Ukweli utakuweka huru. Ukimbie unafiki, msema kweli ni mpenzi wa Mungu.....
Rais Nyerere akakemea sana ikabidi upewe wewe Seif kuwa waziri kiongozi na Ali Hassani Mwinyi kuwa rais wa Zanzibar.
........
Leo tunashangaa baada ya kufutwa matokeo ya Zanzibar mnataka eti serikali ya muungano waingilie matatizo ya uchaguzi Zanzibar.
Maalim Seif hesabu zako kwa kutaka kutawala Zanzibar bado zinafeli.
Tega sikio au fumbua macho na usome hapa:
“Nchi hii tumeheshimu unafiki kuliko ukweli kwa kusahau maadili na misingi. Ni lazima tukae kama Taifa na tukubaliane juu ya namna tutakavyoiongoza nchi yetu,” alisema.
Mgogoro Zanzibar
Kaduma aliungana na wadau wengine ambao wanapinga kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar kwa maelezo kuwa maridhiano baina ya pande zinazosigana yana nafasi nzuri ya kutatua mgogoro uliopo.
“Katika suala la Zanzibar nadhani CCM tungekubali kushindwa. Mimi ni mwanaCCM lakini nasema tungekubali kushindwa. Ningekuwa (Dk Ali Mohamed) Shein ningelinda heshima yangu maana hii ni hatari,” alisema.
Mzee Kaduma alisema kwa kuwa suala la Zanzibar ni baina ya vyama vya CCM na CUF, mtu pekee wa kutafuta ukweli ni mwenyekiti wa CCM.
“Rais mstaafu Jakaya Kikwete ndiye mwenye uwezo mkubwa wa kuweka mambo ya Zanzibar sawa maana yeye ndiye mwenyekiti wa CCM na suala lenyewe linakihusu CCM na CUF, ingawa kwa mbali sana Magufuli naye anaweza kufanya lolote kuondoa tatizo lililopo,” alisema.
Alisema anaamini CCM ingetenda haki kama ingepokea matokeo kama yalivyokuwa ambayo hata waangalizi wa ndani na nje wamesema hayakuwa na dosari.
“Ni vyema Rais Shein angekubali kushindwa. Chama pia kingefanya hivyo. Huko ndiko kujisahihisha. Kufanya hivyo Rais Shein angeondoka na heshima yake.”
Kama huamini wako watu wanaosema ukweli, Jisomee hapa: Link Kaduma: JPM arejeshe nyumba za Serikali