Tanzania Tuitakayo competition threads

joeKendrick

New Member
Mar 2, 2024
2
6
Tanzaniani tuitakayo ya miaka 5 hadi 25 ni ile ambayo kwanza tukubali kuanda kizazi Bora kutoka chini ambacho kitakuwa kimeandaliwa katika Mfumo mzuri wa elimu, Siasa , uzalendo, na teknoljia ambayo itaendana mahitaji ya Dunia ya sasa kivipi?

Katika Mfumo wa elimu tunahitaji kuona mabadiliko kutokea yatakayo kuwa na athari katika siku za usoni kwa wanafunzi wenyewe na taifa kiujumla kwa kuanza kuanda wanafunzi ambao wanauelewa na ufaham kuhusu mifumo mbali mbali ya kama vile ujuzi wezeshi katika masuala ya uchumi na fedha lazima toka chini taundae watu wanajua Kodi nini inapatikanaje kodi umhimu wa kulipa Kodi ni kwa ajili ya maendeleo ya taifa hivyo toka chini tutaanza kuona matokeo katika suala zima la usimamizi wa fedha, uchumi, na vile itolewe elimu sahihi ya fedha kwani hiyo italeta tija hata mwanafunzi anapokuwa kahitimu masomo tayari anao uelewa katika suala zima la fedha hii italeta athari chanya katika usimamizi wa mzuri wa fedha kwa kuwa tayari ana elimu katika nyanja hiyo kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja, familiya hadi taifa.

Katika nyanja ya Siasa na utwala bora ni lazima tuandae vijana wazalendo kwa taifa letu kwa kuleta kupata elimu sahihi katika kumjengea mtazamo thabiti katika uongozi bora Siasa yenye tija na yenye athari chanya kwa taifa letu kwa kubadili mifumo ambayo sio rafiki kwa mtanzania kiujumla katika suala zima la utawala bora Siasa kwani hapo ndipo penye changamoto kubwa na athari katika kujenga au kuharibu dira ya taifa na raia wake kiujumla.

Mfumo wezeshi na shirikishi kati ya wanchi na serikali, mara nyingi kumekuwa na gape kubwa kati ya serikali na wananchi katika kufanya maamuzi kwa kuegemea upande Mmja peke yake ambao kiuhalisia ni serikali yenyewe imekuwa na utaratibu wa kufanya bila kushrikisha wananchi na hivyo kupelekea kuwepo na migogoro baina ya serikali na wananchi ambapo serikali huwa unafanya maamuzi bila kujali maoni ya wananchi kwa kisingizio Cha kuwa bunge linawakilisha ambayo huwa ni sehemu ndogo sana ya uwakikirishi ukilinganisha na wananchi wote, hii inapelekea kuwepo mvutano wa pande hizi mbili na hivyo kupoteza dira ya taifa na kucheleweshwa kwa maendeleo na huduma kwa wananchi ambao ndo taifa lenyewe. Hivyo kuwepo Mfumo thabiti wa kuunganisha wanchi na serikali itachangia kuleta maendeleo katika taifa na kupelekea kuboresha huduma kwa kila mtanzania na sio kuegemea upande mmoja tu. Katika dhana hii basi mifumo pendekezi ni kama ifuatavyo

Kuwepo na mfumo wa kielektroniki tambuzi na mahususi kwa ajili ya kukusanya maoni ya wanchi kwa serikali yao na sio kuegemea bunge peke yake kufanya maamuzi.

bunge kama chombo cha kutunga sheria lipitishe ambayo imezingatia maoni ya wananchi yaliyotoka katika mfumo data wa wanchi kutolea maoni kwa kupiga kura kielektroniki.

Mwisho iwepo mamlaka tambuzi kwa ajili ya kusimamia maoni na mapendekezo ya wananchi kwa serikali mbali na bunge, na kazi ya bunge iwe ni kutunga sheria na kujadili kile kilicho pendekezwa na wanachi pamoja na kufanya thathimini ya maendeleo ya serikali kwa wanachi.
 
Mfumo wa elimu tunahitaji kuona mabadiliko kutokea yatakayo kuwa na athari katika siku za usoni kwa wanafunzi wenyewe na taifa kiujumla kwa kuanza kuanda wanafunzi ambao wanauelewa na ufaham kuhusu mifumo mbali mbali ya kama vile ujuzi wezeshi katika masuala ya uchumi na fedha lazima toka chini taundae watu wanajua Kodi nini inapatikanaje kodi umhimu wa kulipa Kodi ni kwa ajili ya maendeleo ya taifa hivyo toka chini tutaanza kuona matokeo katika suala zima la usimamizi wa fedha, uchumi, na vile itolewe elimu sahihi ya fedha kwani hiyo italeta tija hata mwanafunzi anapokuwa kahitimu masomo tayari anao uelewa katika suala zima la fedha hii italeta athari chanya katika usimamizi wa mzuri wa fedha kwa kuwa tayari ana elimu katika nyanja hiyo kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja, familiya hadi taifa.
Toka chini mpaka juuu, sawa sawia.

Mwisho iwepo mamlaka tambuzi kwa ajili ya kusimamia maoni na mapendekezo ya wananchi kwa serikali mbali na bunge, na kazi ya bunge iwe ni kutunga sheria na kujadili kile kilicho pendekezwa na wanachi pamoja na kufanya thathimini ya maendeleo ya serikali kwa wanachi
Yas, mfano hilo shindano la stories of change. Ni eneo ambalo wabunge na hata usalama wa taifa unaweza kuweka kama moja ya vyanzo vya mapato... sorry🤫 taarifa za kujenga Tanzania tuitakayo
 
Back
Top Bottom