansi na kuyahamasisha kisanaa.
 
brazaj huwezi kuweka pembeni ufukarishaji mawazo uliofanywa na CCM kufikia hapa tulipo.

Ni kwa vipi hiyo "movement" mpya itakavyoweza kuzaliwa nje ya tamaduni zetu za kisiasa bila ya uwepo wa uasi wa kifikra??

Hawa kina Pasco wanaouma na kupuliza siyo watu wa kutegemeka hata kidogo.

Misimamo thabiti haijengwi na watu wenye hasira peke yake, bali na watu wenye uthubutu wenye malengo bayana na watu jasiri.

Bahati mbaya hatuwezi kufikia viwango hivyo bila ya kuwa na falsafa tunayoisimamia na kuipigania.

Kuchukia matendo ya CCM pekee hakutoi fursa ya kuwepo kwa hiyo "movement" unayoitamani.

Lakini pia tuna upungufu wa watu wa kuaminiwa uadilfu wao na wenye dhamira zisizotiliwa shaka kuwa wana malengo binafsi.

Msingi wa mafanikio ni demokrasia tu:

1. Itatupa mawazo bora kabisa
2. Itatupa watu bora kabisa.
3. Itatupa uamuzi bora zaidi.

Mfano:

"Kutokuwa na maadui wa kudumu wala marafiki wa kudumu kutatokea wapi kwenye demokrasia?"

Mapambano yanataka watu wanaohesabika hata kama ni wachache siyo maneno matupu.

Tuwekeze kwenye mashirikiano si mafarakano.

Anayejipa mamlaka ya kutilia mashaka nani huyo? Tuachane na ramli chonganishi hizi ambazo aghalabu ni kwa manufaa ya CCM.

Mengine ni visingizio tu ndugu.
 
Back
Top Bottom